Haya ndiyo yaliyosemwa leo kupitia TBC1 na Mzee Shamte, aliyekuwa katibu mkuu wa kwanza wa Afro Shiraz Party

SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
4,040
8,895
1. Wazanzibari ndio wanaonufakika zaidi na muungano kuliko wabara.

2. Viongozi wengi wa sasa hivi hawana maadili wengi ni wezi na wamejaa tamaa za madaraka.

3. Yeye ni Mzanzibari ila ameoa bara/Pangani Tanga na ana watoto 3.

4. Rais Mwinyi haujui Muungano kwa kuwa alizaliwa baada ya muungano.

5. Wanawake wakae nyumbani walee familia, majukumu ya ofisini waachiwe wanaume.

6. Marehemu Seif Sharif Hamad ndio alimchoma Jumbe na kupitia yeye/Maalim Seif ndioJeshi na Polisi yakawa mambo ya muungano kwa usalama wa Zanzibar.

7. Viongozi wote wapitie vyuo vya uongozi kama Kivukoni na Ihemi.

8. Kabla Karume hajauawa yalifanyika majaribio 11 ya kumuua.

Ameongea mengi sana...

NB: Mzee Shamte ndio katibu mkuu wa kwanza wa Afro Shiraz Party. Mzanzibar mwenye asili ya Pemba.
 
Number 5 na number 1 ni kweli kabisa

Huu muungano unachekesha sana ukiwauliza wanzazibari wanakwambia "oooh nyinyi Watanganyika mmetumeza yani mmetufanya kama Koloni lenu"

Ukiwauliza Watanganyika wanasema "Oooh Zanzibar wanatunyonya gharama za muungano tunabeba sisi hatuoni faida yake"

Lakini ukiwauliza wanasiasa hasa wa CCM wanakwambia muungano utalindwa kwa Nguvu zote! Ukihoji sana wanakwambia wewe ni Adui wa muungano sasa unajiuliza kama muungano unafaida kwa wananchi wa kawaida kwa nini ulindwe kwa Nguvu? hv mtu unaweza kuchezea kile kinachokupa faida?
 
Namba 5 akaiongelee huko huko Zanzibar.

Sema wanaume huwa tunakuwa wabinafsi sana.

Hivi kama mama, au dada yako ndio mwenye nafasi kubwa ya kisiasa utakataa eti kwa kuwa ni mwanamke?
 
Vitu vingine vinachekesha kama wazanzibar ndio wanufaika wakubwa wa muungano, kwanini wanapotaka kuuvunja, wabara ndio ucharuka muungano usivunjwe?
CCM ndio wanaobembeleza muungano.

Ila watanganyika wa kawaida wapo wapotu, whether muungano uwepo au usiwepo hakuna manufaa yoyote kwao.
 
#5 ana mpango wa kujaribu kumzengua mama.

Mama atakuwa ana mcheki na kujisemea: Hiiiiii!
 
Vitu vingine vinachekesha kama wazanzibar ndio wanufaika wakubwa wa muungano, kwanini wanapotaka kuuvunja, wabara ndio ucharuka muungano usivunjwe?
Muungano huu TANGANYIKA ni kwa sababu za KIUSALAMA na sio VUNGINEVYO.
 
CCM ndio wanaobembeleza muungano.

Ila watanganyika wa kawaida wapo wapotu, whether muungano uwepo au usiwepo hakuna manufaa yoyote kwao.
Hao wa Tanganyika wa kawaida kitendo cha kukaa kimya maana yake wamekubaliana na hao viongozi wa CCM.
 
Hao wa Tanganyika wa kawaida kitendo cha kukaa kimya maana yake wamekubaliana na hao viongozi wa ccm
Hawaumii kwa vyovyote na muungano.

Zanzibar wanapata faida huku bara kama Ardhi, Vyeo, Ajira lakini hakuna mtanganyika atayepata chochote cha maana huko Zenji.

Na kwasababu pia ardhi huku ipo hakuna anayejali.
 
Kama wazanzibari ndiyo wanufaika na muungano masheikh wa uamsho wasingedai Zanzibar yenye mamlaka kamili na wasingefungwa bara, na kero za muungano zisingekuwepo wala wazanzibari wasingezileta kwenye majadiliano.
 
Hawaumii kwa vyovyote na muungano.

Zanzibar wanapata faida huku bara kama Ardhi, Vyeo, Ajira lakini hakuna mtanganyika atayepata chochote cha maana huko Zenji.

Na kwasababu pia ardhi huku ipo hakuna anayejali.
Hawaumii vipi wakati ndio kila siku wanalialia humu JF! ! Pesa za sherehe ya muungano kupelekwa Zanzibar kelele humu ndani mtindo mmoja halafu unasema Hawaumii! ! wanaumia sana sema hawana cha kufanya maana ni waoga kuliko ata Kunguru
 
Hoja ya raisi Mwinyi kutojua muungano kwa kuwa kazaliwa baada ya muungano haina mantiki, kwa kuwa muungano ni maridhiano na makubaliano haina ya pande zinazoungana, ni sawa na kusema ndoa ya wazazi wake haijui kwa kuwa wakati wanafunga ndoa yeye alikuwa hajazaliwa, haina mantiki.
 
Back
Top Bottom