Haya, Ngoma nzito

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,950
711
na Mwanne Mashugu, Zanzibar
TD

SAKATA la kuvunjika kwa mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mpasuko wa kisiasa Zanzibar, limechukua sura mpya, baada ya makada wa CCM Zanzibar kufufua ubao wa vijembe, ukiwa na ujumbe; ‘Hatutoi nchi, wala hatuli ukoka’.

Ubao huo mkubwa uliopo katika maskani kuu ya CCM Zanzibar, Mwembe Kisonge, Mtaa wa Michenzani, tangu kuanza kwa mazungumzo ya CCM na CUF, ulisitisha kutoa ujumbe wa maneno ya kisiasa yaliyokuwa yakiandikwa kila siku.

Tangazo hilo la kwanza kutolewa tangu kuanza kwa mazungumzo hayo, lilisababisha msongamano wa watu waliokuwa wanasukumana kulisoma na wenye magari kusimama ili kujua nini kilichoandikwa.

Eneo hilo la Kisonge mara kadhaa limekuwa la mapigano kati ya wafuasi wa CCM na CUF, na baadhi ya wakati askari wa kutuliza ghasia kulazimika kutumia nguvu kutuliza ghasia hizo.

Tangazo hilo limezidi kutia wasiwasi iwapo CCM ilikubali kwa dhati pendekezo la kuanzishwa kwa serikali ya mseto kama njia bora ya kumaliza mpasuko wa kisiasa visiwani humu.

Watu waliosikika wakitoa maoni yao baada ya kusoma bango hilo, walisema kuwa maneno yaliyoandikwa kwenye ubao huo yana uzito wake kwa vile wanachama wengi wanaokaa katika maskani hiyo ni watu wakubwa serikalini, na idadi kubwa ni maofisa wa Usalama wa Taifa.

“Mara nyingi ubao huu ukiandikwa inakuwa sio bure, kwa vile matukio mengi yaliyotokea yaliwahi kutabiriwa na Kisonge na hatimaye yakawa kweli,” alisema Abdulrahman Kombo wa Mtaa wa Rahaleo.

Kuhusu neno lililoandikwa katika ubao huo ‘Hatuli Ukoka’, liliopo katika ujumbe huo, mkazi mwingine wa Mtaa wa Michenzani alisema kwamba huenda linatokana na hatua ya wafuasi wa CUF kuwataka wakulima wa Kisiwa cha Pemba na wafanyabiashara wasilete mazao yao kisiwa cha Unguja.

Hata hivyo, Juma Ameir wa mtaa huo wa Michenzani alisema kwamba ujumbe uliopo katika ubao huo unaweza kusababisha kutofikiwa wito wa Rais Jakaya Kikwete wa kutaka pande mbili hizo zirudi katika meza ya mazungumzo.

Akizungumzia suala hilo, Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Salum Bimani, alisema kwamba kitendo hicho cha makada wa CCM Kisonge ni cha uchochezi na kusema ameshangazwa na vyombo vya dola kutochukua hatua yoyote hadi sasa.

“Kimsingi maneno yale yanakusudia CUF hata tukishinda uchaguzi hatupewi, lakini katika misingi ya demokrasia huwezi kuandika maneno kama hayo,” alisema Bimani.

Alisema CUF ilishafunga mjadala wa mazungumzo na CCM na kama Rais Kikwete anataka kupatikana ufumbuzi wa mpasuko wa kisiasa Zanzibar, basi awakutanishe Rais Karume na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, ili walimalize tatizo liliopo.

Wakati huo huo, mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar na kada wa CCM, Mohammed Raza, ametaka wazee wa Pemba waliokamatwa na kuwekwa mafichoni waachiwe huru kwa vile kosa la uhaini haliwezi kutendeka Zanzibar bila kuhusisha Jamhuri ya Muungano.

Alisema kitendo cha kuwakamata wazee hao kinaweza kuathiri hali ya mshikamano iliyojitokeza tangu vyama vya CCM na CUF kuanza mchakato wa mazungumzo ya kutafuta suluhu.

Raza alisema kwamba serikali lazima ikumbuke wazee waliotoa maoni hayo hawapo peke yao isipokuwa kuna watu wengine wako nyuma yao, na kwamba kuendelea kuwashikilia kunaweza kusababisha matatizo zaidi.

Hata hivyo, watu hao saba waliachiwa kwa dhamana jana na kusafirishwa hadi majumbani kwao huko Pemba.

