Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,597
- 215,270
Haya ndiyo maisha ya takriban 70% ya Watanzania. Bado tunapigana na maadaui tuliowarithi kwa Wakoloni miaka 60 imiyopita Ujinga, maradhi na umasikini.
Mtoto anaezaliwa katika nyumba hii anategemewa akue salama, fikiria changamoto za kudhibiti mbu katika nyumba hii na uepukane na malaria.. Wakazi wa nyumba hii wanahitaji maji safi na salama ya kunywa.
Ukifanya utafiti ya wenye ajira za kudumu katika eneo hili atakua ni Mtendaji wa mtaa, na watu kama watano ofisini. Hakuna mradi ulioanzishwa karibu na hapa unaotoa ajira kwa vijana.
Hili si Tatizo la Tanzania tu, nchi nyingi za Afrika zimeshindwa kuzalisha ajira baada ya uhuru, matokeo yake vijana wengi wanapeleka nguvu kazi katika nchi zenye uchumi imara angalau waweze kuwa tumia wazazi wao mkate. Nguvu hizi zingetumika vyema Afrika zingeketa maendeleo kwetu.
Tusichekane tuangalie jinsi tunavyoweza kujinasua katika mtego huu.