Haya ndio ya kusisitiza zaidi kwa Taifa muda huu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya ndio ya kusisitiza zaidi kwa Taifa muda huu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtu wa Pwani, Oct 14, 2007.

 1. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2007
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  `
  hapa wanaambiwa waislam na pia ni vizuri watanzania wengine na wenye dini tuhimizane kuchapa kazi
  Waislamu msikae vijiweni kucheza bao, fanyeni kazi`

  2007-10-14 09:37:13
  Na Mwandishi Wetu


  Naibu Sheikh wa Mkoa wa Lindi, Sheikh Said Mushagani, amehimiza Waislamu kufanyakazi kwa bidii badala ya kukaa vijiweni kucheza bao na dhumna.

  Akitoa hotuba ya pili katika Swala ya Idd El Fitr iliyoswaliwa katika viwanja vya Ikulu mjini Lindi Sheikh Mushagani, alisema kuna baadhi ya Waislamu wanaojifanya kuwa wanaishi maisha ya kiahera na kila wanapoguswa hujibu `mimi inshallah mambo yangu yako ahera`.

  Aliwaambia bado wanaishi duniani na hakuna anayeishi ahera hivyo kufanyakazi na kutegemeza maisha ya hapa duniani ni lazima ili Mwenyezi Mungu azibariki jitihada zao na kuwapa mafanikio.

  Aliwakumbusha kuwa Mtume Mohammad S.A.W. na Mashwahaba walifanyakazi kwa bidii na kuhimiza kuwaiga kwani hiyo ni ibada inayompasa kila Muislamu.

  Sheikh Mushagani, alitoa mfano wa Hadithi za Mtume Mohammad, aliyempongeza na kumshika mikono Swahiba aliyekuwa ametoka kibaruani akiwa na mikono michafu kwa kumsalimia na kumwinua mikono yake na kumsifu mfanyakazi huyo mwadilifu anayetafuta riziki.

  `Tusikae kucheza bao wala dhumna na kusema maneno mengi bila kutafuta riziki. Waislamu kufanyakazi ni ibada`, alisema katika hotuba yake.

  Aliendelea kukumbusha hadithi nyingine ya Mtume ambaye alikuta muumini akishinda kwenye nyumba ya ibada na kuswali alfajiri, Alasiri, isha na magharibi na akamwambia kuwa ibada yake bila kazi ni sawa na bure.

  `Baada ya kuswalisha isha Mtume akamuuliza muunini yule unakula nini wewe, chakula unapata wapi wewe?

  Akajibu mimi nina ndugu yangu anafanyakazi , mkiondoka ananiletea bakuli la chakula mimi namtakabili Mwenyezi Mungu `alisema ibada pekee bila kazi maisha hayawezi kufanikiwa.

  `Dini ipo tushikamane kiimani lakini pia kazi ipo tufanye na tutekeleze wajibu katika Korani na katika maisha yetu`.

  Alionya: `Tuache kucheza bao kutwa nzima, kukaa bila kazi na pia tukumbuke kuwaheshimu viongozi wetu wote.Masheikhe, viongozi wakuu wa nchi, maulamaa, maimamu viongozi wanaotuongoza kiimani katika maisha yetu.`

  Sheikh wa Mkoa wa Lindi, Suleimani Gorogosi, akizungumza katika hotuba ya pili pamoja na kugusia umuhimu wa kufanyakazi pia aliitaka serikali kuangalia suala la umaskini wa watu wa kipato cha chini ambao wameathiriwa na mzunguko wa fedha.

  Alisema ili nchi iwe na baraka tunawaomba viongozi muangalie matatizo ya mzunguko wa pesa na matatizo ya maisha ya watu wa hali ya chini.

  SOURCE: Nipashe
   
Loading...