Haya ni baadhi ya Majanga/ Mabalaa katika Ndoa.

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,357
11,503
1. Mama mkwe au wifi kujichukulia nafas ya mke ndani ya nyumba.sehem nyingine unakuta mpaka anapanga bajeti au pesa ya matumizi anataka aachiwe yeye. Unakuta mama mkwe au wifi anataka yeye ndo amwandalie mume chakula mezani au ampikie

2. Mama mkwe au wifi anataka yeye anachotaka ndo kifanyike. Wengine hufikia hata hatua ya kuwaadhibu watoto au kumfukuza mfanyakazi ikiwa hawajampenda.

3. Mama mkwe au wifi anataka kaka yake aoe mke mwingne amwache huyu ikiwa hawajampenda. Na nlishuhudia mama mmoja wa kutoka knjaro akishiriki kumwachanisha mtoto wake wa kiume na mke ambaye walishazaa watoto wakubwa tu wawili. Mama mkwe akawa hatak kukaa knjaro anajidai anaumwa ili aje dar.akija dar yeye ndo anaishika nyumba mkwewe anabak tu kama pambo. Kumbe hakutaka mwanawe aoe bint ambaye si mchaga.alifanikiwa kuwatenganisha

4. Mawifi huwa wanaamini wewe mke huna chako pale kwa kaka yao.wao ndo wanasauti zaidi. Hivyo hutaka kutawala na hata watoto wako,house gal wako watakuwa chini yao.huona wivu sana, huwa na uhasidi mioyoni mwao. Na wengine unaweza kuta miaka nenda rudi hawajaolewa au waliolewa wakaachika wanakuja au anakuja kuishi kwenu. Au pengine kamaliza chuo au shule ndo anakuja kutafutia kazi kwenu.

Ushauri: mwanaume mama yako akija kwako asikae zaidi ya week tatu kama hana tatizo then arud kwake. Dada zako wakija pia wasiweke kituo waje wasalimie waondoke. Na waambie kuwa pale ni nyumbani kwa mkeo. So kila wanachotaka wawasiliane na mkeo.ili mradi uwe na uhakika kuwa mkeo hawatesi au hamtesi dada yako.

Lakini kumbuka nyumban hapo unatakiwa uishi wewe na mkeo na watoto wenu basi. Wageni waje watembelee na warudi makwao.wasije nao wakaacha baba na mama zao wakaambatana nanyi.

Alamsiki.
 
Shida ya mwanamke akisha funga ndoa nitofauti na kabla.
Huwa wanatabia ya kujiami kabla halijatokea lakutokea na hapo ndo wanajiaribia kuwapa nafasi mawifi
 
Utakuwa jipu ww!!Tena inaonesha una wadharau ndg wa mmeo.

Cheza; utatumbuliwa ww badala ya wao. Kaa chonjo. Vijana wa 21C kuvunja ndoa ni sekunde 21 tu.
 
1. Mama mkwe au wifi kujichukulia nafas ya mke ndani ya nyumba.sehem nyingine unakuta mpaka anapanga bajeti au pesa ya matumizi anataka aachiwe yeye. Unakuta mama mkwe au wifi anataka yeye ndo amwandalie mume chakula mezani au ampikie

2. Mama mkwe au wifi anataka yeye anachotaka ndo kifanyike. Wengine hufikia hata hatua ya kuwaadhibu watoto au kumfukuza mfanyakazi ikiwa hawajampenda.

3. Mama mkwe au wifi anataka kaka yake aoe mke mwingne amwache huyu ikiwa hawajampenda. Na nlishuhudia mama mmoja wa kutoka knjaro akishiriki kumwachanisha mtoto wake wa kiume na mke ambaye walishazaa watoto wakubwa tu wawili. Mama mkwe akawa hatak kukaa knjaro anajidai anaumwa ili aje dar.akija dar yeye ndo anaishika nyumba mkwewe anabak tu kama pambo. Kumbe hakutaka mwanawe aoe bint ambaye si mchaga.alifanikiwa kuwatenganisha

4. Mawifi huwa wanaamini wewe mke huna chako pale kwa kaka yao.wao ndo wanasauti zaidi. Hivyo hutaka kutawala na hata watoto wako,house gal wako watakuwa chini yao.huona wivu sana, huwa na uhasidi mioyoni mwao. Na wengine unaweza kuta miaka nenda rudi hawajaolewa au waliolewa wakaachika wanakuja au anakuja kuishi kwenu. Au pengine kamaliza chuo au shule ndo anakuja kutafutia kazi kwenu.

Ushauri: mwanaume mama yako akija kwako asikae zaidi ya week tatu kama hana tatizo then arud kwake. Dada zako wakija pia wasiweke kituo waje wasalimie waondoke. Na waambie kuwa pale ni nyumbani kwa mkeo. So kila wanachotaka wawasiliane na mkeo.ili mradi uwe na uhakika kuwa mkeo hawatesi au hamtesi dada yako.

Lakini kumbuka nyumban hapo unatakiwa uishi wewe na mkeo na watoto wenu basi. Wageni waje watembelee na warudi makwao.wasije nao wakaacha baba na mama zao wakaambatana nanyi.

Alamsiki.

Naunga hoja 100% Hua nasema hiv ole wake mkwe anikatae kisa analeta habar za ukabila tu ntamnyoosha kwa dizain yyte ile yaan ntamchezea bonge la muvi ya kikorea labda nisibak nae nyumban kwang na hao mawifi wakithubutu kuingilia ndoa yang ntawaambia wakae mita 200.
 
Hayo yote hutokea iwapo mwanaume anakua amejaaliwa kutoboa(kiuchumi) especially kama katoka familia duni au ya kipato cha kawaida
 
Mke ambae yupo peace sana kwa wakwe na mawifi zake wapo pamoja kucheka na furaha kama ndugu au wazazi wake wa damu amefanikiwa kuimiliki ndoa.
Hata mume akisumbua anampelekea kesi mama mkwe tu moja kwa moja na mume hawezi kuwa na ujanja akiambiwa na mama yake mzazi.
 
Avatar yako inanitia hasiraaa...anyway nirudi kwenye mada ...HUO NI MTIHANI MKUBWA...Inabidi tu ufukuze mke kulinda heshima ya mama ila inauma sana . .
 
Mimi kwangu watatoka tuu. Hawawezi kuja kunitawala kwangu niwachekee tuu
 
"...tatizo sio wifi au mama mkwe,Tatizo ni mume kutokujua nafasi ya familia yake na familia yao..."
 
Mbna iko upande mmoja tu mashemej nao VIP kwa maana ya upande wa mke?
 
Mimi nimeoa ninaishi jirani na mama, yaani nyumba zetu ni kama mita 100 tu, ila nadiliki kusema kwamba mkewangu ndio pasua kichwa, wakija ndugu zake nyumbani muda wote ni kama sherehe ndani, akija Mama na ndugu zangu wengine ananuna bila sababu au anapoa sana kama anaumwa, ukimuuliza kwanini anafanya hivo anajibu 'basi tu' , so wakati mwingine wakezetu nao ni shida. Yaani mda wote wanajihami tu wanahisi ndugu wa mwanaume wabaya
 
Back
Top Bottom