Haya ndio Maoni ya Rais JK kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya

Nina Mawili kuhusu JK

1. Nasubiri atangaze kusimama kwa muda kwa mchakato wa katiba ya Muungano na atangaze kuanza kwa mchakato mpya wa katiba ya Tanganyika kwanza ili tukishapata katiba ya Tanganyika ndipo tuje tuendelee na mchakato wa hii katiba ya Muungano.

2. Naanza kuhisi kuwa Prof. Lipumba was right kuwa JK ataongezewa muda wa kukaa madarakani na hataondoka 2015 sababu lazima mchakao uchukue muda mrefu kuliko ilivyodhaniwa. Mchakato wa katiba ya Tanganyika haujaanza na haijulikani utaanza lini ukizingatia kuwa lazima tujue namna gani tutakuwa na Bunge la Bara, Rais wa Bara, Mfumo wa mahakama wa bara na mengineyo mengi.

Just thinking aloud!
Lipumba alishachungulia jikoni na pale kasema ili kupunguza munkari wakati ukifika... yaweza kuwa kaambiwa akaseme ili kutengeneza njia... anaendelea kumsaidia jk
 
kwa hali ilivyo,uchaguzi kufanyika 2015 ni ngumu sana maana mchakato wa kuipata katiba ya bara haujaanza kabisa na haijulikani utaanza lini... jk endelea mpaka 2017... teh teh
 
Kuna siku usipokuwa na yale magwanda yako unakuwa na akili sana. JK hadi 2017

Mchakato wa katiba hauja suspend katiba ya sasa vinaenda sambamba, uchaguzi wa 2015 utafanyika kwa mujibu wa katiba ya zamani, na mchakato wa katiba ya tanganyika utaendelea, kwahiyo ninachokiona ni kwamba kazi ya warioba bado inaendelea! Kikwete akitaka kubaki itatokana na waga wa uchaguzi walionao na hofu ya kupoteza madaraka na hiki kitendo kitakuwa ni very undemocratic na kisichokubalika..
 
Mkuu bibikuku hapa vovyote iwavyo, JK ni Rais hadi 2016 and above ikiwezekana maana mchakato wa katiba ya Tanganyika ukitangazwa lazima ituchukue walau miaka miwili hivi na hadi sasa haijulikani mchakato ukaanza lini.

Hatuwezi kupitisha katiba ya Muungano bila ya kuwa na Tanganyika au Tanzania Bara kama alivyoiita Warioba et al. Kwahiyo lazima mchakato huu ufikie hatua usimamishwe kwa muda na mchakato mwingine uanze upya kabisa kutafuta katiba ya Bara. Zenji wanayo sio issue sana kwao ni swala la amendments tu.

Kwa ufupi tusahau kuwa na Katiba mpya ya Muungano 2014 hata kama itatokea miujiza!

Kama wanatupa nafasi ya kupata Tanganyika.... LET THE GUY BE THERE.... itakuwa mwanzo wa mwisho wa ku-uma-uma meno kwenye uhalisia
 
Huwezi kutunga katiba ya Tanganyika bila ya kuwa na katiba ya Muungano kwanza.

Katiba ya Tanganyika lazima izingatie yale yaliyomo kwenye katiba ya Muungano.

Kazi ngumu ilikuwa kukubaliana muundo wa serikali ya Muungano.

Kinachoweza kufanyika ni kwa Tanganyika kukubaliana muundo wa serikali na namna ya kuwapata viongozi. mambo mengine yote yanaweza kutungwa na uongozi mpya utakaochaguliwa 2015.

Nina Mawili kuhusu JK

1. Nasubiri atangaze kusimama kwa muda kwa mchakato wa katiba ya Muungano na atangaze kuanza kwa mchakato mpya wa katiba ya Tanganyika kwanza ili tukishapata katiba ya Tanganyika ndipo tuje tuendelee na mchakato wa hii katiba ya Muungano.

2. Naanza kuhisi kuwa Prof. Lipumba was right kuwa JK ataongezewa muda wa kukaa madarakani na hataondoka 2015 sababu lazima mchakao uchukue muda mrefu kuliko ilivyodhaniwa. Mchakato wa katiba ya Tanganyika haujaanza na haijulikani utaanza lini ukizingatia kuwa lazima tujue namna gani tutakuwa na Bunge la Bara, Rais wa Bara, Mfumo wa mahakama wa bara na mengineyo mengi.

Just thinking aloud!
 
Bado sijaona utaratibu wa kuwapta wakuu wa mikoa/wilaya,mkono wa rais bado ni mrefu kupindukia,unaanzia juu kuzunguka chini kisha unarudi juu,hii ni hatari dhahri,mwenyekiti wa tume HURU ya uchaguzi kuwa appointed na rais/mwenyekiti wa chama ni janga jingine,ngoja tuone awamu hii kama kuna atakayekumbuka kulizungumzia hilo bila kwikwi.

:shock:Hapo penye red tumeambiwa ni utaratibu wa kila nchi.....Hii tunayoindaa ni katiba ya JMT....hayo si miongoni mwa mambo ya muungano. Tutaliona hili ktk katiba ya Tanganyika!!.....When? I don't know.....
 
Mchakato wa katiba hauja suspend katiba ya sasa vinaenda sambamba, uchaguzi wa 2015 utafanyika kwa mujibu wa katiba ya zamani, na mchakato wa katiba ya tanganyika utaendelea, kwahiyo ninachokiona ni kwamba kazi ya warioba bado inaendelea! Kikwete akitaka kubaki itatokana na waga wa uchaguzi walionao na hofu ya kupoteza madaraka na hiki kitendo kitakuwa ni very undemocratic na kisichokubalika..

Kweli kabisa kiongozi
 
Huwezi kutunga katiba ya Tanganyika bila ya kuwa na katiba ya Muungano kwanza.

Katiba ya Tanganyika lazima izingatie yale yaliyomo kwenye katiba ya Muungano.

Kazi ngumu ilikuwa kukubaliana muundo wa serikali ya Muungano.

Kinachoweza kufanyika ni kwa Tanganyika kukubaliana muundo wa serikali na namna ya kuwapata viongozi. mambo mengine yote yanaweza kutungwa na uongozi mpya utakaochaguliwa 2015.

Hivi kipi kinaanza, uwepo wa mataifa mawili ili yaunde muungano ama unaanza muungano kisha mataifa mawili yanajitenga na kuwa kila taifa peke yake?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom