Haya ndiyo matokeo ya kukimbia shule, masikini CHADEMA...

Honey K

JF-Expert Member
Sep 14, 2008
629
72
HAYA NDIO MATEKEO YA KUKIMBIA SHULE.
* * * ***masikini CHADEMA**

Nimesoma kwa mshangao sana hoja ya John Mnyika juu ya uamuzi wa CCM kusimamia ilani yake ya uchaguzi ambayo licha ya kuchaguliwa kihalali na wananchi mwaka 2010, utekelezaji wake utaleta mabadiliko katika maisha ya kawaida ya wananchi.

Bila shaka ni katika mtikisiko wa kukata roho kwa Chama mufilisi cha Chadema ndo maana viongozi wake sasa wana kurupuka kutoa matamko yasiyo na kichwa wala miguu katika kuhangaika kukata roho kwa kujidanganya kijinga tu kwamba wanaweza kuzuia nguvu ya timu mpya ya CCM ambayo bilashaka imewatia homa sana watani. Juhudi hizi ni sawa na kuzuia mafuriko kwa vidole..(poor Chadema, R.I.P Chadema).

Kama hata kuzisoma na kuzitafisiri sheria na kanuni za utumishi zimewashinda watani wangu hawa, mnawezaje kuongoza nchi? Katika mazingira haya ni bora kukaa kimya badala ya kufumbua kinywa na kuonyesha jinsi usivyoelewa nchi inaongozwaje. Sasa sina hakika kama hii tafisiri anayojaribu kuijenga Mnyika hapa ni msimamo wa chama kizima au ni matokeo ya kukimbia shule.

Kama ni msimamo wa chama kizima, basi ni aibu kwa chama ambacho kimeendesha siasa kwa miaka 20 sasa kuwa na mtazamo wa hovyo na wa ajabu kama huu. Kama ni msimamo wa mbunge wangu John, basi si vibaya umri bado unaruhusu kurudi darasani kujaribu kumalizia alichokikimbia shuleni.

Pengine tujaribu kutafakari maswali yafuatayo;
1. Ilani ya uchaguzi (kama wanafahamu maana yake) inayotekelezwa ni ya nani?
2. Nani anasimamia na nani anatekeleza Ilani ya uchaguzi ya chama kilichopo madarakani?
3.Ni lini mwenye ilani ana kagua utekelezaji wa ilani yake?...anasubiri miaka mitano? Anamuuliza nani hatua mbalimbali za utekelezaji ukiachilia mbali kwenda na kujionea mwenyewe hatua hizo?
4.Mtiririko gani wa mawasiliano kati ya chama tawala na serikali yake ili kupata mrejesho kwa wananchi?

SOMA KISA HIKI.
Mtoto wa miaka mitatu anamzuia babaake kuingia chumbani baada ya kufika kutoka kazini akamkuta mamaake anavaa hivyo mtoto anamwambia baba usiingie chumbani kwani mama anavaa nguo katoka bafuni.... TATIZO HAPA NI MTOTO KUTOELEWA MAHUSIANO YALIYOPO KATI YA BABA NA MAMA...

MAJIBU YA JOHN MNYIKA:
Nape nashukuru kwa majibu yako na majibu kama haya haya yaliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wenu Mwigulu Nchemba, naona ni vyema nijielekeze kwenye hoja zako na niachane na vioja vingine. Ikiwa majibu haya ni msimamo pia wa Mwenyekiti wenu Kikwete na Katibu Mkuu Kinana, hakika mnadhihirisha kauli niliyoa bungeni kwamba tumefika hapa tulipo kwa sababu ya "udhaifu wa Rais, uzembe wa Bunge na Wabunge na Upuuzi wa CCM". Kinachoendelea katika suala hili ni sehemu tu ya udhaifu, uzembe na upuuzi huo. Maandishi yako yote hayajajibu hoja, nashauri kwanza soma hapa: JOHN MNYIKA: Balozi Sefue na Yambesi watoe kauli iwapo Serikali imetoa waraka wa maagizo kwa watumishi wa umma kutoa taarifa katika mikutano ya CCM kinyume cha maadili Jibu kwanza hoja. Wakati nikisubiri majibu juu ya kauli yangu hiyo na ile ya awali. Nashauri pia ujijibu mwenyewe hayo maswali uliyoyauliza ili udhihirishe uwelewa wako tenge kuhusu masuala hayo uliyohitaji majibu halafu nitakuja kukupa majibu sahihi kwa kuzingatia katiba ya nchi, katiba za vyama vya siasa, sheria za nchi, kanuni za nchi, kanuni za vyama vya siasa, maadili ya nchi na maadili ya vyama vya siasa, waraka wa serikali na waraka wa vyama vya siasa. Kama huna majibu unaweza pia kusema, sasa hivi na nitajibu masuala yote kama ulivyohitaji.