Tambwe Hiza unapenda kurukia issue iliyochezewa usanii na chama chako(SISIEMU). Haya sasa say something about hao makada wenu wanaohatarisha amani kwa POSTER yao.

Kamanda Mwema una kazi kweli kweli. Acha double standard, wananchi wanansubiri kuona action on those SISIEMU's KADAZ. Polisi mnadai hao wanan-CUF mliowaachia kwa dhamana wanachochea uvunjwaji wa AMANI so what about hao jamaa wa Mwembe Kisonge wana kusudi gani na ubao wao? Na inaaminika kuwa maeneo hayo wanaishi maofisa wa Usalama wa Taifa, sasa wanasubiri ushahidi gani au wanahitaji BIG LENS kuona huo ubao. Jamani tusirudi kwenye enzi za Salmin, tukatae kabisa hilo.
 
Halafu cha ajabu ni kwamba Mwenyekiti wa Chama msanii JK amekaa kimya kuhusu bango hilo linaloashiria amani ya Tanzania. Nakumbuka Slaa alipotaja viongozi wa juu serikalini ambao ni mafisadi, msanii alikuwa mstari wa mbele kudai upinzani unataka kusababisha umwagaji damu nchini kwa kutoa tuhuma zisizo na ukweli, lakini hili limetoka miongoni mwa wanaccm anafanya kama hakulisikia.
 
Yaaani unataka JK aende kufuta hayo maandishi kwenye maskani ya Kisonge?

Akiwa kama Mwenyekiti na CCM na Rais wa Tanzania inabidi akemee kwa nguvu zake zote matamshi/maandishi kama hayo yanayoweza kusababisha umwagaji wa damu.

Usiniwekee maneno ambayo sikuyaandika. Wapi nilipoandika kwamba ninataka akayafute maandishi kwenye mabango hayo? :confused:
 
..hilo jambo linaonekana kubwa sana huko unguja.

..huku bara,hayo huyaita maneno ya mtaani.
 
Akiwa kama Mwenyekiti na CCM na Rais wa Tanzania inabidi akemee kwa nguvu zake zote matamshi/maandishi kama hayo yanayoweza kusababisha umwagaji wa damu.

Usiniwekee maneno ambayo sikuyaandika. Wapi nilipoandika kwamba ninataka akayafute maandishi kwenye mabango hayo? :confused:
Kwa taarifa tu Kisonge ni moja ya Maskani nyingi za CCM hapo Zenj, na kwenye maskani mengi yanazungumzwa na kujadiliwa. Maskani hiyo sio wasemaji wa CCM, hivyo kumtaka JK kwenda kufuta maandishi hayo sio sahihi.
 
na Mwanne Mashugu, Zanzibar
TD

SAKATA la kuvunjika kwa mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mpasuko wa kisiasa Zanzibar, limechukua sura mpya, baada ya makada wa CCM Zanzibar kufufua ubao wa vijembe, ukiwa na ujumbe; ‘Hatutoi nchi, wala hatuli ukoka’.

Ubao huo mkubwa uliopo katika maskani kuu ya CCM Zanzibar, Mwembe Kisonge, Mtaa wa Michenzani, tangu kuanza kwa mazungumzo ya CCM na CUF, ulisitisha kutoa ujumbe wa maneno ya kisiasa yaliyokuwa yakiandikwa kila siku.

Tangazo hilo la kwanza kutolewa tangu kuanza kwa mazungumzo hayo, lilisababisha msongamano wa watu waliokuwa wanasukumana kulisoma na wenye magari kusimama ili kujua nini kilichoandikwa.

Eneo hilo la Kisonge mara kadhaa limekuwa la mapigano kati ya wafuasi wa CCM na CUF, na baadhi ya wakati askari wa kutuliza ghasia kulazimika kutumia nguvu kutuliza ghasia hizo.

Tangazo hilo limezidi kutia wasiwasi iwapo CCM ilikubali kwa dhati pendekezo la kuanzishwa kwa serikali ya mseto kama njia bora ya kumaliza mpasuko wa kisiasa visiwani humu.

Watu waliosikika wakitoa maoni yao baada ya kusoma bango hilo, walisema kuwa maneno yaliyoandikwa kwenye ubao huo yana uzito wake kwa vile wanachama wengi wanaokaa katika maskani hiyo ni watu wakubwa serikalini, na idadi kubwa ni maofisa wa Usalama wa Taifa.

“Mara nyingi ubao huu ukiandikwa inakuwa sio bure, kwa vile matukio mengi yaliyotokea yaliwahi kutabiriwa na Kisonge na hatimaye yakawa kweli,” alisema Abdulrahman Kombo wa Mtaa wa Rahaleo.

