Haya ndiyo yanayowafanya wakumbatie muswada wa katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya ndiyo yanayowafanya wakumbatie muswada wa katiba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Escobar, Nov 19, 2011.

 1. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2011
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Ndugu wana jopo, binadam yeyote mwenye afya akili bila kujali ni timamu au la huwa anawaza. Nimekuwa nafuatilia kwa muda mwenendo wa namna ya kuwa na katiba mpya na nimegundua kuwa mambo kadhaa yafuatayo ndiyo yanayopelekea vile tunavyovutana leo na endapo vyama vya upinzani na wanaharakati wataahidi kuyaacha kama yalivyo ninauhakika kabisa jukumu la kuandika katiba anaweza kupatiwa hata Kibamba asimamie zoezi hilo.

  1. Nafasi ya mke wa rais
  2. Uteuzi unaofanywa na raisi ubaki kama ulivyo na asihojiwe juu ya vigezo na sifa za wanaoteuliwa
  3. Nafasi za wakuu wa mikoa na wilaya
  4. Tume ya uchaguzi isiguswe
  5. Maslahi ya rais
  6. Haja ya kuwa na Makamu wa rais na Waziri mkuu
  7. Nchi moja marais 5 na waziri mkuu 1 (Tanganyika marais 2 na waziri mkuu 1, Zanzibar marais 3)
  8. Kubwa kuliko yote ni Rais kushtakiwa akitoka madarakani endapo alifanya kosa enzi za utawala wake.

  Mambo haya yakiondolewa kwenye mjadala wa kuandika katiba mpya i mean yakiachwa kama yalivyo yaani yasiguswe basi hapo roho za watu zitatulia na kazi hiyo watampa yeyote mwenye ufahamu aandike katiba kwanza ni kazi ngumu sana inayofikirisha mno na wataalamu wetu huwa hawana kasumba ya kuumiza vichwa sana unless kuna faida flani anapata katika hicho kitu (rejea mikataba ya madini na ufuajui umeme, inatia shaka kama ilisainiwa na watz wenye nia njema na taifa hili)
   
Loading...