Haya ndio ya kusisitiza zaidi kwa Taifa muda huu

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
`
hapa wanaambiwa waislam na pia ni vizuri watanzania wengine na wenye dini tuhimizane kuchapa kazi
Waislamu msikae vijiweni kucheza bao, fanyeni kazi`

2007-10-14 09:37:13
Na Mwandishi Wetu


Naibu Sheikh wa Mkoa wa Lindi, Sheikh Said Mushagani, amehimiza Waislamu kufanyakazi kwa bidii badala ya kukaa vijiweni kucheza bao na dhumna.

Akitoa hotuba ya pili katika Swala ya Idd El Fitr iliyoswaliwa katika viwanja vya Ikulu mjini Lindi Sheikh Mushagani, alisema kuna baadhi ya Waislamu wanaojifanya kuwa wanaishi maisha ya kiahera na kila wanapoguswa hujibu `mimi inshallah mambo yangu yako ahera`.

Aliwaambia bado wanaishi duniani na hakuna anayeishi ahera hivyo kufanyakazi na kutegemeza maisha ya hapa duniani ni lazima ili Mwenyezi Mungu azibariki jitihada zao na kuwapa mafanikio.

Aliwakumbusha kuwa Mtume Mohammad S.A.W. na Mashwahaba walifanyakazi kwa bidii na kuhimiza kuwaiga kwani hiyo ni ibada inayompasa kila Muislamu.

Sheikh Mushagani, alitoa mfano wa Hadithi za Mtume Mohammad, aliyempongeza na kumshika mikono Swahiba aliyekuwa ametoka kibaruani akiwa na mikono michafu kwa kumsalimia na kumwinua mikono yake na kumsifu mfanyakazi huyo mwadilifu anayetafuta riziki.

`Tusikae kucheza bao wala dhumna na kusema maneno mengi bila kutafuta riziki. Waislamu kufanyakazi ni ibada`, alisema katika hotuba yake.

Aliendelea kukumbusha hadithi nyingine ya Mtume ambaye alikuta muumini akishinda kwenye nyumba ya ibada na kuswali alfajiri, Alasiri, isha na magharibi na akamwambia kuwa ibada yake bila kazi ni sawa na bure.

`Baada ya kuswalisha isha Mtume akamuuliza muunini yule unakula nini wewe, chakula unapata wapi wewe?

Akajibu mimi nina ndugu yangu anafanyakazi , mkiondoka ananiletea bakuli la chakula mimi namtakabili Mwenyezi Mungu `alisema ibada pekee bila kazi maisha hayawezi kufanikiwa.

`Dini ipo tushikamane kiimani lakini pia kazi ipo tufanye na tutekeleze wajibu katika Korani na katika maisha yetu`.

Alionya: `Tuache kucheza bao kutwa nzima, kukaa bila kazi na pia tukumbuke kuwaheshimu viongozi wetu wote.Masheikhe, viongozi wakuu wa nchi, maulamaa, maimamu viongozi wanaotuongoza kiimani katika maisha yetu.`

Sheikh wa Mkoa wa Lindi, Suleimani Gorogosi, akizungumza katika hotuba ya pili pamoja na kugusia umuhimu wa kufanyakazi pia aliitaka serikali kuangalia suala la umaskini wa watu wa kipato cha chini ambao wameathiriwa na mzunguko wa fedha.

Alisema ili nchi iwe na baraka tunawaomba viongozi muangalie matatizo ya mzunguko wa pesa na matatizo ya maisha ya watu wa hali ya chini.

SOURCE: Nipashe
 
Hotuba ya shehe Mshangani naomba Chadema ichukueni iambatanisheni na ile sera mpya mnayosambaza wasambazieni wanachama wenu.Wapeni sera na hiyo hotuba ya naibu shehe mkuu wa Lindi Said Mshangani itawasaidia watu wenu waache kupiga domo vijiweni wafanye kazi
 
Mujarabu huu ujumbe kwa bavicha pia..sio kushinda ufipa tu kila siku kumsubiria mbowe..huko ni sawa na kucheza bao..matokeo yake mbowe anaishia bahari beach hotel wao wanarudi nyumbani wanapiga miayo..wakiulizwa wanasema ridhki zao zipo ufipa..
 
Back
Top Bottom