singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
Evarist Chachali
Kwa huko nyumbani, ninabashiri kuwa Rais Dk John Magufuli ataendelea na utumbuaji majipu, japo habari ninayobaishiri kuwa itatawala zaidi ni kuibuka kwa skandali mbalimbali zilizojitokeza wakati wa utawala wa Rais Jakaya Kikwete na ambazo umma haukuwahi kuzifahamu. Kimsingi, harakati za Dk. Magufuli kutumbua majipu zina kila ishara ya kukutana na madudu yaliyosheheni wakati wa utawala wa mtangulizi wake.
Kadhalika, ninabashiri uwezekano wa baadhi ya mawaziri au manaibu wao kufukuzwa kwa kushindwa kuendana na falsafa ya Hapa Kazi Tu. Kwa vile si vema kumwombea mtu mabaya, ninahifadhi majina ya mawaziri ninaodhani wanaweza kuwa waathirika wa awali.
Vile vile, ninabashiri uwezekano wa kuwepo jitihada za chini chini ndani ya CCM kukwamisha dhamira ya Dk. Magufuli kukabiliana na ufisadi, rushwa, ujangili, biashara ya dawa za kulevya, na maovu mengine. Hata hivyo, jitihada hizo hazitafanikiwa.
Kwa upande mwingine, ninabashiri kuwa Dk. Magufuli ataendelea kunga’ra ndani na nje ya nchi, na dunia itaelekeza macho yake nchini Tanzania kutokana na mafanikio makubwa ya kiuongozi na jitihada za kufufua na kuboresha uchumi.
Kingine ninachoweza kubashiri ni ujio wa sura mpya nyingi katika uongozi ngazi za mikoa na wilaya, huku ikitarajiwa kuwa kama ilivyokuwa kwa Baraza la Mawaziri na Makatibu wakuu, wasomi mbalimbali wakiteuliwa kushika nyadhifa za u-RC na u-DC.
Kwa upande wa vyama vya upinzani, ninabashiri uwezekano wa jitihada za kumng’oa Mwenyekiti wa taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, japo haitakuwa jambo la kushangaza iwapo atanusurika. Kwa kiasi kikubwa, uhai wa kisiasa wa Mbowe utategemea uhusiano wake na aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Ukawa, Edward Lowassa.
Eneo ambalo ninashindwa kubashiri kwa uhakika ni hali ya kisiasa huko Zanzibar. Hata hivyo, ninaweza kubashiri bila uhakika kuwa CCM itafanikiwa kulazimisha marudio ya uchaguzi, na kuna uwezekano CUF wakasusia. Uwezekano mwingine ni kurejewa kwa kilichofanyika baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, yaani kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.
Ubashiri sio sayansi timilifu (exact science) kwa hiyo nitahadharishe kuwa baadhi ya niliyobashiri yanaweza kuwa kinyume. Ubashiri huu umetokana na kufuatilia kwa karibu siasa za kimataifa na za huko nyumbani.
Nimalizie makala hii kwa kuwatakia tena heri na baraka za mwaka mpya 2016. Kwa huko nyumbani (Tanzania), kuna kila sababu ya mwaka huu kuwa mzuri kutokana na dalili za awali za utawala wa Dk. Magufuli kuiondoa Tanzania yetu katika lindi la ufisadi na rushwa, vitu vilivyochangia mno kudumisha umasikini wa nchi yetu. Lakini ili afanikiwe, ni wajibu wa kila Mtanzania kutimiza ‘Hapa ni Kazi Tu’ kwa vitendo.
Raia Mwema