Haya ni aibu kwa Mwema binafsi na Jeshi la Polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya ni aibu kwa Mwema binafsi na Jeshi la Polisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chief Isike, Oct 31, 2011.

 1. Chief Isike

  Chief Isike JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wakuu tutajadili sana utendaji mbovu wa askari wetu wa Jeshi la Polisi na upande mwingine tatizo la wananchi kutojua haki na wajibu wao...lakini katika hili la utendaji mbovu wa polisi, huwezi kumweka kando IGP Mwema. Wakati akiingia madarakani baada ya kuteuliwa na Shemejiye, Rais Kikwete, Watanzania wengi tulikuwa tukimwamini kutokana na rekodi yake ya utendaji kazi huko nyuma (of which ni kitu kizuri kupanda au kupandishwa cheo by merits) ambayo pia ilimfanya akaenda Interpol (wako makini hawawezi kuchukua mtu wa hovyo hovyo hivi tu). Lakini kwa kweli yanayoendelea sasa nchini, kama hili la mgogoro wa Arusha, ambako afande mdogo tu amekua na kazi ya kuwatia taharuki wananchi bila sababu yoyote na kwingine ambako polisi wamegeuka kuwa watoa roho, linadhihirisha UDHAIFU MKUBWA wa Afande Mkuu, Mwema na jeshi zima la Polisi la watu kama akina Kasala, Mtweve, Manumba, tehe tehe tehe, naomba kuwasilisha. Tuajdili kwa hoja na references ikibidi.
   
 2. Steven Robert Masatu

  Steven Robert Masatu Verified User

  #2
  Oct 31, 2011
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 2,393
  Likes Received: 728
  Trophy Points: 280
  narudi baadaye kidogo.
  ngoja waje nguli wa kuthink utasikia matusi yake watakayoshusha.

  bravooooooooooooooooo
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  Lile shangingi la milioni 280 analotembelea ndilo linalo mjaza ujinga unaopelekea uwezo wake wa kufikiria na kufanya maamuzi upungue.
   
 4. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  issue ya EPA ndio iliyomwondolea Mwema weledi. Kuanzia hapo amekua mtu asiejiamini tena kwani ni dhahiri dhamira yake imekuwa ikimsuta.
  .
   
 5. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2011
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Shemeji hiloooo!!!!!!!!!!!!!anaongoza Polisi kama ya mkwe wake.
   
 6. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mwema si mwema tena tangu abanange issue ya EPA kwa kusamehe watuhumiwa bila kuwafikisha mahakamani ilimuondolea sifa za kuongoza idara nyeti ya usalama wa raia kwani sasa ni uhasama na raia
   
 7. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ccm na mashangingi bwana!
  umenikumbusha zamani zile za 90s wakati katibu mkuu wa ccm kolimba (RIP) akikampeni ili mtukufu na mtukuka raisi wa awamu ya pili mheshimiwa sana alhaj (pbuh) AHM aongezewe kipindi cha tatu akiwabeza wale wabunge waliokuwa wanapinga ajenda hiyo alisema "mimi ninalo na wewe unalo, mtukufu raisi aongezewe muda". kwa kweli ccm na mashangingi ni oyeee!!
   
Loading...