Haya ni baadhi ya matatizo ya kuchaguliwa mchumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya ni baadhi ya matatizo ya kuchaguliwa mchumba

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by GM7, Nov 25, 2009.

 1. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kuna mwanadada mmoja ambaye ni miongoni mwa watu wasomi sana. Amemaliza chuo hapa mlimani. Wakati alipokuwa chuoni aliibahatika kupata mchumba ambaye walikubaliana kuoana. Na walikuwa katika maelewano mazuri katika uchumba wao,

  Baada ya uchumba wao huo kuendelea, aliamua kumpeleka kwa wazazi wake na kuwafahamisha kuwa mimi nimepata mtu ambaye naona atanifaa katika maisha yangu. Baada ya kuwafahamisha ishu hiyo, mama wa dada huyo alikubaliana na wazo lake la kutaka kuolewa na huyo mchumba wake lakina upande wa baba yake kulikuwa na shaka. Huyo binti alikuwa karibu sana na baba yake na aligundua kuwa baba yake hataki kukubaliana na wazo lake. Baada ya mazungumzo ya hapa na pale na baadaye mvulana yule kuondoka, binti alimfuata baba na kuzungumza naye na akasema kwa jinsi nilivyomuona huyo mvulana hakufai. Binti akamwambia si vizuri kumhukumu mtu kwa kumwangalia tu. Mimi nimekuwa naye kwa muda mrefu namfahamu vizuri sina shaka naye. Baba yake bado hakukubaliana na hilo lakini upande wa mama yake hakukuwa na shida.

  Uchumba uliendelea na yule mvulana akasema inaonesha baba yako hataki kabisa, lakini nitaumia sana endapo kama bado ataendelea na msimamo wake huo. Ni mtu ambaye nimekuzoea, tumeheshimiana sana. Yule binti akamwambia kila kitu kinawezekana na itawezekana tu.

  Siku moja yule binti akiwa katika mizunguko yake ya hapa na pale akiwa mjini, alikutana na kaka mmoja akiwa katika mavazi ya kijeshi, na alikuwa na mwonekano mzuri sana, lakini cha kushangaza yule kaka baada ya kumwona binti huyu aliduwaa. Baada ya kuduwa kwa kipindi aliamua kumfuata binti na kumsalimia na kumwuuliza kila kitu, na baadaye walianza kuwasiliana mawasiliano ya kawaida kabisa lakini mwanajeshi huyo alikuwa na mawazo tofauti, na ndipo siku moja akamweleza kuwa angetamani siku moja awe mke wake. Yule binti akamwambia hapana, mimi tayari nina mtu wangu na tunaheshimiana sana, akamwambia sawa. Kwa ni watu marafiki alimrudisha mpaka kwao, kumbe lengo lake yule kijana ni kutaka kujua binti anaishi wapi.
  Na ndipo siku hiyo yule kijana aliamua kwenda peke yake nyumbani kwa wazazi wa binti huyo na kukutana na baba yake (Baba wa binti). Na ndipo alipozungumza ukweli wa kile alichokiona na lengo lake ni lipi. Na mzee aliweza kumdadisi kijana na kumweleza kila kitu. Kwa wakati huo yule binti pamoja na mama yake walikuwa hawapo na binti aliporudi akamweleza akaelezwa na baba yake kuwa kuna kijana mmoja alikuja yuko hivi na hivi akanieleza kila kitu, nadhani huyo ndiye atakayekufaa. Binti akamwambia hapana, wewe ndiye umemuona na mimi itabidi nimuone. Baadaye yule mjeshi akaja wakazungumza.

  Baadaya ya mazunguzo marefu ya hapa na pale yule kijana mjeshi aliamua kuondoka, na kwa kuwa binti hakutaka kukorofishana na baba yake aliamua kukubaliana na mawazo yake na baadaye wakamwita tena kijana huyo mjeshi. Baadaye taratibu zote za kuoana na mjeshi huyo zikafanyika, kisha binti huyo alienda kwa mchumba wake wa kwanza na kumweleza yote yaliyotokea na kumrudishia pete ya uchumba waliyovishana hapo awali. Kijana huyo alisikitika sana kwa uamuzi aliouchukua lakini hakuwa na jinsi aliamua kufuata shinikizo la baba yake. Hatimaye baadaye yule binti aliolewa na mwanajeshi na ndoa ilifungwa kanisani.

  Baada ya tu ndoa kinachotokea sasa hivi ni kwamba kosa kidogo tu anaambulia kipigo ambacho hajawahi kukipata, kiasi kwamba inampelekea kumkumbuka yule wa kwanza ambaye walikuwa wakiongea naye kwa utaratibu kabisa.

  Ndipo baadaye binti (ambaye sasa ni mke wa mwanajeshi) akamtafuta yule mchumba wake wa kwanza na kumweleza kila kinachotokea. Lakini kijana huyo alijaribu kumweleza namna ya kufanya ili waendelee kuishi vizuiri na mme wake na kuzidi kumwombea ili waishi vizuri.

