Haya ni maajabu 6 ya kahawa yanayowaduwaza wengi duniani

LUKAMA

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,081
1,271
Nb:Naomba mods kuheshimu thread za watu, kazi yenu isiwe kufuta au kuunganisha thread za watu, sometime mnakera kinyama

Dunia haijawahi kuwa na wasiwasi kuhusu kahawa.
Iwe tunakunywa kikombe kimoja cha kuamka asubuhi, espresso baada ya chakula cha mchana au cappuccino jioni, hatujawahi kutumia sana.
Mwaka 1991, matumizi ya kahawa duniani yalikuwa karibu mifuko milioni 90 ya kilo 60, kulingana na Shirika la Kimataifa la Kahawa (ICO).
Kufikia 2020/21, matumizi yanakadiriwa kuwa zaidi ya mifuko milioni 167. Kahawa ni nzuri lakini kunywa kwa tahadhari, na usinywe kiwago kikubwa kupita kiasi kutokana na kutajwa kwake kuwepo na madhara ya matumizi ya muda mrefu na ya kiwango cha juu.
Kwa hivyo kwa nini usichukua sasa kikombe chako cha kahawa unayopenda ukae mahaliu ukipumzika nili kusoma ukweli huu kuhusu kahawa ambao pengine umeusahau ama haujui?
1. Kahawa iligunduliwa na mbuzi huko Ethiopia
Kulingana na simulizi zilizopo, katika karne ya 9, mchungaji wa mbuzi anayeitwa Kaldi alikuwa akitazama kundi lake la mbuzi aliokuwa anawachunga likila tunda la mti wa ajabu na kugundua kuwa wanyama hao walikesha usiku kucha wakiwa wamejawa na nguvu.
Ethiopia inachukuliwa kuwa mahali palipogundulika kahawa na mila yake ya unywaji wa kahawa ni maarufu.
Aliliambia kundi la watawa kuhusu hilo, ambao walitambua kwamba wangeweza kugeuza tunda hilo kuwa kinywaji cha moto ili kukaa macho kwa ajili ya maombi.
2. Kahawa inaliwa na inanywewa
Watu wamekuwa wakinywa kahawa kwa muda mrefu, lakini wapo watu wengine wanapendelea kula kahawa.
Kahawa haitumiki kama kinywaji kila wakati: ilibadilishwa kuwa unga unga unaoweza kutumika kwa njia nyingi.
Kampuni zingine pia zimetumia mbegu za kahawa zilizopotea kutengeneza unga. Inaweza kutumika kutengenezea keki, mikate, chokoleti, michuzi, na kadhalika.
3: Awali kahawa ilijulikana kama divai.
Katika karne ya 15, kahawa ilikuzwa huko Yemen. Jina lake la asili, qahwah, linatokana na neno la Yemeni la divai.
Karne moja baadaye, ilikuwa tayari inajulikana katika maeneo ya Uajemi, Misri, Syria na Uturuki.

4. Kahawa yote duniani hukuzwa katika eneo maalumu linaitwa "ukanda wa kahawa"
Kahawa hulimwa katika nchi zaidi ya 50 zilizoko katika eneo linaloitwa "ukanda wa kahawa", Ni kutoka mashariki mwa Mexico hadi Papua New Guinea. Ukitazama kwenye ramani ni eneo linalotengeneza mkanda fulani kupitia nchi zinazolima kahawa. Hawa ndio wazalishaji wakubwa zaidi ulimwenguni: Brazil, Vietnam, Colombia, Indonesia, Honduras na Ethiopia
5. Watumiaji wakubwa wa kahawa duniani ni wafinland
Kulingana na ICO, Finland ndio wanywaji wa kahawa wakubwa zaidi kwa mtu mmoja moja duniani. Nchini Finland, kila mtu hunywa wastani wa kilo 12 za kahawa kwa mwaka.
Nchi inayofuata ni Norway (kilo 9.9 kwa kila mtu), Iceland (kilo 9), Denmark (kilo 8.7) na Uswidi (kilo 8.2). Kwa ujumla nchi za Scandnavia ndio wanaongoza duniani ingawa Waitaliano poia wako juu wao hutumia kilo 5.9 kwa kila mtu kwa mwaka
6. Vita ya kahawa na chai?
Jumuiya ya Kahawa ya Uingereza inasema kahawa ni "kinywaji maarufu zaidi duniani", na takriban vikombe bilioni mbili hutumiwa kila siku, lakini si rahisi hivyo kutokana na uwepo wa chai.
Nchi kubwa mbili zenye watu wengi zaidi duniani - China na India - hutegemea sana wa chai. Kahawa hutumiwa sana bara la Amerika na bara la Ulaya, ilhali kuna watu hupendelea chai katika nchi nyingi za Asia na uliokuwa Muungano wa Sovieti.
Mwanajiografia David Grigg wa Chuo Kikuu cha Sheffield nchini Uingereza alijaribu kutatua mzozo huu katika makala ya 2006 iliyochapishwa katika jarida la GeoJournal.
Kwa mujibu wa Grigg, ulinganisho huo lazima ufanywe kwa lita, kwa sababu ingawa ulimwengu hutumia takriban 80% ya kahawa zaidi ya chai kwa uzani kila mwaka, inachukua gramu mbili tu za chai kuandaa kikombe, ikilinganishwa na gramu 10 za kahawa.
Kulingana na hesabu hii, alihitimisha kuwa "vikombe vitatu vya chai vinatumiwa kwa kila kikombe kimoja cha kahawa".
 
Nilikua mnywaji sana wa kahawa. Lakini baada ya kugundua inaweza kusababisha hypertension kwa matumizi ya mda mrefu nimeona niachane nayo kwanza.
 
Kahawa ni ulevi kama ulevi mwingine, maana wakati natumia kahawa napata hasira, uchungu, na wasi wasi kumbe kahawa ndio ilikua inasababisha hayo yote kwa Sababu ilikua inaenda kufanya damu inaenda kasi. Nilipoamua kupumzika bila kahawa naweza kucheka tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kahwah ghali duniani ni ile inayokuja kama kinyesi cha paka na inajiunda kama kashata
images - 2022-04-30T175117.354.jpeg
 
Kula kahawa ushinde usilale ni uongo


Chuo kipindi cha ue nimezinywa sana ili nitoboe ozone lakini naishia kusinzia
Ulikuwa haunywi "kahawa", ulikuwa unakunywa "chai" ya kahawa.

Kuna matumizi aina mbili ya kahawa mitaani:
Kahawa inanywewa kama chai, yaani ikishasagwa ama ile ya paketi, huchukuliwa unga wake kidogo kuchanganywa na maji ama maziwa pamoja na sukari kutengeneza ladha ya kifungua kinywa.

Na kuna kahawa ambayo Concentration yake kubwa ikikorogwa katika maji hufanya ladha kuwa chungu kabisa na hiyo sasa ndiyo "kahawa" kuweza kukufanya ukeshe usiku kucha.

Kadri maji yanavyoongezwa kwenye chombo husika na concentration ya kahawa hiyo hushuka kama ilivyo kwa chumvi.

Kwa hiyo wewe hapo ulikuwa unakunywa kahawa kweli, lakini concentration yake ilikuwa ya chini.

Emb nenda leo mtaani kwa wauza kahawa, wakupondee unga wake ili ukaandae mwenyewe uone matokeo yake.

Koroga na kuongeza unga hadi iwe nzito kabisa, kisha chuja uonje kama ni chungu na inanata kwenye ulimi, hiyo ukitumia utakesha huku mnara umesoma 5G!
 
Ulikuwa haunywi "kahawa", ulikuwa unakunywa "chai" ya kahawa.

Kuna matumizi aina mbili ya kahawa mitaani:
Kahawa inanywewa kama chai, yaani ikishasagwa ama ile ya paketi, huchukuliwa unga wake kidogo kuchanganywa na maji ama maziwa pamoja na sukari kutengeneza ladha ya kifungua kinywa.

Na kuna kahawa ambayo Concentration yake kubwa ikikorogwa katika maji hufanya ladha kuwa chungu kabisa na hiyo sasa ndiyo "kahawa" kuweza kukufanya ukeshe usiku kucha.

Kadri maji yanavyoongezwa kwenye chombo husika na concentration ya kahawa hiyo hushuka kama ilivyo kwa chumvi.

Kwa hiyo wewe hapo ulikuwa unakunywa kahawa kweli, lakini concentration yake ilikuwa ya chini.

Emb nenda leo mtaani kwa wauza kahawa, wakupondee unga wake ili ukaandae mwenyewe uone matokeo yake.

Koroga na kuongeza unga hadi iwe nzito kabisa, kisha chuja uonje kama ni chungu na inanata kwenye ulimi, hiyo ukitumia utakesha huku mnara umesoma 5G!
Kahawa ni hatari sana kwa afya hususan wenye dalili za hbp. Kama ilivyo sigara, inatakiwa pia jamii ielimishwe kuhusu risk za kiafya za kahawa. Drink at your own risk.
 
Back
Top Bottom