Hata hivyo, katika hatua ya sasa ni vizuri nikaweka kwenye muktadha masuala yafuatayo: kuna tofauti kati ya viongozi na wateule wa kisiasa na watumishi wa umma (political appointees and public leaders Vs Civil Servants); kauli yangu imehusu watumishi wa umma (Civil Servants) kufuatia kauli yenu ya Mwanza ya kutaka watumishi wa umma wa TANROADS, TANESCO nk kuja kujieleza kwenye mikutano ya CCM. Nape na Nchemba mmejikita katika kujibu hoja juu ya wateule wa kisiasa kama Mawaziri, nayasema haya kwa kurejea maandiko yenu kwenye mitandao mingine ya kijamii kuhusu kauli yangu. Ni vizuri mkasoma kwanza kauli yangu na kuielewa kabla ya kuanza kujibu.

Ieleweke pia sipingi CCM kusimamia ilani yake pale ambapo ina mamlaka ya kufanya hivyo, na Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwamba 'chama legelege huzaa serikali legelege' hivyo ulegelege wa sasa wa Serikali ni matokeo ya ulegelege wa CCM. Tiba yake sio kuwaita watumishi wa umma kwenye vikao vya CCM, tiba yake ni kusimamia wateule wa wachaguliwa na wateule wa kisiasa waliotokana na chama chenu wenye wajibu wa kuwawakilisha na pia kusimamia utekelezaji kwenye Serikali. Rais Kikwete ni mjumbe wa Kamati kuu ya chama chenu na vikao vingine vyote, mmewahi kumwita kumhoji kuhusu utekelezaji wa ilani yenu kuhusu maisha bora kwa kila mtanzania wakati huu ambapo gharama za maisha zinapanda wa ari, nguvu na kasi zaidi? Waziri Mkuu ni mjumbe wa vikao vya chama chenu, Kinana anasema mawaziri watajieleza kwenye NEC, hivi kabla ya kuwaita mawaziri kujieleza; mmewahi kumwita Waziri Mkuu na kumwajibisha? Mnaweza kuwaita viongozi wa kisiasa watuele wenu kuwahoji kwenye vikao vyenu lakini si watumishi wa umma kama ambavyo nitaeleza kwa kirefu kwa mujibu wa katiba, sheria, kanuni na maadili baada ya majibu yako.

Kwa upande mwingine, kitendo cha mawaziri sasa kuitwa kuhojiwa kwenye NEC ni ishara ya udhaifu wa Rais kama mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri katika kuwasimamia mawaziri hao na uzembe wa wabunge wa CCM katika kuwasimamia mawaziri bungeni kwa kiwango ambacho sasa kazi hiyo inataka ifanywe na watu wengine. Katika mazingira hayo, watanzania ikiwemo wanachama wa CCM wanasababu ya kumlipa mshahara Rais na kuwalipa wabunge wenu huku kazi inaenda kufanywa na NEC? Je, mnataka kuwaambia watanzania kwamba vyombo vyenu hivyo vimeshindwa kufanya kazi zake ipasavyo za kuisimamia serikali kutekeleza ilani na chama kutoa sera na uongozi wa ujumla?

