Haya ndio matunda ya mateso na taabu za wabunge wa upinzani

monjozee

Senior Member
Sep 19, 2016
115
297
HAYA NDIYO MATUNDA YA MATESO NA TAABU ZA WABUNGE WA UPINZANI BUNGENI.

Ni dhahiri kuwa Wabunge wa upinzani na viongozi wa vyama vya upinzani nchini tangu mwaka 2005 wamejizatiti sana kuchomoza na kuendelea kuonesha umuhimu wao katika Taifa la Tanzania kwa kupigania na kulinda raslimali za nchi hii kwa maslahi makubwa wa vizazi vilivyopo na vijavyo.
Kamwe kwa sasa kama Watanzania hatuwezi kufurahia kupuuza wa kuzisahau jitihada kubwa za Wabunge na viongozi wa vyama vya upinzani.

Tutakubaliana kuwa masakata mengi ya wizi, ufisadi na ufujaji wa mali za umma nchini yamekuwa yakiibuliwa na wabunge wa upinzani Bungeni, na kwa bahati mbaya huonekana kama "vichaa" na kubezwa na wabunge wa chama tawala, lakini wamekuwa wakisimamia kile wanachokiamini juu ya Taifa lao hadi upatikanaji wa muafaka, jambo ambalo huleta mshangao na aibu kubwa kwa Wabunge wa chama tawala.
Hakika huu ndiyo upinzani, yaani upinzani ule unaoweza kuiona kesho ambayo kabla yake mtawala hajaiona.

Kimsingi hiyo ndiyo maana halisi ya "Uzalendo".Maana haswa ya uzalendo ni pale unapoamua kuitetea nchi yako kwa jambo fulani lenye manufaa juu yake na kukufanya uonekane uko tofauti na wengi, kiasi cha kufikia kutengwa na kutukanwa matusi mbalimbali kwa ajili ya nchi yako, lakini kesho yake unabaki kuwa mshindi katika yale uliyosimamia.

Watanzania sasa ni wakati wa kutambua michango ya Wabunge na viongozi wa upinzani walioanzisha "spirit" ya ujasiri na uzalendo kwa nchi yao na kuwaambukiza Watanzania vijana wanaokuja.
Ni wakati wa kutambua mchango mkubwa wa chama cha CHADEMA na wabunge pamoja na viongozi wake kama ifuatayo (kwa maoni yangu);

1. Freeman Mbowe
2.Tundu Lissu
3. Dr. Wilbroad P.Slaa
4. Zitto Kabwe
5. David Kafulila
6. John Mnyika

Hapo ni kwa kuwataja baadhi tu, ambao walikubali kuhatarisha maisha yao kwa ajili ya kuusema ukweli kwa maslahi ya nchi hii.
Kuna watu waliitwa majina ya wanyama "tumbili",wengine wakapewa majina mbalimbali kama "wahujumu uchumi", "vibaraka" lakini waliendelea kuisimamia haki na kweli.

Watanzania ni lazima tufahamu kuwa, kujitoa hadharani na kuwatamka vigogo wanaohujumu uchumi na mafisadi siyo kujitoa hadharani na kumtaja "kibaka aliyekwapua nyanya kwa mama ntilie",HAPANA!! hii ni kazi inayohitaji moyo wa kujitoa. Unapomtaja kigogo kama Basil Mramba au Chenge ama Seth, ni lazima ufahamu kuwa usiku unaofuata utalala wapi??

Inaumiza sana kuona kuna makada wa CCM wanaubeza upinzani wa nchi hii. Nawashauri usemeni ukweli nayo kweli itawaweka huru,... muda wa vijembe na propaganda haupo kwa sasa, kwa kuwa Watanzania wengi tunafahamu jitihada na uzalendo mkubwa wa wapinzani wa nchi hii.
Ikumbukwe Wabunge wa CCM wamekuwepo miaka yote, lakini kwa sababu ya kulinda maslahi ya chama wamekuwa wakijivika vazi la unafiki na kuliacha vazi la uzalendo.

Watanzania tuendelee kuwaunga mkono wabunge wa upinzani, wawapo ndani ya bunge ama nje ya Bunge.
Pia, kuna haja ya kuwapa tuzo wabunge wanaojitoa kwa kiwango hiki kikubwa cha uzalendo wa Taifa lao.

Joseph Mohonia Politician
 
Tutahakikisha jizi kubwa lililokuwa linatangatanga nchi za watu kutafuta wateja wa kuwauzia mali za watanzania na sasa linavunga kuwa liko kijijini linafuga na kulima mahindi pembezoni mwa msata.


Swissme
 
Mkuu monjozee,uzi huu una jambo la msingi sana. Kuwatambua tu wale waliokuwa wakipigania maslahi ya Taifa ni moja ya hatua za kutengeneza "uzalendo" kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Nawapa kongole wote waliotajwa na ambao hawakutajwa ambao mchango wao katika kutetea maslahi ya Tz hauna mashaka.
 
Back
Top Bottom