  Kwa wakati huu kijana huyo bado hajaoa na anamweleza binti huyo kuwa itachukuwa muda mrefu kwa sababu kwanza itabidi nikusahau wewe pili nikae chini nitulie tatu nijianze upya hivyo itachukuwa muda sana.

  Kikubwa zaidi ni kuwa binti huyo amekubali kuolewa na mwanajeshi kwa shinikizo la baba yake, lakini kinachoendelea ni kwamba kosa dogo tu anaambuliwa kipigo kisicho cha kawaida na kinachomuuma zaidi huyo dada ni kuwa siku walipotoka OUT walienda sehemu ile ile ambayo walikuwa wakienda na mvulana yule wa kwanza na hivyo kuumia zaidi.

  Sasa dada huyu anaomba mawazo, ushauri na maoni afanyaje?

  Kazi kwenu wana JF
   
 2. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mmh! Hii kali imekaa ki Danielle Steel!
   
 3. D

  Dally Kimoko Member

  #3
  Nov 26, 2009
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndoa haina maana upokee kipigo na kutulia tu..Kwa kweli walienda kanisani..kuifunga na arejee kanisani huko huko...akaseme na paroko/mchungaji wake amueleze hali anayokabiliana nayo.Me binafsi sina imani,subira na wala heshima na mume anae nyanyua mkono kumkung'uta mkewe.Ndoa is about sharing life.Si mmoja kumchapa makofi mwenzi wake kama mtoto wake(hali kadhalika,sina imani kumpiga mwana ni kumfunza).Na kama imefikia hapo basi hii si ndoa tena na nadhani anayefanya hivyo aliingia kwenye hiyo ndoa bila kujua maana yake ama anajaribu kuishi maisha yake ya ndoa kutokana na vile aliona wazazi wake ama wakubwa wake ambao alivutiwa na mtindo wao wa maisha.Had I been in that position...?Mmmhh!Hata nisingesubiria mtu anishauri...Maana this is ABUSE!!DOMESTIC ABUSE ya nguvu!!Wakati anasuburia humu...huyu mume anaweza mtwanga mahali pabaya hata haya maoni anayosubiria yasimfikie..Inasikitisha kuona kwamba hata katika maisha haya tunaishi leo bado kuna sehemu kubwa ya kinamama wanaishi katika maisha haya na wanaogopa kuongea!!.Kuna siku nilisoma article kwenye michuzi ina Mama Salma Kikwete kuhusiana na domestic abuse,na alitoa no ya simu kumtafuta .Ngoja nijaribu itafuta .Ntaiweka labda wataweza msaidia...Hii kitu ipo na wala asiionee aibu...She should speak out and get professional help pia...Maana mara nyingi sio physical abuse tu...it comes with psychological abuse.Wanafikia kuamini kuwa hawana thamani tena,akimwacha mumewe hamna atakaye mtaka.Na kikubwa hapo si kutoka kwa huyo na kufikiria nani atanitaka.Hiyo ni habari nyingine...you'll cross the bridge when you get there.For now...jisalimishe...nafsi yako.Sorry If I sound like I don't sympathise with her.I do...Ila kwa hasira mno.He married her not to use her as a punching bag.If he needed a punching bag why not join a boxing club.Dada pole sana...I personally wish I could help.Ila naomba kwanza ujisaidie kwa hili.Nobody should tell you ati haya ndiyo maisha ya ndoa.Hell no!Kuna matatizo...Ila si haya ya kutwangana bibi.Plse plse Get the hell out of there.Mungu akusaidie
   
 4. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Kuna wanaume bado tu wanapiga wake zao!! Huyo mdada ni educated lakini bado tu anakubali kupigwa,sasa elimu yake anaitumiaje hapo?
  .......Huyo mwanaume wala sio wa kuishi nae, aachane naye hata kama ni ndoa ya kanisa
  yeye aondoke tu, maana huyo ni mjeshi na wanajeshi ndio zao kupiga wanawake zao. Nimeshaona ndoa nyingi za wajeshi zinayumba kwa mtindo huu.
  ........Kama huyo mdada hajazaa na huyo mume kwa ushauri wangu bora aondoke tu, wanaweza hata kushauriwa na wazee lakini tabia ya huyu mume haiwezi kubadilika......ataendelea kumpiga tu.
  ........Ningekuwa mimi na hivi ninavyoogopa kupigwa ningemuacha zamani hata kama ni ndoa ya kanisa.
  Maisha yenyewe mafupi haya jamani, baada mtu upate raha ya ndoa kutoka kwa mumeo, mume tena anakupiga.Mume mpigaji wala sio mume bali ni karaha na mzigo kwa huyo dada.
   
 5. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wachangiaji kuwa kupiga mke/mme si vizuri na si tabia ya kiungwana.
  Ili kutatua tatizo, tutafute kwanza chanzo chake na ndipo ufumbuzi utakuwa wa kudumu. Mtoa habari anasema mke akifanya kakosa kadogo tu anaambulia kipigo; labda angetueleza kakosa hako ni kapi ili tumshauri mke namna ya kukaepuka.
  Pili inaonekana mke bado anamkumbuka sana yule mchumba wake wa zamani hadi inafikia yeye na mme wake walipotoka OUT kwenye sehemu ile ile aliyokuwa akienda na mchumba wa zamani, hujisikia kuumia zaidi!
  Kuumia huku kunaweza kuwa ni kumbumbuka mchumba wa zamani au/ na kufikiria mateso anayoyapata. Unajua kuna emotions fulani zinatokea involuntary. Kwa huyo mke kutomsahau mchumba wa zamani, inawezekana kuna kitu anakifanya bila kujua na hicho ndicho kinamuuma mmewe.
  Namshauri ajitahidi kusahau hayo ya zamani kwani sasa ameshaolewa. Wengi wamepitia maisha ya kuwa na wachumba lakini si wote ambao wachumba hao wa zamani/ wa kwanza waliolewa nao. Ebu nyote mliochangia mjihukumu wenyewe, mliwahi kuwa na wachumba wangapi na je hao wa mwanzo mwanzo si mliwaacha na mkaolewa na wengine?
  Sikubaliani na kipigo, na suluhu si kuachana na mme huyo haraka, bali kutafuta sababu ya makosa hayo madogo madogo na kuyaepuka, kwa sababu kama akiolewa na mtu mwingine na makosa hayo yakaendelea, mme mpya anaweza asipige, lakini akazusha na tabia nyingine mbaya zaidi kama uasherati nk. Kumbuka kama makosa yakiendelea kujitokeza, mme mpya atasema -kumbe ndicho kilichokuwa kinakusababishia kipigo!
  WENGI HAWASEMI ILA KATIKA NDOA KUNA MATATIZO MENGI NA NDIYO MAANA WATU HUSEMA NDOA NI KUVUMILIANA.
  Ndoa ni ya kwanza.
   
 6. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Kumbe unajua kuna matatizo katika ndoa, ila kwako wewe kutwangana hakuvumiliki. Je wewe unaweza kuvumilia matatizo yapi? Au waweza kuvumilia uasherati? Wewe waweza kuvumilia hili na mwingine hili!
  Tusikimbilie kuvunja ndoa haraka, tutafute chanzo cha hivyo 'vijikosa vidogo vidogo'
   
 7. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ukishakuwa na ndoa (at least from a christian point of view) siku zzote ni kuwa na mtazamo wa kusolve matatizo na si kuvunja ndoa unless ni issue kubwa sana, lakini si tofauti ndogondogo ambazo zinaweza kurekebiswa au kuvumilia, after all hakuna perfect human being.
   
 8. D

  Dally Kimoko Member

  #8
  Nov 26, 2009
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kutwangana kwangu na ndoa ni vitu visivyoendana kabisa...Anapomtwanga mwenzie anafaidika vipi zaidi ya ku-inflict maumivu?Inaonyesha ni jinsi gani huyu mtu ana upeo mdogo wa maisha,hamuheshimu na wala hampendi mwenza wake na ni jinsi gani analazimisha kile anachotaka kiwe,kitokee hata kwa kutumia nguvu.Sawaaa...kipo kinachosababisha yeye kuvurumusha mangumi....lakini hakihalalishi yeye kuvurumusha mangumi...na mnaposema avumilie...mbona huyo mwanaume hakuvumilia akaanza kurusha mangumi?Does this work one side only...Mwanamke akipigwa vumilie...mwanamme akikerwa arushe mangumi.Jamani...kuna kesi ngapi duniani humu zinatokea kila leo mwanamke anakungutwa hadi anakuja kufa???Kwa hayo mnayoyaita ya kuvumilia....Hii habari kubwa...tunaongelea uhai wa mtu...japo hajasema anakungutwa kiasi gani...lakini hilo hatulijui...na huyu jamaa anapoanza kutandika mangumi...none of us will be there kumsaidia huyu mwanadada.Jiweke kwenye mahali pa huyu dada...with the little info tulizopewa...Hayo ni maoni yangu...ni juu yake kuchekecha yale anayoona yanamfaa ayachukue...na yale yasiyo mfaa atatuachia.Kila mtu ana haki sawa ya kuchangia.Dada mungu akusaidie katika hili...uwe na uwezo wa kuchekecha maoni ya watu vyema kwa mafao na afya yako na familia yako.Before anything seriously worse happens to you.Wanaanzaga na vibao...mangumi...baadae wanavamia makubwa zaidi.
   
Loading...