Haya ndio masomo yote wanayosoma shule za international: Scheme of work

Iziwari

Member
Jun 5, 2021
76
56
Kama ulitaka kujua masomo ambayo yanafundishwa kwenye shule za international. Hapa ntakuonesha masomo yote na topics mbali mbali wanazojifunza. Ili wewe kama mwanafunzi ujue masomo ambayo ungejiendeleza kujifunza. Ata ukiwa mtandaoni, maana dunia ya sasa unaweza ukajifunza kitu chochote kwa kupitia chanzo Zaidi ya kimoja.

Hapa tutaangalia kwanza, kwanzia shule za msingi ni vitu gani wanavojifunza. Pia kama utapenda kuendelea kufanya uchunguzi. Utajua Zaidi ni masomo gani wanajifunza wakiwa secondary.

Mara nyingi tumekuwa tukitafuta shule nzuri kwa ajili ya wanafunzi wetu. Tukiamini kuwa shule inayofaulisha sana ndio shule nzuri. Na sa nyingine inatokea, matokeo ya shule yanashuka na kupanda kutokana na mwaka husika wa masomo.

Kwaio tukiangalia tu ufaulu wa wanafunzi kutokana na mwaka husika tunakuwa hatujaangalia vizuri.

Kikubwa cha kuangalia hapa ni walezi na walimu waliojitolea kwa moyo kumfundisha mwanao. Kama wanauwezo wa kutosha, na kama ni mbinu gani watatumia mpaka kumfanya mwanao aweze kuwa msomi mzuri.

Kingine ni kwamba kuna shule hazifundishi jinsi ya kusoma, bali zinafundisha tu masomo. Hii hupelekea mwanafunzi kushindwa kujua njia nzuri ya kujisomea. Na baada ya hapo kushindwa kufanya vizuri kwenye masomo yake.

Tukiangalia shule nyingi, wanafunzi wake huwa wanaamua kujisomea jinsi wanavotaka. Nikimaanisha kuwa, wengine watatumia notes, au wengine watatumia summaries na wengine watatumia vitabu.

Lakini inatulazimu tujue kuwa, mfumo wa kumjenga mwanafunzi unaanzia kwenye kumlazimisha kusoma kwa njia zinazokubalika duniani.

Na moja ya njia nzuri ni kusoma kwa kupitia vitabu mbali mbali. Au kusoma vitabu.

Hii inajirudia tena na tena, kwamba wanafunzi wanaojijenga kwenye kusoma vitabu ndio wanafunzi wenye ufaulu mzuri na ndio viongozi wa baadae. Na pia ndio wanafunzi wenye uwezo mkubwa sana wa kufikiria, kulinganisha na wale wanaosoma kwa njia za kutaka tu kufaulu.

Tufahamu pia, mfumo wa elimu unaokubalika duniani, ni mfumo utakaomuwezesha mwanafunzi kuweza kutatua matatizo mbali mbali. Na sio mfumo wa kufaulu vizuri kwa kukariri na kushindwa kutatua matatizo yalio mzunguka.

Na pia ningependa kuwakumbusha wazazi wote, kwamba, tabia ya mtoto inaanza kujengwa akiwa na miaka 10. Nikiwa na maana kuwa, hapa ndio unatakiwa kumsimamia mwanao kusoma vitabu badala ya kumuacha apoteze mda.

Maana mwanafunzi anaejizoesha kusoma vitabu, anajijengea tabia nzuri. Tabia ambayo inampelekea akikutana na tatizo, kurudi kwenye vitabu na kusoma njia ya kulitatua.

Ila tunaona wasomi wengi hadi sasa waliosoma kwa kukariri, na hawawezi kutatua matatizo kwa kutumia fikra zao. Sio ivo tu, bali kwa kuwa hawana tabia ya kusoma vitabu na kufikiri kwa undani, wanaamua kufanya vitu vingene tofauti na walivovisoma.

Lakini tukumbuke pia kuwa, njia yenye ,kuhusisha mtu kusoma vitabu ndio njia yenye mwanga Zaidi.

Tukirudi kwenye shule za intenational zenye mtaala wenye kila sifa ya kumjenga mwanao. Hapa ni mahali pazuri sana pa kujiongeza kama unataka kufungua shule yenye mafanikio ya kweli. Na shule yenye wanafunzi ambao watakurudishia matokeo mazuri. Pia wenye weledi, wa kuweza ata kukutibu au kukusaidia kwa Imani nzuri Zaidi.

Haya apa masomo wanayofundishwa wanafunzi wa shule za msingi za international: (Ukifika kwenye hii link click, mahali pameandikwa (what will my child learn))
Na pia unaweza ukaendelea kuangalia masomo ya secondary na sith form wanayofundishwa wanafunzi wa international. kwenye menu ilioandikwa learning.

Ila pia ningependa kutilia msisitizo kwa wale wanaotafuta shule nzuri za secondary, zenye kumjenga mwanao kwenye maadili ya kuja kuwa daktari wa kuaminika au mtu mwenye elimu nzuri hapo baadae.

Kuwa shule kama izi zipo, na wanafunzi wake wanatoka na sifa zote kama wanafunzi wa international.

Na hapa tunaongelea shule kama RENEA, iliyopo Arusha. Shule ina malazi na maktaba nzuri, Pia ina walimu wenye uzoefu, waliotayari kumfundisha mwanao kubobea kwenye taaluma yake, vizuri na kufaulu kwa Imani thabiti.

Ukimfikisha mwanafunzi wako hapa, Hakika atasoma kweli. Piga simu 0756 43 10 32 kama upo tayari kumleta mwanao. Na usisite kuwapa taarifa na wengine maana mwanao akipata elimu bora na ndio Taifa nalo linapona.



View: https://www.youtube.com/watch?v=MlLBPekiMM4&t
 
Back
Top Bottom