Haya ndiyo maswahibu kwa abiria wa basi baada ya kuzuia mifuko ya plastiki

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,744
21,194
ROUTE 01: DAR - ARUSHA
11:45 asubuhi Tunaanza safari kutokea shekilango kwa kupitia njia ya Bagamoyo konda wa kike anatangaza na kutukaribisha kwenye basi lao huku akijitanabaisha kuwa wana huduma nzuri kweli kweli. 'labda kuliko mabasi mengine', kisha anawasha TV za jumla na wengine wanajichagulia (self service)

Kama kawaida awamu hii hatuulizani speed za mabasi, (mnajua kinachoendelea) tunafika check point bagamoyo, sioni huduma ya ziada kwa abilia au haikutangazwa ukihitaji ufanye nini. Mara paap tunaitafuta segera konda anagawa maji na soda it's your choice.

Mara nyingi ukipewa mlo, lazima kuna body tissue zinazalisha appetite na mate ya kula yanajaa mdomoni hapa uwe unatapika au hutapiki safarini.

05:30 tukielekea pande za mombo naona uhitaji wa plastic bag za kurudishia chenji zinahitajika kwa speed sana, ila hazipo kutokana na katazo la serikali. Nini kinafuata, baadhi wanafungua madirisha na kutupa chenji nje, wale wenye nguo za ziada wanahifadhi wenyewe, wenye mabasi ya choo wanakimbia kwa haraka kuhifadhi huko.

Tunafika mombo hapo kwenye mojawapo ya hiyo migahawa mikubwa ya wasafiri, naangalia baadhi ya mabasi kwenye bodi zake naona michirizi ya chenji a.k.a matapishi mpaka aridhini hapo hapo mgahawani.

Baada ya kuuliza kwa baadhi ya abilia hakuna hata mmoja anayekupa jibu muswano nini afanye pindi anapopatwa na dharula ya kutapika bali kila mtu amaisingizia serikali kukataza matumizi ya hizo mifuko.

11:50 jioni hatimaye nilifika ninaposhuka, nikawa najiuliza huyu jamaa anawekeza kwenye mabasi na kujiwekea nadhiri ya huduma bora na za kisasa huku akichukua mfano wa huduma bora za Dreamliner iliyokwenda SA juzi na kurudi fasta bongoland ila alishindwa kukopi aina ya mifuko inayotumika kuhifadhia chenji nk.

Wamiliki wa mabasi nawasihi kama siyo ushauri kwenu, kila mtu kwa wakati wake ili uboreshe huduma na abilia waje kwako hebu nenda kiwandani popote wanapozalisha mifuko wakutengenezee mifuko maalumu ya kutapikia a.k.a chenji.

Niliwahi kuelekea pande za Unguja ndani ya kile chombo hata kabla ya kupigwa stop matumizi haya wao wana mifuko yao maalum na ina nembo zao na matangazo ya huduma wanazotoa.

NB.

WanaJF kama unasoma uzi huu angalia fulsa hii kwa kutengeneza mifuko maalum kwa kampuni ya basi na kuwapelekea as sample then chukua deal.

Route 02: Dar - Mwz
Route 03: Dar - Mbeya
Route 04: Dar - Mtwara
n.k hizo 👆 mtajazia huko njiani mnaweka wapi chenji.


SIKU NJEMA KWAKO.
 
Kuta
Kutapika safarini ni uzembe...ujinga....na kujiendekeza..
Ndugu kutapika ni ugonjwa/au tunasema kiwewe cha safari au sababu ya kula vyakula ambavyo hajazoea au kuwepo kwa harufu mbaya ambayo hawezi kuhimili, na huwa inatokea pasipo mtu kuweza kujizuia na ukilazimisha kuzuia utafanya matapishi (chenji) kujilazimisha kuingia kwenye sehemu nyingine ambayo itakuwa hatari zaidi na inaweza kupelekea hata kifo.
Njia mbadala aliyeshauri mleta mada ni muhimu sana
 
Kuta

Ndugu kutapika ni ugonjwa/au tunasema kiwewe cha safari au sababu ya kula vyakula ambavyo hajazoea au kuwepo kwa harufu mbaya ambayo hawezi kuhimili, na huwa inatokea pasipo mtu kuweza kujizuia na ukilazimisha kuzuia utafanya matapishi (chenji) kujilazimisha kuingia kwenye sehemu nyingine ambayo itakuwa hatari zaidi na inaweza kupelekea hata kifo.
Njia mbadala aliyeshauri mleta mada ni muhimu sana

Kama mtu ana tatizo la kurudisha chenji awapo safarini, ni bora akajizuia kula (afunge tu kwa masaa kadhaa) hadi atakapofika mwisho wa safari yake. Kiukweli mambo ya kurudisha chenji huwa yanakera abiria wengine! Bora hata uwe mgonjwa! wengine ni uroho tu wa kufukia kila kitu awapo safarini.
 
Juzi kati nikiwa naelekea huko kusini mwa Tz kuna jamaa alipanda basi pale Tunduru akiwa amevaa kanzu nabaraghashia. baada ya mwendo kidogo alianza kutapika.alipoona hali tete alivua baraghashia akatapikia humo, hali ilipozidi alivua kanzu akaviringishia ,safari ikaendelea. Hatari sana
 
Kama wamekutoboa hilo tundu litakuwa tendo lisilo la hiyari ila kama wewe ni mwanaume basi unaweza kujizuia kupumua kupitia njia ya haja kubwa.
Ndugu acha tu ubishi usio na mana. Farting ni involuntary action. Wewe unaongelea kutoa sauti kwa kitendo hicho na sio kitendo chenyewe. Kujamba ni lazima, huwezi zuia ejection yake bali unaweza control how it ejects.
 
Back
Top Bottom