Haya ndiyo matokeo ya watawala ya kuwapuuza wapinzani

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,331
2,000
Tumefika siku ya kile kinachoitwa siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa, lakini mimi niiite siku ya UCHAFUZI.

Hivi katika mazingira ya kawaida unaposhindana na mshindani wako na akaamua kujitoa kutokana na dhuluma za waziwazi unazomfanyia, hivi wewe unayebaki kwenye ushindani huo, utawezaje kuwa na ari ya kushangilia ushindi huo, wakati ni ushindi wa AIBU?

Hivi inapotokea wagombea zaidi ya asilimia 95 ya washindani wako wa vyama vya upinzani, umewaengua kugombea, na nyinyi maccm mmewapitisha wagombea wenu asilimia 100, inapotokea wapinzani hao hao wametangaza kujitoa, hivi unaweza kweli kuwalazimisha kwenda kupiga kura katika huo UCHAFUZI wenu?

Wahenga wamenena kuwa huwezi kumlazimisha punda anywe maji kisimani

Haya ndiyo matokeo ya ubabe wenu wa kupitiliza, kwa hiyo mnavuna mlichokipanda!
 
Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
7,745
2,000
Mbona hata kwenye soka haya yapo, mechi ikipangwa na timu zikakubaliana uwanja , timu moja ikitokea na nyingine isitokee, point 3 anapewa aliyetokea.

Muwaache wachukue point 3 za mezani, dunia haijasimama next time tutaangalia mchuano.
 
jabulani

JF-Expert Member
Aug 1, 2015
4,513
2,000
CCM mapinduzi yao yamehamia kwenye kutangaza matokeo ya uchaguzi. Sasa safari hii hawana wa kumpindua, hawatoweza kujidai wameshinda kwa kishindo. Aibu yao.
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,331
2,000
CCM mapinduzi yao yamehamia kwenye kutangaza matokeo ya uchaguzi. Sasa safari hii hawana wa kumpindua, hawatoweza kujidai wameshinda kwa kishindo. Aibu yao.
Wao CCM wametembeza ubabe ili washinde kwa asilimia 100 kwenye chaguzi hizi, wapinzani wenu wamejitoa mnawalazimisha kushiriki

Hivi hamjawahi kusikia msemo wa wahenga usemao, huwezi kumlazimisha punda anywe maji kisimani??
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,969
2,000
Politics is a game, kuna rules of the game, usipozifuata unakuwa disqualified, timu pinzani inakula point tatu.
Kwa vile this is a game, usipopeleka timu uwanjani, mwenzako akatoka na ushindi wa mezani.

Uchaguzi ni leo, tuliojiandikisha, kama hakuna poits za mazeni, tujitokeze kwa wingi, twendeni tukapige kura kuwachagua viongozi wetu.
P
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,331
2,000
Pascal Mayalla,
Mkuu Pascal, ngoja nikupe tafsiri sahihi ya uchaguzi, ni ile kupewa fursa ya wewe mchaguaji, kuchagua kile unachoona kinafaa kwa Uhuru, lakini inapotokea wewe mchaguaji, katika mazingira uliyopo "unalazimishwa" kuchagua kitu ambacho hujaridhia nacho, huo unaitwa UCHAFUZI na wala si uchaguzi!
 
ngusillo

JF-Expert Member
Nov 5, 2019
1,067
2,000
Tusubiri tuone hayo matokeo. Nitaenda kukaa karibu na kituo kilichopo karibu nikusanye takwimu za wapigakura. Naamini hayo matokeo nitayaona
 
Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
7,745
2,000
Sijawahi kuona uchaguzi ambao vyama vyote vyenye usajili vimeshiriki, sioni kwanini huu tusiuone kama chaguzi zingine zilizowahi kupita.
 
lukoma

JF-Expert Member
Jul 1, 2013
2,991
2,000
Mbona hata kwenye soka haya yapo, mechi ikipangwa na timu zikakubaliana uwanja , timu moja ikitokea na nyingine isitokee, point 3 anapewa aliyetokea.

Muwaache wachukue point 3 za mezani, dunia haijasimama next time tutaangalia mchuano.
Hoja yake ni ari ya kushangilia au kujisifi sio point 3/ ushindi. Hata kwenye soka ushindi wa mezani huwa haushangiliwi.
 
Brakelyn

JF-Expert Member
Oct 6, 2009
1,183
2,000
Pascal unaelewa kabisa wagombea wa upinzani Nchi nzima wamekuwa disqualified makusudi kabisa and yet you of all the people is blessing this kwa kusema usipopeleka timu uwanjani, mwezako anatoka na ushindi wa mezani. Sijui wamekufanya nini ccm hivi karibuni but if you stand for free and fair elections you should rethink your position. Umekuwa mtu wa ndiyo mzee kirahisi sana aise...
Politics is a game, kuna rules of the game, usipozifuata unakuwa disqualified, timu pinzani inakula point tatu.
Kwa vile this is a game, usipopeleka timu uwanjani, mwenzako akatoka na ushindi wa mezani.

Uchaguzi ni leo, tuliojiandikisha, kama hakuna poits za mazeni, tujitokeze kwa wingi, twendeni tukapige kura kuwachagua viongozi wetu.
P
 
King Kisali

JF-Expert Member
Nov 20, 2019
772
1,000

Hakuna wa kujitokeza mzee na leo ndio kipimo chenu kama ndege, stiegersgorge, standard gauge zinalipa, majibu mtayaona.
 
storyteller

JF-Expert Member
Nov 5, 2014
1,391
2,000
Umekoment km mlevi.
Politics is a game, kuna rules of the game, usipozifuata unakuwa disqualified, timu pinzani inakula point tatu.
Kwa vile this is a game, usipopeleka timu uwanjani, mwenzako akatoka na ushindi wa mezani.

Uchaguzi ni leo, tuliojiandikisha, kama hakuna poits za mazeni, tujitokeze kwa wingi, twendeni tukapige kura kuwachagua viongozi wetu.
P
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,969
2,000
Pasco Uneshindwa kusema chochote japo kumuunga Mkono Rais lkwa Ndege kukamatwa Hata pole jamani!
Pole kwa Rais wa JMT kwa ndege yake kukamatwa.
Pole kwa Waziri Kabudi kwa TZ kusalitowa.
Pole kwa Waziri Mahiga kwa mateso kutuma vijana Canada
Pole kwa serikali yetu yote kwasababu ndege ni ya serikali.
Pole kwa CCM, kwasababu serikali ni ya CCM.
Pole kwa wanasheria watakaoteseka.
Pole kwa ATC ndege yao kukamatwa hivyo kuchelewesha kupiga pesa.
Pole kwa sisi Watanzania wote kwa ndege yetu kukamatwa na kututia hasara ambayo ni sisi tutaifidia.
Ndege ni rais Magufuli kwasababu ndiye aliyeamua kuinunua kwa cash money.
Ndege ni ya serikali kwasababu inamilikiwa na serikali 100%.
Ndege ni ya ATCL kwasababu ATCL ndio wanaitumia.
Ndege ni ya Sisi Watanzania wote kwasababu fedha zilizonunulia ni fedha zetu, na sisi ndio tunaoipanda.

Pole wote
P
 
konyola

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
2,080
2,000
Politics is a game, kuna rules of the game, usipozifuata unakuwa disqualified, timu pinzani inakula point tatu.
Kwa vile this is a game, usipopeleka timu uwanjani, mwenzako akatoka na ushindi wa mezani.
Kweli Africa kuna laana yaani msomi kama huyu nae anatoa hoja yenye utopolo kama hii kisa mtu anatafuta TEUZI.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom