Haya ndiyo matokeo ya kukimbia shule, masikini CHADEMA...

Nimesoma kwa mshangao sana hoja ya John Mnyika juu ya uamuzi wa CCM kusimamia ilani yake ya uchaguzi ambayo licha ya kuchaguliwa kihalali na wananchi mwaka 2010, utekelezaji wake utaleta mabadiliko katika maisha ya kawaida ya wananchi.
Bila shaka ni katika mtikisiko wa kukata roho kwa Chama mufilisi cha Chadema ndo maana viongozi wake sasa wana kurupuka kutoa matamko yasiyo na kichwa wala miguu katika kuhangaika kukata roho kwa kujidanganya kijinga tu kwamba wanaweza kuzuia nguvu ya timu mpya ya CCM ambayo bilashaka imewatia homa sana watani. Juhudi hizi ni sawa na kuzuia mafuriko kwa vidole..(poor Chadema, R.I.P Chadema).


Pengine tujaribu kutafakari maswali yafuatayo;
1. Ilani ya uchaguzi (kama wanafahamu maana yake) inayotekelezwa ni ya nani?
2. Nani anasimamia na nani anatekeleza Ilani ya uchaguzi ya chama kilichopo madarakani?
3.Ni lini mwenye ilani ana kagua utekelezaji wa ilani yake?...anasubiri miaka mitano? Anamuuliza nani hatua mbalimbali za utekelezaji ukiachilia mbali kwenda na kujionea mwenyewe hatua hizo?
4.Mtiririko gani wa mawasiliano kati ya chama tawala na serikali yake ili kupata mrejesho kwa wananchi?

...

Nape nashukuru kwa majibu yako na majibu kama haya haya yaliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wenu Mwigulu Nchemba, naona ni vyema nijielekeze kwenye hoja zako na niachane na vioja vingine. Ikiwa majibu haya ni msimamo pia wa Mwenyekiti wenu Kikwete na Katibu Mkuu Kinana, hakika mnadhihirisha kauli niliyoa bungeni kwamba tumefika hapa tulipo kwa sababu ya "udhaifu wa Rais, uzembe wa Bunge na Wabunge na Upuuzi wa CCM". Kinachoendelea katika suala hili ni sehemu tu ya udhaifu, uzembe na upuuzi huo. Maandishi yako yote hayajajibu hoja, nashauri kwanza soma hapa: JOHN MNYIKA: Balozi Sefue na Yambesi watoe kauli iwapo Serikali imetoa waraka wa maagizo kwa watumishi wa umma kutoa taarifa katika mikutano ya CCM kinyume cha maadili Jibu kwanza hoja. Wakati nikisubiri majibu juu ya kauli yangu hiyo na ile ya awali. Nashauri pia ujijibu mwenyewe hayo maswali uliyoyauliza ili udhihirishe uwelewa wako tenge kuhusu masuala hayo uliyohitaji majibu halafu nitakuja kukupa majibu sahihi kwa kuzingatia katiba ya nchi, katiba za vyama vya siasa, sheria za nchi, kanuni za nchi, kanuni za vyama vya siasa, maadili ya nchi na maadili ya vyama vya siasa, waraka wa serikali na waraka wa vyama vya siasa. Kama huna majibu unaweza pia kusema, sasa hivi na nitajibu masuala yote kama ulivyohitaji.

Hata hivyo, katika hatua ya sasa ni vizuri nikaweka kwenye muktadha masuala yafuatayo: kuna tofauti kati ya viongozi na wateule wa kisiasa na watumishi wa umma (political appointees and public leaders Vs Civil Servants); kauli yangu imehusu watumishi wa umma (Civil Servants) kufuatia kauli yenu ya Mwanza ya kutaka watumishi wa umma wa TANROADS, TANESCO nk kuja kujieleza kwenye mikutano ya CCM. Nape na Nchemba mmejikita katika kujibu hoja juu ya wateule wa kisiasa kama Mawaziri, nayasema haya kwa kurejea maandiko yenu kwenye mitandao mingine ya kijamii kuhusu kauli yangu. Ni vizuri mkasoma kwanza kauli yangu na kuielewa kabla ya kuanza kujibu.

Ieleweke pia sipingi CCM kusimamia ilani yake pale ambapo ina mamlaka ya kufanya hivyo, na Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwamba 'chama legelege huzaa serikali legelege' hivyo ulegelege wa sasa wa Serikali ni matokeo ya ulegelege wa CCM. Tiba yake sio kuwaita watumishi wa umma kwenye vikao vya CCM, tiba yake ni kusimamia wateule wa wachaguliwa na wateule wa kisiasa waliotokana na chama chenu wenye wajibu wa kuwawakilisha na pia kusimamia utekelezaji kwenye Serikali. Rais Kikwete ni mjumbe wa Kamati kuu ya chama chenu na vikao vingine vyote, mmewahi kumwita kumhoji kuhusu utekelezaji wa ilani yenu kuhusu maisha bora kwa kila mtanzania wakati huu ambapo gharama za maisha zinapanda wa ari, nguvu na kasi zaidi? Waziri Mkuu ni mjumbe wa vikao vya chama chenu, Kinana anasema mawaziri watajieleza kwenye NEC, hivi kabla ya kuwaita mawaziri kujieleza; mmewahi kumwita Waziri Mkuu na kumwajibisha? Mnaweza kuwaita viongozi wa kisiasa watuele wenu kuwahoji kwenye vikao vyenu lakini si watumishi wa umma kama ambavyo nitaeleza kwa kirefu kwa mujibu wa katiba, sheria, kanuni na maadili baada ya majibu yako.

Kwa upande mwingine, kitendo cha mawaziri sasa kuitwa kuhojiwa kwenye NEC ni ishara ya udhaifu wa Rais kama mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri katika kuwasimamia mawaziri hao na uzembe wa wabunge wa CCM katika kuwasimamia mawaziri bungeni kwa kiwango ambacho sasa kazi hiyo inataka ifanywe na watu wengine. Katika mazingira hayo, watanzania ikiwemo wanachama wa CCM wanasababu ya kumlipa mshahara Rais na kuwalipa wabunge wenu huku kazi inaenda kufanywa na NEC? Je, mnataka kuwaambia watanzania kwamba vyombo vyenu hivyo vimeshindwa kufanya kazi zake ipasavyo za kuisimamia serikali kutekeleza ilani na chama kutoa sera na uongozi wa ujumla?

Hali hii unaweza kushuka ngazi ya chini kwenye Halmashauri na kwenye taaasisi na mashirika mengine kwenye ngazi mbalimbali. Hivi inamaana Mameya na madiwani wenu katika maeneo ambayo mnatawala wana udhaifu na uzembe kwa kiwango ambacho sasa mnataka wakurugenzi wa Halmashauri na maafisa wao (watumishi wa umma) wakajieleze kwenye vikao vya CCM vya wilaya kinyume cha katiba, sheria, kanuni na maadili? Kwa mfano wa Nyamagana kwa kutaka TANROADS na TANESCO wakajieleze vikao vya CCM vya mkoa na wilaya, hivi maana yake mna mkuu wa mkoa na kamati ya ushauri ya mkoa (RCC), Mkuu wa wilaya na kamati ya ushauri ya Wilaya (DCC) wenye udhaifu na uzembe kwa kiwango cha sasa watumishi wa umma wa mashirika (watumishi wa umma) hayo wakajieleze ndani ya vikao vya CCM. Katibu ya chama chenu tayari ilishaweka mfumo ambao kwa misingi ya utawala bora na demokrasia si sawa lakini ni mfumo uliovumilika kwa miaka mingi wa wakuu wa wilaya na mikoa kuwa sehemu ya kamati za CCM za mikoa husika, hawa wateule wa kisiasa ndio waliopaswa kwenda kwenye vikao vya chama chenu na kutoa hizo unazoziita taarifa za utekelezaji wa ilani na wanayo fursa ya kukutana na hao watumishi wa umma. Kwa hiyo, kama kweli mngekuwa na dhamira ya dhati ya kubadilika, sio kufanya 'danganya toto' mngeanza kwanza kuwawajibisha hao kwa kushindwa kutimiza wajibu wao!.

Mmejaribu kuigeuza nchi kuwa dola ya kipolisi ukirejea matukio kama ya Ulimboka, Mwangosi nk baada ya kuambiwa msikimbilie polisi, mnayo hamu ya kurejesha mfumo wa chama kushika hatamu katika ya mfumo wa vyama vingi. Afadhali wakati wa Nyerere chama kilishika hatamu kwenye mfumo wa chama kimoja na kutoa uongozi, sasa chama hakishiki tena hatamu, kinatafuta 'utamu', utamu wa kubaki madarakani baada ya kuzidiwa na M4C na utamu wa kufanya ufisadi kupitia ofisi za umma. Katika hili la kuwataka watumishi wa umma wahudhurie vikao vya CCM na kutoa taarifa kwa lazima (na wala sizungumzii mawaziri kuzungumza kwenye mikutano yenu ya hadhara kwa nafasi zao za kichama) hamko sahihi. Na iwapo ni mfumo mpya wa utawala na utamaduni mpya wa kisiasa mnataka kuuanzisha fanyeni hivyo, na sisi tutawaita waje kwenye mikutano yetu na mtaona matokeo yake. Nitaeleza zaidi ukijielekeza kwanza kujibu hoja kwa hoja kutokana na kauli yangu: JOHN MNYIKA: Balozi Sefue na Yambesi watoe kauli iwapo Serikali imetoa waraka wa maagizo kwa watumishi wa umma kutoa taarifa katika mikutano ya CCM kinyume cha maadili na pia ukajibu mwenyewe hayo maswali yako uliyouliza, iwapo huna majibu yake; nitakusaidia kujibu.

JJ
 
Matumaini yangu ni kwamba ulicoandika bwana nape ni mtizamo wako na wala sii maoni ya chama. Kama utakuwa umetumwa na chama,basi, sina jingine zaidi ya kufikiri kuwa Tz tunaongozwa na misukule.
 
Endelea kulopolopo huku kodi zetu mjineemeshe wenyewe! Hakiyanan mm nilikuwa shabiki wako hadi kukupa kura yangu ya maoni pale ubungo nikiwa UD, mimaneno yako na upuuzi wa ccm umenikimbiza, hiv ww utajifananisha na mnyika kwa lipi?
Endelea kuwatumikia hao merchants then time will tel!
 
Mkuu John Mnyika

Nikkushukuru kwa kuamua kumjibu, tena jibu lenye uzito wa juu unaotambuliwa na shirikishisho la Great Thinkers duniani


Lakini umemjibu majibu mazito sana tofauti na uwezo wake kifikra na kitungamo,

Yeye hoja nyepesi ndio huzipenda na huzishadadia kwelikweli!
 
Mnyika ali acha chuo? unataka kutu aminisha kuwa kuacha chuo ni ujanja?

You missed the point, Ukiacha shule sababu ya bangi na mengine yanayoendana na hayo upuuzi. Akina Bill Gates Mzee wa Facebook pale Havard Maprofesa walikuwa wanawachelewesha tu. Mfano Mark Co- founder wa Facebook alikuwa mbele ya maprof kwa kila kitu.

Sijui Kuhusu elimu ya Mnyika, its my hope Nape Anaijua vizuri sababu kasema alikimbia shule, ila ninachokijua ni kwamba JJ Mnyika is one of the talented politicians Tanzania, he is several mile ahead of wanasiasa uchwara kama Nape. Pia, imekuwa sasa ni kasumba kwa Tanzania to glorify certificates. Ujinga huu!!
 
Nnauye Jr Kwanini UNA MATUSI? HAUJUI ULIKOTOKA??? MZEE MUSSA MOSES NNAUYE pia ALIKIMBIA SHULE???

Lakini alimudu kazi alizopewa zaidi ya AMBAO HAWAKUKIMBIA SHULE???

