Haya ndiyo yaliyotumika kuvuruga uchaguzi leo; Jeshi, DCs, DEDs, Mameya, Wasimamizi

CHADEMA

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
490
2,471

Huko Tandahimba magari ya jeshi tangu jana yanazunguka mitaani. Kutokana na kumbukumbu za wananchi wakati wa sakata la gesi, wananchi wengi wametishika na wameshindwa kabisa kupiga kura.

Wakuu wa wilaya; mathalani Sikonge, Mkalama, Kaliua, Kilindi wamejitokeza hadharani kuingilia uchaguzi huu, kutangaza matokeo, kuengua watu, kutangaza washindi. Hakuna mahali popote wakuu wa wilaya wanatajwa kuwa na mamlaka kwenye uchaguzi huu.

Meya wa Ilala, yeye kwa kihoro cha CCM kushindwa kwenye kata na mtaa anayoishi, katangaza kuahirisha uchaguzi katika maeneo hayo. Hakuna mahali popote meya anahusika katika uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa.

Muda huu, Mbunge Idd Azzan amekwenda Kituo cha Polisi Oyster bay, kuwatoa polisi watu walioingia na mapanga Kituo cha Kinondoni Mjini, mapema asubuhi, wakiwa wametumwa kuvuruga uchaguzi kituoni hapo.

Kila mahali wakuu wa wilaya kwa kushirikiana na wakurugenzi wameingilia uchaguzi huu kwa kiwango ambacho kinadhihirisha CCM ilijua mapema kuwa inaanguka vibaya katika uchaguzi huu.

Moja ya mambo waliyofanya DCs na DEDs leo ni pamoja na kuengua wagombea wa CHADEMA leo asubuhi vituoni au kutangaza mapingamizi au kufuta uchaguzi.

Huko Simanjiro, kada mwandamizi wa CCM amekodisha gari zilizobeba morani ambao wamedaiwa kumvamia na kumkatakata kwa mapanga wakala wa CHADEMA kituoni kwenye Kijiji cha Korongo...polisi pamoja na kushuhudia hawajachukua hatua yoyote.
 
Tunasubiri kuona Ukawa watachukua hatua gani,tunachotaka ni ushindi kwa gharama yoyote ile
 
propaganda zishaaanza...eti ukimwona mwanajeshi unaogopa kupiga kura? kwani katka hao wananchi hawakuwemo wana ccm...au wenyew chuma...
tanzania nzima umeona hayo tu? tunataka mabadiliko ya ukweli...cyo kidogo tu eti mwaenda ktkt maridhiano...HUWA MNAKUBALIANA NN HUKO? mmeshindwa kumwajibisha pm bungeni...mnaleta uzushi hapa...wote wamoja tu!!
 
Hapa ndipo unapopatikana ushahidi tosha kwamba vyeo vya kishemejishemeji hivi kama vya wakuu wa Mikoa, wilaya, Makatibu Tarafa, kata havina hata chembe ya faida kwa watanzania! Ni jambo la kawaida kabisa kuwaona watu hawa wakiambatana na wana CCM katika kampeni, kuna moja juzi kule Kigoma aliyepanda jukwaa na kujinadi eti yeye ni mara wa CCM na kuwatisha wapinzani.
Ni vyeo vya rushwa ambavyo kamwe CCM haitavifuta labda wakija poteza mamlaka. Wakuu wa Mikoa, wilaya, makatibu tarafa na kata ndiyo haswa wahusika katika kuratibu wizi wa kura, kuwatisha watumishi kwamba 'watashughulikiwa" CCM isipopita mahali fulani. Ni mzigo kwa taifa na ni ajabu kwa wananchi kubebeshwa zigo la kuwatunza na kuwalipa wahaini wa demokrasia hawa.
 
Hili linchi halina demokrasia kabisa!

Kuna Nchi hata hili ulilopost lingeweza kukufanya uchukuliwe hatua za kutisha.
Huu ni mfano tu kuwa nchi hii ina Demokrasia, nadhani unaelewa kuwa uhuru wa kujieleza ni kati ya mihimili ya Demokrasia.
 
Back
Top Bottom