Elections 2010 Haya ndiyo matokeo Halisi?: Kikwete: 44.56% Na Dr. Slaa 44.45%

Hii attachment ya Kura Halisi nayo inaonekana imechakachuliwa. mbona idadi ya kura ina points e.g Mwanza - Lipumba (Votes: 21,575.333) hizi 0.333 ni nini????? Sina imani na report yote. Labda iletwe nyingine!!
 


Habari nilizozipata ni kwamba DR SILAA alishinda kwa 58% kabla zoezi la kuchakachua halijaanza
.
 
Superman asante info ni nzuri ni brain storming. Ukitazama kwa haraka unaweza kuamini likini inakosa uhalisia pia. Nilimuliza wakala mmoja kuhusu matokeo ya jimbo mmoja la Manyara alionyesha tofauti japo inakaribiana na ukweli. Mimi nadhani aliyetengeneza takwimu hizi anazo zile za ukweli na ametengeneza hii with a very clear objective. Ninaamini lengo lake nikuonyesha bado ushindi ni wa JK na kupooza hasira za watu.
Je tutapataje ya kweli?
 
Mimi ninavyoona hii tathmini ilifanyika kabla ya zoezi la uchaguzi na hii ndiyo sababu mwandaaji amekisia kuwa asilimia 65 (column C) ya wapiga kura walioandikishwa wangepiga kura. Kwa mujibu wa NEC ni asilimia 42 pekee waliopiga kura. Hata kichwa cha habari cha "column C" kinasomeka (VOTERS TO VOTE) ikimaanisha kuwa hawa ndiyo waliotarajiwa kupiga kura.

Hivyo huu ushahidi hausaidii kuhitimisha kuwa kura ziliibwa.
 


Habari nilizozipata ni kwamba DR SILAA alishinda kwa 58% kabla zoezi la kuchakachua halijaanza
.

Hii nina maana kuwa hakuna mtu anayejua hasa nini kilitokea kwenye zoezi zima la kupiga, kuhesabu na kuchakachua matokeo ya kura. Mimi nashauri wataalam wa CHADEMA wafanye upembuzi yakinifu wakitumia karatasi za matokeo zilizosainiwa na mawakala wao katika vituo vya kupigia kura walau kwa mkoa mmoja ili tujue pumba na mchele.
 
Duh....tunaishi kwenye jumuiya ya ajabu...tunadanganywa macho wazi hvi hvi...ngoja nikamwambie bibi yangu apigie deki tu ile kanga waliompa coz hawafai hawa watu.....
 
Nchi yetu bwana... Haiishi kuwa na mambo ya Kipuuzi sasa hizi excel document nani asiweza kutengeneza?
 
Naona kama ziko kinyume na za mleta hoja na hakuna kura za Zanzibar....Yote yote ni kwamba jamaa wametuchakachua sana tu.....


ni kweli iliyo wazi kama hakina za Zanzibar hata na sisi mmet\uchakachua
 

UPDATE 2:

Waungwana, nimeongea tena na chanzo changu ambacho ndicho kilichonipatia taarifa hii. Matokeo yaliyoambatanishwa nimejulishwa ni yale ya utafiti wa ndani ambao ulifanywa kabla ya uchaguzi. Actual results nimeambiwa zikitolewa sasa hivi inaweza kusababisha kutoelewana.

Tuvute subira mpaka hapo taarifa ya uhakika itakapotolewa.

SM
 
Wana JF;

Nimepata taarifa kutoka chanzo cha kuaminika kuwa original results kutoka katika vituo vya kupiga kura ambazo Mgombe wa CHADEMA Dr. Slaa na vijana wake walikuwa wanahakiki zinaonyesha kuwa Mgombea wa CCM Kikwete alipata 44.56% wakati Mgombea wa CHADEMA alipata 44.45%.

Matokeo haya ni pamoja na mchakachuo uliofanywa wa baadhi kupiga kura zaidi ya moja na kuweka katika ballot boxes bila kushtukiwa.

Chanzo changu cha habari kimenijulisha kuwa na faili lote la original results. Kama atanitumia basi bila ya shaka na mimi nitawabadikieni hapa.

Naomba kutoa hoja.

UPDATE 1:

Je haya ndiyo Matokeo Halisi (Original) yale ya majumuisho ya vituoni na yale ya NEC ??

UPDATE 2:

Waungwana, nimeongea tena na chanzo changu ambacho ndicho kilichonipatia taarifa hii. Matokeo yaliyoambatanishwa nimejulishwa ni yale ya utafiti wa ndani ambao ulifanywa kabla ya uchaguzi. Actual results nimeambiwa zikitolewa sasa hivi inaweza kusababisha kutoelewana.

Tuvute subira mpaka hapo taarifa ya uhakika itakapotolewa kutoka kwa wahusika.

SM
Du kaka File uliloweka la kura halisi linaonekana ni File lililotumika kwa ajili ya estimates. Kwa Mfano Limezingatia idadi ya wataopiga kura kuwa ni 65% ya wale waliojiandikisha na ndo maana kuan wapiga kura ktk decima places kitu ambacho si sahihi ktk reality,we don't have decimal voters! kingine Ukichkua ushindi wa either kikwete ama Slaa kwa kila mkoa ulikuwa katika Pecentage ambazo hazina decima places e.g 40% 33% e.t.c.Hii ni ishara kubwa ya matokeo haya yalikuwa estimated.Sikatai uchakachuaji wa kula ulifanyika lakini kwa file hili labda lilitumika kabla ya uchaguzi kwa ajili ya planning na matarajio.We need the actual votes kama zilivyochukuliwa vituoni. Hutaona decimal wala percentage kamili kamili.
Nimechangia
 
Ok. tunashukuru mkuu. kumbe SLAA alichobisha ni kushindwa kwa asilimia nyingi ila anakubali kuwa alishindwa pamoja nayeye kuchakachua kura zake ameshindwa kujionyesha mshindi. Nzuri hii JK president yeye wa pili akubali basi.
 
hata kama yangetangazwa matokeo hayo bado jk angetangazwa kuwa rais wa jmt coz kwa mujibu wa katiba ya tz viongoz wetu wanachaguliwa kwa SIMPLE MAJORITY
 
Back
Top Bottom