ACHA KU-JUDGE HUMAN BEING's is a SIN... WEWE SHUKURU CCM ilikusomesha INDIA wengine hawana BAHATI HIYO

SHAME ON YOU - INA MAANA UNAMTUKANA MZEE MUSSA MOSES NNAUYE --- KULI!!!!

Kama CCM waliwekeza katika kumsomesha mtu kama NAPE inadhihirisha ni kwa jinsi gani chama hicho kisivyokuwa na uwezo wa kupambanua mambo na kufanya maamuzi yaliyo sahihi. Chama makini hakiwezi kupoteza rasilimali zake kwa kumsomesha mtu wa aina hiyo vinginevyo ilikuwa ni kwa ajili ya kutoa shukrani/kulipa fadhila kwa baba yake. Hivi huko India alikuwa anasoma kweli ama ndiyo kuzuga ili na yeye aonekane kwenye kundi.
 
John Mnyika umemaliza nadhani hatuhitaji ubishi hapa ni Nape kuja kujibu hoja ya Mnyika kwanza then Mnyika amalize kila kitu maana hadi sasa tumeona mtiririko wa msomi na Mtu wa kuunga unga
 
Last edited by a moderator:
Kama CCM waliwekeza katika kumsomesha mtu kama NAPE inadhihirisha ni kwa jinsi gani chama hicho kisivyokuwa na uwezo wa kupambanua mambo na kufanya maamuzi yaliyo sahihi. Chama makini hakiwezi kupoteza rasilimali zake kwa kumsomesha mtu wa aina hiyo vinginevyo ilikuwa ni kwa ajili ya kutoa shukrani/kulipa fadhila kwa baba yake. Hivi huko India alikuwa anasoma kweli ama ndiyo kuzuga ili na yeye aonekane kwenye kundi.

India - KILA MTU anapasi... ALIFELI NSUMBA HIGH SCHOOL... MNYIKA alipata DIV 1 Point 7 O' LEVEL

Ni sawasawa na WILLIAM MALECELA... CCM inabeba WANAO left and right... ndio UZURI wa CULT...

Sasa PRINCE alibebwa akaenda kusoma LLM UK akafeli VIBAYA... na CCM na KIKWETE ndio ILIYOMPELEKA
 
Nnauye Jr mbona siku hizi hujadili tena hoja za ufisadi na kujivua gamba, badala yake unawekeza nguvu nyingi kuijadili na kuikosoa CHADEMA? Adui wa CCM ni CHADEMA au UFISADI?

Hivi kwa kutumia akili ya kawaida hata ya mtu ambaye hajaenda shule (ordinary person) unaona ni sawa watumishi wa umma, kama vile walimu wakuu wa shule nk, kusimama kwenye mikutano ya CCM kutolea ufafanuzi juu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa CCM? Kama ndivyo basi mna sababu gani ya kuwa na wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na mawaziri? Kwani hawa si mlisema kwa midomo yenu kwamba ni makada wenu? sasa yanini kuwasumbua watumishi wa umma ambao wana uhuru wao wa kuwa wanachama wa chama chochote?

Hii ni mara ya kwanza tangu mfumo wa vyama vingi uanze, tunasikia kiongozi wa chama anatoa amri kwa watumishi wa umma kama kwamba yeye ndiye mwajiri. Na hizi ni dalili za wazi kabisa kwamba CCM inaelekea kufa na ndiyo inatapatapa kushika hata nyasi japo kujizuia isiende na maji. Ni aibu kwa mtu kama wewe kuja mbele za watu na kusema CHADEMA inakufa.

Nakushangaa sana unavyoisifia safu mpya ya CCM iliyosheheni mafisadi. Kwani hao akina Mangula, Meghji na Kinana si ndiyo waliratibu wizi wa fedha za EPA? Na wewe si ulitangaza vita na mafisadi wa nchi hii? Kulikoni leo unashikana mkono na mafisadi na kujinasibu kwamba ni safu ya kutisha? CCM imepoteza mwelekeo na inakoelekea na kufutika kabisa katika historia ya Tanzania.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom