Haya ndo maneno yangu ya mwisho kwake siku ya kesho namaliza mchezo kabisa

Richson16

Member
Jul 2, 2017
37
13
Nikiwa nae sehemu tulivu nitaanza kumwambia maneno haya:

"Kipindi tulipokuwa pamoja tulikuwa kama marafiki tulishirikiana katika mambo mbalimbali, inawezekana kuna sehemu nilikukwaza kwa namna moja au nyingine lakini nataka ujue kwamba siku zote nilikupenda kwa dhati japo pamoja na kuonesha upendo wangu katika urafiki wetu lakini kwangu upendo huu ulikuwa ni zaidi ya urafiki".

Nitahema kwanza ndani kwa ndani then,"jua ya kwamba upendo wangu ni zaidi ya sisi kuwa marafiki, natumaini ya kwamba sasa ndo muda sahihi wa mimi kukwambia kuliko muda wowote ule, naomba unikubalie niwe wako siku zote ikiwezekana mpaka tuwe mume na mke".

Nakupenda sana "M" zaidi ya unavyofikiria natumaini wewe ndo nuru na taa yangu siku zote za maisha yangu.

Maoni yako kama naweza kurekebisha mstari wowote au niongezee nini wadau?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikiwa nae sehemu tulivu ntaanza kumwambia maneno haya:

"Kipindi tulipokuwa pamoja tulikuwa kama marafiki tulishirikiana katika mambo mbalimbali, inawezekana kuna sehemu nlikukwaza kwa namna moja au nyingine lakini nataka ujue kwamba siku zote nlikupenda kwa dhati japo pamoja na kuonesha upendo wangu ktk urafiki wetu lakini kwangu upendo huu ulikuwa ni zaidi ya urafiki"
Ntahema kwanza ndani kwa ndani then,

"Jua ya kwamba upendo wangu ni zaidi ya sisi kuwa marafiki, natumaini ya kwamba sasa ndo muda sahihi wa mimi kukwambia kuliko muda wowote ule, naomba unikubalie niwe wako siku zote ikiwezekana mpaka tuwe mume na mke" .....

nakupenda sana M zaidi ya unavyofikiria natumaini wewe ndo Nuru na taa yangu siku zote za maisha yangu.

Maoni yako kama naweza kurekebisha mstari wowote au niongezee nini wadau??

Sent using Jamii Forums mobile app


Huyo ni lazima akupotezee, usifanye kosa la kumwambia Mwanamke maneno kama hayo, atakuona dhaifu, cha kufanya siku zote wewe sex naye tu na uhskikishe unampe Game fresh na usiongelee mambo ya mahusiano hiyo ni kazi ya Mwanamke siyo yako, hivyo usithubutu na kama ukipuuzia ushauri wangu mwambie hayo maneno hlf uone baada a muda utarudi hp kama wenzako kulalamika na kutukana Wanawake baada ya kupigwa chini!

Wee kula good time naye tu hlf yeye mwenyewe atakuuliza vp tunaelekea wapi kimahusiano!
 
Back
Top Bottom