Uchaguzi 2020 Haya ndiyo ambayo Tundu Lissu hukuyasema

Afande Fojuman

JF-Expert Member
Sep 27, 2014
650
534
1. Tundu Lissu umetangaza nia ya kugombea Urais lakini hukuweka wazi nia yako ya kuutaka Urais, badala yake umeanza na kampeni ya kusema mengi unayodhani Rais Magufuli amekosea.

2. Hujaweka wazi chanzo cha mapato yako kwamba unaishi Ulaya kwa gharama za nani? Watanzania hatuhitaji Rais ambaye anaingizwa madarakani kwa nguvu ya fedha ya watu wasiojulikana.

3. Hujaweka wazi kwamba unaishi Ulaya kwa status” ipi? Maana uliingia Ubelgiji kwa visa ya mgonjwa ulikwenda kutibiwa, lakini sasa umepona na unaendelea kuishi Ulaya, hujaweka wazi kama una “asylum” maana wenye hifadhi ya kisiasa kimsingi hawaruhusiwi kuendesha siasa za kupinga serikali zao.

4. Nakukumbusha ambayo Magufuli anakuzidi kwa mbali, alipoingia madarakani alipambana bila woga na unyonyaji ambao Tanzania ilikuwa ikionelewa na wachimba madini wasio waaminifu. Wewe ulisimama upande wa ACACIA ukidai kwamba ripoti ya kitaalamu iliyofunua ukweli kuhusu makinikia uliita “rubbish.” Mtu unayesimama upande wa wanyonyaji hutawafaa Watanzania.

5. Nakukumbusha kwamba Magufuli tangu aingie madarakani katika miaka mitano hajaenda Ulaya wala Marekani kuombaomba. Kumbuka Rais Trump amewaita wasomi aina yako yaani wasomi wanaotegemea misaada ya Ulaya kuwa ni “shameless beggars” hilo halikukuuma. Wakati Trump anatoa kauli hiyo ya masimango wewe ndio ulikuwa umepamba moto kuzunguka London, Berlin, Paris, Washington na Toronto. Magufuli unayemponda alisema mapema kabla hata Trump hajatoa kauli yake, Magufuli alisema haukubali mkate wa masimango.

6. Unajivunia kuzungukia mabara yote ya dunia, huna tofauti na Marais wanaoitukanisha Afrika ambao kila mwaka wanakwenda Ulaya kuhiji “Paris club.” Wanakwenda kuwaangukia wahisani ili wasaidiwe, Tanzania bado inamhitaji Magufuli ambaye kwa miaka mitano hajaenda Ulaya kuhiji anairudisha Tanzania yetu kwenye misingi ya kujitegemea.

7. Umedai Magufuli amevuruga diplomasia na uhusiano wa kimataifa umetoa mfano wa Shirika la Afya WHO, nakukumbusha kwamba Magufuli ameipaisha Tanzania kwenye kipindi cha “corona” kuliko wakati mwingine wowote. Magufuli alipoufunua ukweli kuhusu vifaa vya kupimia “covid 19” kwamba vinatoa matokeo yasiyo na uhakika, dunia ya wenye akili timamu ilimjadili na waungwana walimheshimu zaidi. Magufuli angekuwa alisema uwongo, watengenezaji wa vifaa hivyo wangemjibu ama wangeweza hata kumshitaki, lakini walikaa kimya kwasababu aliyoyafunua ni kweli tupu.

8. Nakukumbusha kwamba wakati dunia inahamanika “panic” kutiokana na jinamizi la “corona” Magufuli hakuikubali “lockdown.” Kwanza dunia haikumwelewa, lakini baadaye ilipomwelewa Marais makini wa dunia hii wameiiga Tanzania. Ingekuwa ninyi wenye sifa ya kuwa “adoptive” mngekuwa ndio mko madarakani, Tanzania ingeteswa na “covid 19” kuliko mabaya mengine yote yaliyowahi kuitesa nchi hii. Mngekuwa ninyi mlio hodari wa kupokea yatokayo nje pasipo kuyachuja, leo Watanzania tungekuwa tunasota mahabusu tukiitumikia “lockdown.”

9. Nakukumbusha kwamba sasa hivi “covid 19” siyo tishio tena kwa Watanzania, chini ya shujaa Magufuli tumeishinda “corona.” Ukitaka kuhakikisha waambie Wabelgiji wanaokutunza waelekeze kamera zao Kariakoo, Manzese na stendi ya ubungo, muone wananchi wanavyoendelea na shughuli zao kwa uhuru na hakuna maiti zilizozagaa barabarani wala hata wanaozimia. Wapiga debe wanapiga kelele zao bila “baracoa” wala hawazimii, waumini wanakusanyika kwenye nyumba za idada wala hakuna wafao kwa maelfu, kama waongo walivyotabiri. Ninyi “adoptive” mngekuwa ndio mnatawala Watanzania tusingeyafurahia mazuri tunayofurahia chini ya Magufuli.

10. Mwisho nakukumbusha ambalo hukulisema, nalo ni kuhusu mchango wako au “role” yako katika kuwaelekeza wasiolitakia mema shirika la ACTL. Uliwasaidia kukamata Ndege zetu huko Afrika kusini na Canada, maana hayo ulianza kuyasema mapema Bungeni kabla hujaenda Ulaya, kwamba mali zetu zitakamatwa. JE, wewe uliyefanya kama Yuda Iskariote aliyewaongoza wabaya akawaonyesha Yesu alipo, nawe ukawaonyesha wabaya wetu Ndege zetu kwamba zipo Canada na Afrika kusini, wakaenda kuzikamata kweli una manufaa kwa Tanzania?
 
Mnajisumbua tu na lisu!
Lisu sahivi kaja kujipima ubavu tu,wanasoma upepo ili wajue 2025 wataendaje.
 
1. Tundu Lissu umetangaza nia ya kugombea Urais lakini hukuweka wazi nia yako ya kuutaka Urais, badala yake umeanza na kampeni ya kusema mengi unayodhani Rais Magufuli amekosea.

2. Hujaweka wazi chanzo cha mapato yako kwamba unaishi Ulaya kwa gharama za nani? Watanzania hatuhitaji Rais ambaye anaingizwa madarakani kwa nguvu ya fedha ya watu wasiojulikana.

3. Hujaweka wazi kwamba unaishi Ulaya kwa
status” ipi? Maana uliingia Ubelgiji kwa visa ya mgonjwa ulikwenda kutibiwa, lakini sasa umepona na unaendelea kuishi Ulaya, hujaweka wazi kama una “asylum” maana wenye hifadhi ya kisiasa kimsingi hawaruhusiwi kuendesha siasa za kupinga serikali zao.

4. Nakukumbusha ambayo Magufuli anakuzidi kwa mbali, alipoingia madarakani alipambana bila woga na unyonyaji ambao Tanzania ilikuwa ikionelewa na wachimba madini wasio waaminifu. Wewe ulisimama upande wa ACACIA ukidai kwamba ripoti ya kitaalamu iliyofunua ukweli kuhusu makinikia uliita “rubbish.” Mtu unayesimama upande wa wanyonyaji hutawafaa Watanzania.

5. Nakukumbusha kwamba Magufuli tangu aingie madarakani katika miaka mitano hajaenda Ulaya wala Marekani kuombaomba. Kumbuka Rais Trump amewaita wasomi aina yako yaani wasomi wanaotegemea misaada ya Ulaya kuwa ni “shameless beggars” hilo halikukuuma. Wakati Trump anatoa kauli hiyo ya masimango wewe ndio ulikuwa umepamba moto kuzunguka London, Berlin, Paris, Washington na Toronto. Magufuli unayemponda alisema mapema kabla hata Trump hajatoa kauli yake, Magufuli alisema haukubali mkate wa masimango.

6. Unajivunia kuzungukia mabara yote ya dunia, huna tofauti na Marais wanaoitukanisha Afrika ambao kila mwaka wanakwenda Ulaya kuhiji “Paris club.” Wanakwenda kuwaangukia wahisani ili wasaidiwe, Tanzania bado inamhitaji Magufuli ambaye kwa miaka mitano hajaenda Ulaya kuhiji anairudisha Tanzania yetu kwenye misingi ya kujitegemea.

