Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,479
- 30,144
Tumefika siku ya kile kinachoitwa siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa, lakini mimi niiite siku ya UCHAFUZI.
Hivi katika mazingira ya kawaida unaposhindana na mshindani wako na akaamua kujitoa kutokana na dhuluma za waziwazi unazomfanyia, hivi wewe unayebaki kwenye ushindani huo, utawezaje kuwa na ari ya kushangilia ushindi huo, wakati ni ushindi wa AIBU?
Hivi inapotokea wagombea zaidi ya asilimia 95 ya washindani wako wa vyama vya upinzani, umewaengua kugombea, na nyinyi maccm mmewapitisha wagombea wenu asilimia 100, inapotokea wapinzani hao hao wametangaza kujitoa, hivi unaweza kweli kuwalazimisha kwenda kupiga kura katika huo UCHAFUZI wenu?
Wahenga wamenena kuwa huwezi kumlazimisha punda anywe maji kisimani
Haya ndiyo matokeo ya ubabe wenu wa kupitiliza, kwa hiyo mnavuna mlichokipanda!