Mwakaboko King
JF-Expert Member
- Apr 22, 2015
- 1,099
- 207
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilianzishwa tarehe 13 Januari, 1993, kwa mujibu wa Ibara ya 74 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 baada ya kurejeshwa kwa Mfumo wa Vyama vingi vya Siasa nchini Tanzania mwaka 1992.
Kwa mujibu wa Ibara ya 74 (7) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni Idara huru inayojitegemea. Aidha, Ibara ya 74(11) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza kuwa Tume katika kutekeleza majukumu yake ya Kikatiba haitalazimika kupokea maelekezo au amri kutoka kwa mtu yeyote au Idara yoyote ya Serikali au kufuata maoni ya Chama chochote cha Siasa.
Majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi yameainishwa katika Ibara ya 74 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kama ifuatavyo:
(i) Kusimamia na Kuratibu Uandikishaji wa Wapiga Kura katika Uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuri ya Muungano;
(ii) Kusimamia na kuratibu uendeshaji wa Uchaguzi wa Rais na Wabunge;
(iii) Kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya Uchaguzi wa Wabunge;
(iv) Kusimamia na kuratibu uandikishaji wa Wapiga Kura na uendeshaji wa Uchaguzi wa Madiwani.
(v) Kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.
Majukumu mengine ya Tume kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa ni pamoja na yaliyotajwa katika kifungu cha 4C cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, ambayo ni,
(i) Kutoa Elimu ya Mpiga Kura kwa nchi nzima, kuratibu na kusimamia watu wanaotoa Elimu hiyo.
(ii) Kuteua na kuwatangaza Wabunge na Madiwani Wanawake wa Viti Maalum.
Source: NEC Website.