Haya ndiyo Maendeleo (Picha)

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
3565.jpg


Shimo kubwa ambalo lililopo katika barabara ya Morogoro karibu na NSSF jijini Dar es Salaam. (Picha na Hamisi Athumani)

My Take:

Kwa aliye kwenye Benz ameendelea sana; kwa anayetembea kwa miguu anaona maendeleo ya mwenye Benz na kuyatamani. Kwa mhandisi wa barabara, na yeye anatamani kuwa na Benz na viongozi wa Halmashauri wanajiuliza ni jinsi gani wataweza kuagiza Benz kwa watendaji wake.
 
Na hapo yalikuwa ni Makao makuu ya Nchi (Kwa sasa ni Makao Makuu lakini -Kimawazoni). Halafu bado kuna member mmoja ajulikanae kama Kasheshe anadai kwenye thread nyingine Quote "haya mambo ya say TZS Billioni 800; ukiachilia mbali TZS Billioni (1) Moja ya Mzee wa Vijisenti hazileti kitu chochote significant kwenye taifa letu changa". Hivi kweli hiyo pesa haiwezi kuwa na significancy kwa Mtanzania, kweli..kweli....kweli. Tusilete Comedy kwenye mambo muhimu yanayohusu nchi yetu na wananchi kwa ujumla.
 
Lakini siku hizi watu wanaweza kununua mabenzi, mahammer, kwenda shopping za nguvu hata majuu na kununua vitu bwelele! Haya ndio maendeleo jamani. Kwani yale mabilioni ya "Kikwete" yalikuwa na lengo gani si kujaza watu mapeza mifukoni?
 
Mwanakijj,
Kitu kimoja kimenishangaza Bongo, watu wanakualika kwenye nyumba zao za kisasa;nzuri tu pale Mikocheni, au Masaki, Oyster Bay. Lakini unapokaribia kitu cha kwanza unachoona ni barabara isiyopitika ila tu kama una trekta. Sasa mimi nimeamua nitakaporudi Bongo kitu
cha kwanza nanunua trekta la kulainisha barabara. Kwa sababu gari langu la mwaka 47 litakong'oloka kwenye barabara hii baada ya wiki mbili tu.
 
na mkuu wa mkoa yupo hapahapa kalala tu?
na hii ndo tabu ya kuchukua marafiki uje ulipe fadhira matokeo yake ndo wanaharibu kazi lawama inamuendea yeye sasa
 
I am shua zisi izi paintshop job.

Nzoka, unajua nini mkuu..... viongozi wetu wanapotembelea nje ya nchi na kujionea yaliyoko huko nadhani wanafikiria vivyo hivyo, yaani "maendeleo yote waliyo nayo huko ni photoshop job" ya viongozi wa nchi hizo!!

Mtu akivunja mguu hapo ataambiwa ni uzembe wake...... hii nayo itakuwa 'photoshop job' ya Mwenyezi Mungu!!

Kadiri mashimozzzz hayo yanavyo achiwa kupanuka, ndivyo gharama zaidi zinaongezeka za ukarabati... hii nayo ni 'photoshop job' ya serikali yetu!!!!!!


Good thing Nyani Ngabu hayupo leo, na yule The Truth naye kafungiwa...

Baadae..
 
na mkuu wa mkoa yupo hapahapa kalala tu?
na hii ndo tabu ya kuchukua marafiki uje ulipe fadhira matokeo yake ndo wanaharibu kazi lawama inamuendea yeye sasa

...na ikitokea wamejitokeza kukarabati shimo hilo, watatumia kifusi na kulifunika kwa mchanga.... mambo mwendo mdundo!!

... Gang, si unajua jinsi mchanga unavyoharibu lami... basi, umeshajionea jinsi vile mchanga unavyozolewa kutoka barabarani wakati wanasafisha barabara halafu unawekwa pembeni tu na baada ya siku mbili wote unakuwa umesharudi barabarani tena.... shame shame shame, yaani saa nyingine mtu unatamani ung'atuke tu na kuwa wa jamii nyingine... but again, you can't do that, ni bora ubakie hapa hapa na kugombana na watu wakati ukiwahimiza utendaji bora wa mambo so soo basic!!
 
Hata ulaya kuna mashimo barabarani;
M450d79d10d0a0.gif


cool_street_painting.jpg


Bongo New York bana. Au tambarare.

Lakini kusema ukweli hiyo rami nyembamba ile mbaya. Yaani imekonda ki-ufisadi fisadi tu. Unaweza ukaingiza mkono halafu ukavunja hiyo rami kama unavyomega ukoko wa ugali.
 
Nakumbuka kulikuwa nakampuni ya wazawa ya kutengeneza barabara ambayo iliwaomba kina Kimbisa na Kandoro contract ya kuziba mashimo jijini kwa malipo ya madafu...na hii kampuni inavyo vifaa na maengineer waliokubuhu wengine kutoka enzi za commworks....wakaambiwa ati jiji halina fungu la pesa ya kutosha za kukarabati.

Ukweli wa mambo hawa manationalist hawkuwa tayari kutoa 10% ambayo imekuwa dini katika serikali yetu ya bongo.
 
Kipi bora? Kutengeneza barabara hiyo au kununua magari mazuri ya kutufanya tujisikie vizuri?
 
Kipi bora? Kutengeneza barabara hiyo au kununua magari mazuri ya kutufanya tujisikie vizuri?
....Well according to government philosophy, ni bora watembelee kwenye mashangingi kwa lengo la kukwepa mashimo kama hayo.... kwao, ni bora gharama za magari ya kianasa yenye gharama kubwa kuya run kuliko kutengeneza barabara za kupitia magari hayo...

....ooh, may be ni 'bora tiba kuliko kinga'!!
 
Nzoka, unajua nini mkuu..... viongozi wetu wanapotembelea nje ya nchi na kujionea yaliyoko huko nadhani wanafikiria vivyo hivyo, yaani "maendeleo yote waliyo nayo huko ni photoshop job" ya viongozi wa nchi hizo!!

Mtu akivunja mguu hapo ataambiwa ni uzembe wake...... hii nayo itakuwa 'photoshop job' ya Mwenyezi Mungu!!

Kadiri mashimozzzz hayo yanavyo achiwa kupanuka, ndivyo gharama zaidi zinaongezeka za ukarabati... hii nayo ni 'photoshop job' ya serikali yetu!!!!!!


Good thing Nyani Ngabu hayupo leo, na yule The Truth naye kafungiwa...

Baadae..

Hey I'm baack!!

U already know what it is....
 
Nyinyi kubalini tu...halafu baada ya hapo ndo muanze mikakati ya nini kifanyike...
Kuendelea kuwa kwenye denial hakusaidii chochote zaidi ya kuendeleza matatizo....
 
ndio kikwete akienda safari za nje, anawaambia watu warudi tanzania maana kila kitu kilichoko ulaya na bongo kipo.
alitoa mfano magari ya kifahari, majumba mazuri sana kuliko hata za ulaya, na vyakula vizuri, alichoshindwa kusema ni kuwa hivyo ni kwa watu wachache mno.
 
Hilo benzi si kama la ubalozi? Hizo nambaplets naona kama ni za kijani! Ndiyo maana wanatuona basket case! Hatubebeki.
 
Back
Top Bottom