Hali hii unaweza kushuka ngazi ya chini kwenye Halmashauri na kwenye taaasisi na mashirika mengine kwenye ngazi mbalimbali. Hivi inamaana Mameya na madiwani wenu katika maeneo ambayo mnatawala wana udhaifu na uzembe kwa kiwango ambacho sasa mnataka wakurugenzi wa Halmashauri na maafisa wao (watumishi wa umma) wakajieleze kwenye vikao vya CCM vya wilaya kinyume cha katiba, sheria, kanuni na maadili? Kwa mfano wa Nyamagana kwa kutaka TANROADS na TANESCO wakajieleze vikao vya CCM vya mkoa na wilaya, hivi maana yake mna mkuu wa mkoa na kamati ya ushauri ya mkoa (RCC), Mkuu wa wilaya na kamati ya ushauri ya Wilaya (DCC) wenye udhaifu na uzembe kwa kiwango cha sasa watumishi wa umma wa mashirika (watumishi wa umma) hayo wakajieleze ndani ya vikao vya CCM. Katibu ya chama chenu tayari ilishaweka mfumo ambao kwa misingi ya utawala bora na demokrasia si sawa lakini ni mfumo uliovumilika kwa miaka mingi wa wakuu wa wilaya na mikoa kuwa sehemu ya kamati za CCM za mikoa husika, hawa wateule wa kisiasa ndio waliopaswa kwenda kwenye vikao vya chama chenu na kutoa hizo unazoziita taarifa za utekelezaji wa ilani na wanayo fursa ya kukutana na hao watumishi wa umma. Kwa hiyo, kama kweli mngekuwa na dhamira ya dhati ya kubadilika, sio kufanya 'danganya toto' mngeanza kwanza kuwawajibisha hao kwa kushindwa kutimiza wajibu wao!.

Mmejaribu kuigeuza nchi kuwa dola ya kipolisi ukirejea matukio kama ya Ulimboka, Mwangosi nk baada ya kuambiwa msikimbilie polisi, mnayo hamu ya kurejesha mfumo wa chama kushika hatamu katika ya mfumo wa vyama vingi. Afadhali wakati wa Nyerere chama kilishika hatamu kwenye mfumo wa chama kimoja na kutoa uongozi, sasa chama hakishiki tena hatamu, kinatafuta 'utamu', utamu wa kubaki madarakani baada ya kuzidiwa na M4C na utamu wa kufanya ufisadi kupitia ofisi za umma. Katika hili la kuwataka watumishi wa umma wahudhurie vikao vya CCM na kutoa taarifa kwa lazima (na wala sizungumzii mawaziri kuzungumza kwenye mikutano yenu ya hadhara kwa nafasi zao za kichama) hamko sahihi. Na iwapo ni mfumo mpya wa utawala na utamaduni mpya wa kisiasa mnataka kuuanzisha fanyeni hivyo, na sisi tutawaita waje kwenye mikutano yetu na mtaona matokeo yake. Nitaeleza zaidi ukijielekeza kwanza kujibu hoja kwa hoja kutokana na kauli yangu: JOHN MNYIKA: Balozi Sefue na Yambesi watoe kauli iwapo Serikali imetoa waraka wa maagizo kwa watumishi wa umma kutoa taarifa katika mikutano ya CCM kinyume cha maadili na pia ukajibu mwenyewe hayo maswali yako uliyouliza, iwapo huna majibu yake; nitakusaidia kujibu.

JJ
 

C.T.U

JF-Expert Member
Jun 1, 2011
5,041
3,593
Kwa hiyo mnyika kakimbia shule ? Si nilisikiankuwa ni graduate?
 

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,780
Nnauye Jr Kwanini UNA MATUSI? HAUJUI ULIKOTOKA??? MZEE MUSSA MOSES NNAUYE pia ALIKIMBIA SHULE???

Lakini alimudu kazi alizopewa zaidi ya AMBAO HAWAKUKIMBIA SHULE???

ACHA KU-JUDGE HUMAN BEING's is a SIN... WEWE SHUKURU CCM ilikusomesha INDIA wengine hawana BAHATI HIYO

SHAME ON YOU - INA MAANA UNAMTUKANA MZEE MUSSA MOSES NNAUYE --- KULI!!!!
 

FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,081
6,189
Naona bado kuna dhamira ya ku-politicise civil service chini ya mwavuli wa 'chama kushika dola'. Sina hakika kama CCM wanaelewa madhara yake! Itakuwa vibaya kwaO (CCM). Serikali ya CCM haina mahusiano mazuri na walimu, madaktari na sasa chama kinata ku-drag the entire civil service! CCM itaangukia wapi?

NB: Nape ajitahidi kujifunza kuandika statement zenye hadhi ya nafasi anayotumikia. Very unprofessional statements za huyu kijana. Kuna tatizo gani? Katibu mwenezi kapata cheo bila hata kujua namna ya kuandaa statement?
 

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,348
3,080
Nape nnauye uelewa wako ni mdogo sana ndugu yangu, sifa kubwa ya mtumishi wa Umma duniani kote ni kutekeleza majukumu yake bila kuegemea upande wowote wa siasa( NONE PARTISAN) na hata kanuni zetu za utumishi ndivyo zinavyoelekeza, ilani ya uchaguzi ya CCM inatoa mwelekeo wa kisera wa utekelezaji wa majukumu ya serikali kwa kuzingatia masuala kama katiba na vipaumbele vya Taifa ambavyo hata ikiingia CHADEMA leo ni lazima vipaumbele vya Taifa vitaendelea kusimamiwa hata kwa sera tofauti.

Hakuna mtumishi yeyote wa Umma hapa Tanzania anayewajibika kwako wewe au kwa kiongozi wa CCM , ukiondoa Rais ambaye ndio mkuu wa utumishi wa Umma ( na ndiyo sababu kuna hoja hapa ya kutenganisha urais na uenyekiti wa chama cha siasa).

Nape naomba kufahamu elimu yako pia ni ya kiwango gani. Kwa sasa nakubaliana na wote wanokuona wewe kama muongeaji asiyezingatia ukweli, umeacha kujibu hoja ya kisheria na kikanuni inayomtaka mtumishi wa umma kusimama kwenye majukwaa ya kisiasa ya CCM , umekuja kumshabulia mnyika, Usemi huu unarefelect maisha yako, UKITAKA KUMFAHAMU MTU TABIA YAKE YA NDANI NA YA KWELI, MPE MADARAKA AU PESA, sasa nape tunakufahamu wewe ni mtu wa namna gani, na pengine huijui CCM vilivyo, muda utakwambia.Nape umelewa madaraka na ndio sababu wakubwa zako ndani ya chama hawaropoki unayoropoka wewe hadharani, sio kweli kwamba ni wajinga ila wanakuenjoy na unayofanya, watumishi wa Umma wanakudharau sana kwa taarifa yako tu.
 

HIMARS

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
46,016
46,989
Najua huu ni uchokozi unaofanyika hapa na lengo kuu ni kuondoa watu kwenye hoja za muhimu.
Sizani kama interms of class Nape unamfikia Mnyika ila sababu ni maoni yako na kuvuta watu kutoka kwenye mambo ya muhimu haina tabu

Pili hebu mpe John Myika hata muda katoka leo kweye kesi yenu ya uongo
 

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,437
Last edited by a moderator:

Froida

JF-Expert Member
May 25, 2009
8,774
3,226
Mahala popote duniani Civil Servants ni workforce ambayo inakuwa non- partisan,Nape wewe kama katibu mwenezi huwezi kumuita kiongozi wa Tanroads simply haiwezekani lakini kwa umbumbu wako unachanganya facts na interest, Interest ya CCM kwa sasa ni kujifufua toka kwenye kifo munajaribu kuimba wimbo ambao mumeushindwa kabla.

Nape huwezi kwenda hospitali ukamwita mkurugenzi wa muhimbili aje kujibu hadharani ,yaani huko CCM neno Ethics na etiqquates lilishachuja Mumekosea.

Tatizo lenu Secretariati ya CCM tangu ya Gama zote zilizofuata zinatumia nguvu na maamuzi ya kukurupuka hakuna mtiririko wa utendaji.

Wanaopaswa kutekeleza ilani ya CCM ni mawaziri kwa kuwasimamia watendaji chini ya wizara zao ,lakini wewe Nape kamwe huwezi ukamwita katibu mkuu na yeye akaja kwa sababu si mwana siasa ni mtumishi wa serikali,huyu na watendaji wengine wote waliochini yake hawawajibiki kwa chama hivi nyie CCM ni vipofu kiasi cha kwamba hamna chain of communication command duh. Nape umeenda kusoma usiku kuja kutafuta njia ya kujibu hoja ya Mnyika.

haya ngoja aje aliyekimbia shule ambaye huwezi kumfika hata chembe ya ufahamu wake shukuru sana Malecela na Msekwa India ungeisikia tuuh
 

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,872
4,530
Hoja za huyu Nape huwa sizielewi. Kwani yeye na Mnyika nani anaonyesha cheche za elimu?