Kuhusu neno lililoandikwa katika ubao huo ‘Hatuli Ukoka’, liliopo katika ujumbe huo, mkazi mwingine wa Mtaa wa Michenzani alisema kwamba huenda linatokana na hatua ya wafuasi wa CUF kuwataka wakulima wa Kisiwa cha Pemba na wafanyabiashara wasilete mazao yao kisiwa cha Unguja.

Hata hivyo, Juma Ameir wa mtaa huo wa Michenzani alisema kwamba ujumbe uliopo katika ubao huo unaweza kusababisha kutofikiwa wito wa Rais Jakaya Kikwete wa kutaka pande mbili hizo zirudi katika meza ya mazungumzo.

Akizungumzia suala hilo, Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Salum Bimani, alisema kwamba kitendo hicho cha makada wa CCM Kisonge ni cha uchochezi na kusema ameshangazwa na vyombo vya dola kutochukua hatua yoyote hadi sasa.

“Kimsingi maneno yale yanakusudia CUF hata tukishinda uchaguzi hatupewi, lakini katika misingi ya demokrasia huwezi kuandika maneno kama hayo,” alisema Bimani.

Alisema CUF ilishafunga mjadala wa mazungumzo na CCM na kama Rais Kikwete anataka kupatikana ufumbuzi wa mpasuko wa kisiasa Zanzibar, basi awakutanishe Rais Karume na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, ili walimalize tatizo liliopo.

Wakati huo huo, mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar na kada wa CCM, Mohammed Raza, ametaka wazee wa Pemba waliokamatwa na kuwekwa mafichoni waachiwe huru kwa vile kosa la uhaini haliwezi kutendeka Zanzibar bila kuhusisha Jamhuri ya Muungano.

Alisema kitendo cha kuwakamata wazee hao kinaweza kuathiri hali ya mshikamano iliyojitokeza tangu vyama vya CCM na CUF kuanza mchakato wa mazungumzo ya kutafuta suluhu.

Raza alisema kwamba serikali lazima ikumbuke wazee waliotoa maoni hayo hawapo peke yao isipokuwa kuna watu wengine wako nyuma yao, na kwamba kuendelea kuwashikilia kunaweza kusababisha matatizo zaidi.

Hata hivyo, watu hao saba waliachiwa kwa dhamana jana na kusafirishwa hadi majumbani kwao huko Pemba.

Tambwe Hiza unapenda kurukia issue iliyochezewa usanii na chama chako(SISIEMU). Haya sasa say something about hao makada wenu wanaohatarisha amani kwa POSTER yao.

Kamanda Mwema una kazi kweli kweli. Acha double standard, wananchi wanansubiri kuona action on those SISIEMU's KADAZ. Polisi mnadai hao wanan-CUF mliowaachia kwa dhamana wanachochea uvunjwaji wa AMANI so what about hao jamaa wa Mwembe Kisonge wana kusudi gani na ubao wao? Na inaaminika kuwa maeneo hayo wanaishi maofisa wa Usalama wa Taifa, sasa wanasubiri ushahidi gani au wanahitaji BIG LENS kuona huo ubao. Jamani tusirudi kwenye enzi za Salmin, tukatae kabisa hilo.

INDUME YENE hiyo hoja ya bango wala haina tatizo lolote ispokuwa kwa wakaereketwa wa CUF ndiyo ina Impact kwa sababu wao wanataka kutawala nchi tu na si vinginevyo huwezi ukalinganisha kauli za kujilipua na kauli hiyo ya kusema hatutoi nchi kwamba zinalingana hata kidogo na tena hiyo kauli imetolewa na maskani wakati kauli y CUF imetolewa kwenye mkutano wa hadhara tena mbele ya viongozi wa kitaifa kuna tofauti kubwa
 
Jamani, jamani, ifike mahali tujieshimu, CCM jaribuni kulimaliza hili tunakwenda pabaya jamani, amani yetu itachukuliwa jamani, lakini ccm mtakuwa responsible kwa hili, haiwezekani kumwagiana mchanga machoni huku mkicheka, hii ni hatari ndugu zangu.
 
Kibunango ukereketwa wako umezidi hebu twambie una maslahi gani katiaka hichi Chama Cha Mafisadi (CCM) pengine nitakuelewa.
Tatizo mmezidi sana na kuitafuta hiyo CCM, mpaka maneno ya kwenye maskani mnayapa Headline kwenye front page za magazeti yenu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom