Haya ndiyo yatakayoiua CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya ndiyo yatakayoiua CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kigarama, Nov 11, 2009.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2009
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kila mara inaonekana kana kwamba CHADEMA inakwenda kusambaratika, mara zote hizo ni bahati tu ya mtende inayokinusuru chama hicho kusambaratika. Ndani ya CHADEMA kuna mambo makubwa MATATU yanayokisumbua chama hicho.

  Mosi: Katiba yao
  PILI: Kujaza wasomi wasio wanasiasa
  TATU: Oganizesheni mbovu makao makuu.

  Kwa maoni yangu siyo Mbowe, Zitto wala Slaa bali ni haya mambo matatu ndiyo yatakayoiua CHADEMA.

  KATIBA YA CHADEMA

  Katiba hii ilipitishwa na Mkutano mkuu wa CHADEMA pale kwenye ukumbi wa PTA mwaka 2006. kwenye katiba hii mamlaka makubwa yaliwekwa kwenye mikono ya mwenyekiti na katibu wake na kurugenzi watakazo ziteua.

  wakati wa kuipitisha katiba hii kwenye Baraza kuu la wakati huo wajumbe walitahadharisha kwamba mfumo wa katiba hii utaviza chama. Kina kafulila na wenzake Mnyika ndiyo walikuwa vinara wa kuitetea Katiba hiyo.

  Wajumbe walimtahadharisha Mwenyekiti kwamba kuondoa ngazi ya kiutendaji ya Mkoa na kuibakisha kama ni ngazi ya kuratibu tuu bila ya kuipa nguvu ya kusimamia ngazi za Wilaya ni kuviza chama kina Danda walikuja Juu.

  Kilichoonekana wakati ule ni watu wa makao makuu (Danda, Mnyika,Kafulila) kuogopa nguvu kubwa walizokuwa nazo viongozi wa mikoa kwenye vikao vya Baraza Kuu.

  katiba hiyo iliwaondoa viongozi wa mikoa kuwa wajumbe wa Baraza kuu badala yake wakaingizwa viongozi (wenyeviti) wa wilaya kuwa wajumbe wa baraza hilo.

  Matoke ya hali hiyo mpaka sasa hakuna kikao chochote kile cha kitaifa ambacho Makatibu wa Mikoa wa CHADEMA ambacho wao ni wajumbe. Au kwa maneno mengine Makatibu wa CHADEMA wa mikoa hawatakutana kisheria kwa miaka mitano mfululizo wakiwa ni watendeji wa chama hicho ngazi ya mkoa.

  makatibu huchaguliwa na mikutano ya ngazi zao lakini huthibitishwa na baraza Kuu,chombo ambacho mpaka sasa hakijawathibitisha makatibu hawa waliochaguliwa mwaka huu. Na idadi kubwa ya makatibu wa Mikoa hawajahudhuria mkutano mkuu wa mwaka huu wa CHADEMA kwa sababu wao si wajumbe.

  Katiba hii ndiyo ilisanifiwa na kina Mnyika, Kafulila na wenzao ambao leo hii wanalialia kwamba wameonewa. Imekuwa Mchimba kisima kaingia mwenyewe!!

  WASOMI WASIO WANASIASA

  Hili ni tatizo linatakalo watafuna sana CHADEMA, kwani kila jambo badala ya kutatuliwa kiuhalisia zinaingizwa nadharia za kiusomi. Sina maana kwamba kwenye siasa hatuhitaji wasomi, la hasha, bali tunahiktaji wasomi wanasiasa.

  OGANIZESHENI MBOVU

  Kutokana na Katiba yenye Utata na wasomi wasio wanasiasa, Chama cha CHADEMA kimekuwa na Oganezesheni mbovu kupita Kiasi.Pale makao makuu kila mtu anatumia rasirimali za chama kujenga chama kwenye maeneo yao wanayotoka kwa lengo la kugombea ubunge.

  Kafulila wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa alikuwa Kigoma, Komu Moshi, Danda Njombe, Slaa Karatu, Kigaila Kibaigwa,Mdee kawe na hivyo chama kukosa Oganezesheni ya kitaifa kwa ajili ya uchaguzi huo.
   
 2. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Katiba haina tatizo ila uwezo wa mwenyekiti ndio tatizo
   
 3. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Ngoja niipitie katiba yao niweze kucomment, though sikubaliani na wewe na point namba 2. Labda ufafanue usomi kwako una maana gani??
   
 4. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #4
  Nov 11, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Ni uwoga wa kuwajibishana kwa sababu ya umashuhuri wa Mtu katika CHAMA, LAZIMA ifike mahali kuwe na nidhamu thabiti na sikuogopana na kuoneana haya.

  CHADEMA inaonyesha mfano wa kulinda nidhamu na maadili, lazima watu waheshimu vikao na maamuzi ya chama. hii si CCM ya watu kutukanana kisa kutetea ufisadi, huku ni nidhamu bila haya wala aibu.

  HONGERA CHADEMA
   
 5. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #5
  Nov 11, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  CHADEMA ilikufa pale utawala wa wa juu ulipomzuia Zitto kabwe asigombee kuwa mwenyekiti wao

  umesahau pia kuna UKABILA wa hali ya juu kwenye utawala wao

  bila kusahau allegations kuwa chama kina sura ya KIFAMILIA au kwa maneno mengine kinaonekana kama pet ya family ya EDWIN MTEI na FREEMAN MBOWE

  Its sad walivyomfanyia Zitto simply kwa kutazama undugu badala ya maslahi ya chama

  Hilo la USOMI habu tupumzishe kwani tunajua fika kuwa CHADEMA na washabiki wao na hasa waliopo humu JF hawapendi kulizungumzia hilo...kama kipimo chako cha USOMI ni JJ MNYIKA then you need to back to the drawing board...what did you seriously expect kwenye chama ambacho mwenyekiti wake anatuhumiwa kuwa amefukuzwa chuo kikuu baada ya kufeli masomo?

  kwa nini Freeman Mbowe hataki kuita press conference na kuaddress hizi issue yake ya shule once and for all?

  anaficha nini?  Halafu the so called WAPIGANAJI wanakuja humu kutaka ku-justify huu ujinga wa kutetea FREEMAN kufukuzwa/kutomaliza chuo kikuu

  Hiyo katiba yao uliyoizungumzia iko shallow sana especially kwa chama kinachojiita chama mbadala wa CCM au chama ambacho kitachukua nchi in 2010!

  lakini stay tuned kuona watakavyokuja humu kutetea visivyoteteeka

  counting...1
   
 6. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #6
  Nov 11, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  kwa hiyo unaona sawa kwa mwenyekiti wao kutokuwa open na maendeleo yake ya kimasomo?

  kama anaficha simple issues kama shule what makes you think atakuwa open akishakuwa rais wetu?

  its time CHADEMA face the fact kuwa haya mambo ya kufika ugonjwa yatakifanya hiki chama ki ji self destruct
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Nov 11, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Rostam Azizi alisoma shule gani vile? Mweka hazina wa CCM hapo nyuma give us his academic credentials GT!!!!!!!!!
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Nov 11, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  WE Masanilo punguza Hasira NA ROSTAM usije ukamla nyama
   
 9. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #9
  Nov 11, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  1..........
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Nov 11, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Rostam alisoma wapi na alisomea nini mazeee!???? Mwache chairman Mbowe
   
 11. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #11
  Nov 11, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nadhani uko nje ya mada! kwahiyo unataka chadema iwe kama CCM..we need a serious alternative party...sasa umeshaanza kulinganisha na wafu ambao sisi tulishawakataa tangu vyama vingi vilipoingia nchini..chadema wako na serious problem ya mwenyekiti..ngoja uone atakavyo watimua walio mpinga, upuuzi huo..siyo kudhibiti nidhamu wala nini bali uwoga wa mwenyekiti..lol anaogopa slogan ya chama chake demokrasia..lol
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Nov 11, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  I do not think so.....!
   
 13. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #13
  Nov 11, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  come on man...we are talking about Freeman Mbowe ambaye anaweza kuwa rais wa Tanzania, unless wewe kama mwana CHADEMA huamini mna nafasi ya kushinda uchaguzi

  Rostam anaingia vipi kwenye huu mjadala...if anything he's a non issue humu

  Mbowe aje clean address hizo allegations kuwa CHADEMA ni Chama cha familia na kama kweli kafukuzwa HULL UNIVERSITY
   
 14. m

  msasa Member

  #14
  Nov 11, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  nne - udini(ukatoliki)
  tano - ukabila (chagga)
   
 15. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #15
  Nov 11, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu mbona huwa hutaki kabisa aguswe Rostam ama Lowassa kwani wewe ni zao la ufisadi? give us some hints tuendelee na Mbowe!
   
 16. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #16
  Nov 11, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kigarama

  Inaelekea hujasoma katiba ya CHADEMA. Ipo hapa: http://www.chadema.or.tz/nyaraka/katiba_2006.pdf, wenyeviti wa mikoa hawajaondolewa kuwa wajumbe wa Baraza Kuu. Ni wajumbe. Makatibu wa Mikoa hawajaondolewa kuwa wajumbe wa Mkutano Mkuu, ni wajumbe.

  Mabadiliko ya Katiba yaliyofanyika chini ya Mbowe na Dr Slaa yalilenga kupeleka mamlaka ya kichama chini zaidi, ikaanziswa ngazi ya MSINGI. Pia mamlaka makubwa zaidi yameelekezwa kwenye ngazi za MAJIMBO, na sasa kila jimbo Tanzania linawakilishwa Mkutano mkuu na Wilaya zote zinawakilishwa kwenye Baraza Kuu la chama.

  Soma hapa: http://www.chadema.or.tz/chama/uzinduzi.php

  Asha
   
 17. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #17
  Nov 11, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama nyinyi mnataka kife basi haina maana kwa siasa za Tanzania lazima watu wenye malengo mazuri ya kweli na Tanzania kufanya yale Mababu zetu walifanya
   
 18. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #18
  Nov 11, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Any way, isiwe kwa sababu watu waliochukuliwa hatua ni wa kundi la mtu fulani ndo ina kuwa kelele..kama chama kimetumia taratibu kilizojiwekea za kumshughulikia mwanachama yeyote basi waachiwe Chadema na utaratibu huo...ila kama wanafanya kwa ajili ya kukomoana basi hayaishii hapo...yataendelea kama yalivyokuwa kwa Mrema na TLP yake...kabaki na Makao makuu na Bendera tu...hana chama.
  Ushauri wa bure kwa Chadema...wangejaribu kuziba hizi nyufa zinazoelekea kuleta hali isiyoeleweka ndani ya chama chao,hali hii ikiendelea itawavunja moyo wafuasi wao na maendeleo ya chama chenyewe na kudhoofisha nguvu ya upinzani nchini, tunahitaji kuwa na vyama madhubuti vya upinzani.
   
 19. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #19
  Nov 11, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  Nov 11, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  upele umepata mkunaji
   
Loading...