Nnauye Jr mwanangu achana na ujinga wa kichama. Soma alama za nyakati. Huo mkangafu wako ukipigwa chini unaweza kukimbia nchi. Usikubali kutumikia tumbo lako kiasi cha kulitumia kufikiri badala ya kichwa.

Nisingependa kusema kuwa unafikiri kwa kutumia masaburi ingawa ni hiyo. Unashangaa wenzako wanaweza kuongoza nchi vipi wakati nyinyi mnaoifuja hamjionei hata kinyaa achia mbali shaka? Unasema RIP Chadema bila aibu wakati ukijua kuwa CCM iko ICU ikingoja kutupwa jenezani na kupigiliwa msumali wa mwisho!

Vipi hoja yako ya kujivua gamba ulipowalenga Chenge na Lowassa imeishia wapi zaidi ya wewe kuvishwa gamba tena zito? Maskini kijana unayejiona msomi unatumiwa kama nepi na bado unajionea fahari. Umejirahisi kiasi cha kutumiwa kama kiatu kukanyaga kila mahali.
 

MpigaFilimbi

JF-Expert Member
Apr 30, 2008
1,169
180
Nchi yetu ishakuwa ya ajabu sana!

Hivi tunaweza hata kulinganisha IQ yako na ya Mnyika? Mdomo wako wa uongo ndio mtaji wako, bahati mbaya ndio kazi ya CCM iliyobaki, kwa kuwa kazi ya msingi imewashinda, imebaki tu Dr.Slaa, Mnyika etc. watu wanataka maendeleo, sio hizi blah blah!! Badala ya kuweka mipango ya kuendeleza nchi kila mara mko kwenye mikakati ya kuangamiza wanaoitakia mema nchi hii!

Mungu si athumani bwana, hii nchi itakuja kupata viongozi wenye kuwajali watu wao.
 

Papa D

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
753
182
Nnauye!!
Probably you are right!!
Lakini nifafanulie hapa kabla sijachangia hoja zako:-

Suala la kuandika katiba mpya lipo kwenye ukurasa upi ndani ya Kitabu cha sera mlichonadi kwa wananchi hadi mkapewa nchi? Huoni mnayofanya yanahalalisha ile nadhalia kwamba hamkushinda uchaguzi?

If you insist on winning the election then, don't you see ccm is committing a criminal offence by doing what was not agreed between them and the citizen?
 

Head teacher

JF-Expert Member
Mar 10, 2012
1,796
405
Pengine tujaribu kutafakari maswali yafuatayo;
1. Ilani ya uchaguzi (kama wanafahamu maana yake) inayotekelezwa ni ya nani?
2. Nani anasimamia na nani anatekeleza Ilani ya uchaguzi ya chama kilichopo madarakani?
3.Ni lini mwenye ilani ana kagua utekelezaji wa ilani yake?...anasubiri miaka mitano? Anamuuliza nani hatua mbalimbali za utekelezaji ukiachilia mbali kwenda na kujionea mwenyewe hatua hizo?
4.Mtiririko gani wa mawasiliano kati ya chama tawala na serikali yake ili kupata mrejesho kwa wananchi?

Majibu:
1.Ilani asilimia 80 zinazotekelezwa ni za Chadema, mf. Katiba mpya, kupunguza bei vifaa vya ujenzi. n.k
2.Anayesimamia utekelezaji wa ilani ni Serikali, anayetekeleza ni watumishi wa umma na sekta binafsi
3.Kila baada ya uchaguzi aliyetoa ilani anakagua ilani yake, anawauliza wananchi na si kuzionyesha kwa wananchi
4. Aliyetoa ilani na Msimamizi wa ilani watafanya tathmini kwa kuzingatia maoni ya wananchi
 

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,437
Ngoja tukupe Darasa wewe Kibwengo Iko Hivi

1. Kwanza naona unashindwa Kutofautisha Sera za Chama au Ilani kwa Kiingereza inaitwa Party Manifesto ( Hiyo Inayoongoza Bila shaka ni ya CCM) na Sera za Serikali (Policy).

2. Chama Kinaposhinda Uchaguzi huwa Kinaunda Serikali ambayo inakuwa na Wanasiasa (Mawaziri) na Watumishi wengine

3. Wizara Inajukumu la Kutengeneza Sera (Policy) ambazo hutumiwa kama Dira and From Policy Bunge Hutunga Sheria

4. Baada ya Sheria Wizara Hutunga Kanuni za Utekeleza wa Hizo Sera na Huzikabidhi kwa Watumsihi wa Uma kwa Utekelezaji

5. Anayewajibika Kwa Chama si Mtumishi wa Uma bai ni Waziri

6. CCM ikimwita Waziri wa Nishati na Kumbana na Kumtaka atoe Maelezo juu ya Utekelezaji wa Ilani ni Sahihi kabisa Ila CCM inapotaka Kumwita Haruna Masebo kujibu wananchi juu utekelezaji wa Ilani ya CCM huo ni Ukengeufu na Ulevi wa Madaraka kwa sababu hakuna Mahala Masebu amepanda Jukwaani kuwaomba Waananchi Kura

Kwa Hili Katibu Mwenezi Umekurupuka Kweupeee na Tena sasa unatafuta Vita na TUKTA maana hutaiweza
 

Chief Isike

JF-Expert Member
Jan 17, 2010
445
462
Very poor guy.

Nakuomba ukimaliza kusoma comments za watu na kabla hujasaini posho yako kwa kazi yako ya leo, ikiwemo kumkodi kijana aitwaye Eddo Makata ukampachika ujumbe wa mkutano mkuu wa CHADEMA na hii ya sasa ulichoandika hapa JF, nakuomba sana tafuta na usome signature ya Invisible.

Ure toooooo low to Mnyika. Yaani leo umejiingiza kwenye 18, yaani umejidhalilisha. Kwa nafasi yako ulitegemewa uje uchambue tamko la Mnyika hapa useme vifungu vipi vya kanuni, sheria na katiba havijatafsiriwa ipasavyo, kisha wewe sasa nawe uoneshe uwezo wako, badala yake umepuyanga vichakani kutafuta fallacies, tena za kuokoteza.

Naona hamchoki kuiga. Umechukua msemo wa mwanaCHADEMA mmoja ambaye yeye huoenda kuita CCM R.I.P in advance. Kwa post hii mtu mzima umeuvaa mkenge. Huwezi kuchambua mambo, unaweza kutukana na kuropoka, si kujenga hoja na vijana wa CHADEMA. Unajaribu kuonja pepo, huwezi kabla hujafa.
 

sosoliso

JF-Expert Member
May 6, 2009
8,538
9,433
Mtoto wa miaka mitatu anamzuia babaake kuingia chumbani baada ya kufika kutoka kazini akamkuta mamaake anavaa hivyo mtoto anamwambia baba usiingie chumbani kwani mama anavaa nguo katoka bafuni.... TATIZO HAPA NI MTOTO KUTOELEWA MAHUSIANO YALIYOPO KATI YA BABA NA MAMA...

Kwa matuci hakuna anaewafikia ila Kama mna ubavu jaribu kuwafukuza wale watendaji waliogoma kuja kwenye ile meetin yenu muone kasheshe.. Ati waje kuelezea ilani ya ccm.. My foot..
 

Jakubumba

JF-Expert Member
Mar 5, 2011
1,624
495
Eti na huyu nae anajiita msomi, kwa akili ya kawaida mtu aliesoma huwa hadhalau wasiokwenda shule. Kukosa elimu kwa mtu kunachangiwa na mambo mengi sana sio kwamba hana akili.

Lakini mtu kama wewe ambae ni kiongozi wa juu wa chama tawala unaandika upuuzi KAMA huu, unatudhihilishia ni kwa namna gani chama chako hakikomakini na viongozi wabovu kama wewe.

Na pia tambua kuwa elimu pekee haiwezi kukufanya kuwa kiongozi makini.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

27 Reactions
Reply
Top Bottom