7. Umedai Magufuli amevuruga diplomasia na uhusiano wa kimataifa umetoa mfano wa Shirika la Afya WHO, nakukumbusha kwamba Magufuli ameipaisha Tanzania kwenye kipindi cha “corona” kuliko wakati mwingine wowote. Magufuli alipoufunua ukweli kuhusu vifaa vya kupimia “covid 19” kwamba vinatoa matokeo yasiyo na uhakika, dunia ya wenye akili timamu ilimjadili na waungwana walimheshimu zaidi. Magufuli angekuwa alisema uwongo, watengenezaji wa vifaa hivyo wangemjibu ama wangeweza hata kumshitaki, lakini walikaa kimya kwasababu aliyoyafunua ni kweli tupu.

8. Nakukumbusha kwamba wakati dunia inahamanika “panic” kutiokana na jinamizi la “corona” Magufuli hakuikubali “lockdown.” Kwanza dunia haikumwelewa, lakini baadaye ilipomwelewa Marais makini wa dunia hii wameiiga Tanzania. Ingekuwa ninyi wenye sifa ya kuwa “adoptive” mngekuwa ndio mko madarakani, Tanzania ingeteswa na “covid 19” kuliko mabaya mengine yote yaliyowahi kuitesa nchi hii. Mngekuwa ninyi mlio hodari wa kupokea yatokayo nje pasipo kuyachuja, leo Watanzania tungekuwa tunasota mahabusu tukiitumikia “lockdown.”

9. Nakukumbusha kwamba sasa hivi “covid 19” siyo tishio tena kwa Watanzania, chini ya shujaa Magufuli tumeishinda “corona.” Ukitaka kuhakikisha waambie Wabelgiji wanaokutunza waelekeze kamera zao Kariakoo, Manzese na stendi ya ubungo, muone wananchi wanavyoendelea na shughuli zao kwa uhuru na hakuna maiti zilizozagaa barabarani wala hata wanaozimia. Wapiga debe wanapiga kelele zao bila “baracoa” wala hawazimii, waumini wanakusanyika kwenye nyumba za idada wala hakuna wafao kwa maelfu, kama waongo walivyotabiri. Ninyi “adoptive” mngekuwa ndio mnatawala Watanzania tusingeyafurahia mazuri tunayofurahia chini ya Magufuli.

10. Mwisho nakukumbusha ambalo hukulisema, nalo ni kuhusu mchango wako au “role” yako katika kuwaelekeza wasiolitakia mema shirika la ACTL. Uliwasaidia kukamata Ndege zetu huko Afrika kusini na Canada, maana hayo ulianza kuyasema mapema Bungeni kabla hujaenda Ulaya, kwamba mali zetu zitakamatwa. JE, wewe uliyefanya kama Yuda Iskariote aliyewaongoza wabaya akawaonyesha Yesu alipo, nawe ukawaonyesha wabaya wetu Ndege zetu kwamba zipo Canada na Afrika kusini, wakaenda kuzikamata kweli una manufaa kwa Tanzania?
Lissu kachanganyikiwa,ni wakuhurumiwa tu
 
Mkuu umenena vyema sana badala ya kusema kwanini anakuhiraji urais yeye anaendeleza Manung'uniko.

Tanzania sasa hivi inatunga na kuimba nyimbo zake yenyewe ile biashara ya kutungiwa na kutengenezewa melod sisi tuimbe Kama kasuku ilishapita ikaenda
 
Umemaliza??

Basi kakojoe ulale,kwa sababu hujui kitu,ama unaelewa na unajifanya kutoelewa.
 
Unataka kujua gharama za matibabu? Unauliza Leo wakati alidai fedha na mshahara wake mlikaa kimya mkajidai hamna taarifa kuwa anafanya matibabu nje ? Kumbe mnafahamu!

Kabla sija kupa majibu waambie watanzania kuwa kulikuwa mnafahamu kuhusu matibabu yake na bunge na serikali Yanu ilikataa kutoa fedha kwa sababu gani.

Mkimaliza kueleza hayo kwa kupitia vyombo vya habari nitakupa majibu yako, Lkn kwa sasa siwezi kukupa majibu, endelea na siasa zako maji tope
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom