Haya ndio mambo yaliyo tokea Jijini Mbeya Mtoto azaliwa Mahabusu na kuendelea kutunzwa huko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya ndio mambo yaliyo tokea Jijini Mbeya Mtoto azaliwa Mahabusu na kuendelea kutunzwa huko

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Toneradio, Jan 27, 2012.

 1. T

  Toneradio Member

  #1
  Jan 27, 2012
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 65
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ukitaka kushangaa yanayo tokea nchini utachanganikiwa sana:

  Wakati Tanzania ikiwa imeridhia mkataba wa kimataifa wa kutekeleza na kulinda haki za watoto na kusimamia kwa karibu ulinzi wa haki za binadamu, sasa serikali ina kila sababu ya kuangalia haki za watoto walioko gerezani kwa makosa ya wazazi wao.

  Miongoni mwa haki ambazo serikali inapaswa kuchunguza kwa undani na kubainisha kisa kilichosababisha mtoto mdogo wa kike wa miezi sita , Azra Vuyo Jack, ajikute yeye na wazazi wake wakiwa katika mahabusu ya gereza la Ruanda jijini Mbeya wakikabiliwa na tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya.

  Azra ambaye kwa jina la utani, kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Mbeya yetu huko gerezani anaitwa Merryciana au bibi jela jina ambalo limezoeleka zaidi mbali ya jina lake halisi alilopewa na wazazi wake la Azra .
  Mtoto huyo wa kike aliendelea kukua katika tumbo la mama yake akiwa gerezani, hatimaye alizaliwa salama Julai 15 mwaka jana katika hospitali ya wazazi meta.

  Mama yake ni Anastazia Cloete (27) mwenye asili ya kizungu, raia wa Afrika ya kusini
  Cloete alikamatwa mwaka juzi, Novemba katika mpaka wa Tanzania na Zambia , mji mdogo wa Tunduma akiwa mjamzito na kutupwa mahabusu katika gereza hilo hali iliyomfanya aendelee kulea ujauzito wake.

  Uchunguzi wa kina uliendelea kufanywa na madaktari wa hospitali hiyo hadi alipojifungua salama.
  Uchunguzi wa tukio la mtoto huyo hadi sasa umezusha mwendelezo wa harakati za kihabari na wanaharakati wa haki za binadamu kuona umuhimu wa kuondolewa kwa mtoto huyo ambaye kwa muda wote tangu azaliwe amekuwa akitumia maziwa ya kopo na hanyonyeshwi na mama yake mzazi.

  Mmoja wa ya wasamaria wema aliyejitolea kuwahudumia watuhumiwa hao waliyokumbwa na tuhuma za kukutwa na dawa hizo ni Emily Mwaituka ambaye amekuwa akifanya kazi kubwa ili kuhakikisha mtpto anakuwa na afya nzuri kwa kununuliwa makopo mawili ya maziwa kila wiki tangu alipozaliwa julai, mwaka jana.

  Mwaituka anasema amekuwa akinunua kopo moja la maziwa ya unga aina ya SMA 1 ambalo huuzwa sh 26000 na anapaswa kununua makopo mawili ili kuweza kumudu mahitaji ya mtoto huyo wa kike ambaye hanyonyi maziwa ya mama yake mzazi anayesubiri hatima ya kesi inayomkabili akiendelea kuwa mahabusu kwenye gereza la Ruanda jijini Mbeya.

  Uchunguzi uliofanywa na Mbeya yetu umegundua kuwa Cloete aliyekuwa akisoma nchini kwao katika chuo cha Capetech alijifungua mtoto wa kike miezi sita iliyopita baada ya kushikwa uchungu akiwa mahabusu na kukimbizwa hospitali ya wazazi ya meta.

  Cloete ambaye amekuwa akitumia majina mawili kwani alipolazwa katika hospitali hiyo aliandikishwa jina la Anastazia Elizabeth wakati alifikishwa hospitalini hapo kwa uchunguzi akiwa mjamzito Januari 14 mwaka jana na kufunguliwa jarada la matibabu lenye namba 46 – 26 – 83.
  Uchunguzi umebaini kuwa raia huyo wa afrika ya kusini na mumewe , Vuyo Jack ( 31 ) waliokamatwa mpakani hapo, aligundulika kuwa mjamzito alipokuwa mahabusu na kuanza kupatiwa matibabu sahihi yaliyosaidia ujauzito wake kukua vizuri.

  Habari za ndani zinadai kuwa kwa muda wote huo baada ya ujauzito wake kugundulika alikuwa akipatiwa matibabu chini ya uangalizi wa madaktari na alipofikia hatua za mwisho mjadala mzito ulifanywa na jopo la madaktari walioonyesha mashaka kuwa asingeweza kujifungua kwa njia ya kawaida na kutakiwa afanyiwe upasuaji.

  Imeelezwa kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake katika hospitali hiyo Peter Msafiri , alipofanya uchunguzi alibaini kuwa raia huyo hapaswi kufanyiwa upasuaji kwa vile alikuwa na uwezo wa kujifungua bila matatizo.
  Dk Msafiri alipohojiwa anasema Cloete alijifungua salama ingawa walitaka kumfanyia upasuaji lakini alipinga hatua hiyo na kudai kuwa anaweza kujifungua salama kwa njia ya kawaida.

  Baadhi ya wauguzi wa hospitali hiyo ambao hawakutaka majina yao kutajwa walidai kuwa raia huyo wa Afrika ya Kusini alijifungua mtoto wa kike na kwamba mama yake akiwa mahabusu amekataa kumyonyesha kwa madai kuwa hapati mlo wa kutosha unaomuwezesha kutoa maziwa ya kutosha kwa ajili ya mwanae.

  Cloete alilazwa hapo kwa ajili ya uchunguzi , hamnyonyeshi mtoto wake, kweli amejifungua mtoto mzuri wa kike, amesema kuwa hawezi kumnyonyesha na anamlisha maziwa ya kopo akidai kuwa akinyonyesha atakosa nguvu kwa kuwa mahabusu alikowekwa hapati lishe bora anadai muuguzi mmoja.

  Miongoni mwa wanaharakati wa haki za binadamu walioguswa na habari za mtoto huyo kuendelea kukaa mahabusu na mama yake kulimgusa. Mchungaji William Mwamalanga, anasema kuwa kitendo cha mtoto huyo kuishi katika mazingira hayo hakuendani na haki za binadamu ambazo Tanzania imeridhia kwenye umoja wa mataifa.

  Mwamalanga anasema yeye na wanaharakati wenzake wanaandaa mpango maalumu wa kupigania haki ya mtoto huyo na kuhakikisha kuwa anaondolewa mahabusu baada ya kubainika kuwa amekuwa hanyonyeshwi na mama yake mzazi tangu alipozaliwa kwa madai kuwa hawezi kumnyonyesha kutokana na lishe duni anayopata akiwa mahabusu.

  Nakushukuru sana kuzisoma taarifa hizi, tunajiandaa ili kuona njia sahihi inayoweza kutusaidia kumtoa mtoto huyo mahabusu na kuiomba serikali iangalie kwa undani shauri hili kupitia kwa mwendesha mashtaka mkuu wa serikali ili kujua haki na stahili za mtoto huyo mchanga vinginevyo tunakiuka haki za watoto na binadamu ambazo Tanzania imeridhia kuzitekeleza, anasema Mwamalanga.

  Kumbukumbu za tukio hilo tulizonazo zinaonyesha kuwa raia hao wawili wa Afrika ya Kusini, waliokuwa wakiishi mtaa wa 2A Valley Road – Schaapkraal – Capetown walikamatwa na kilo 42 .5 za dawa za kulevya Novemba 18 mwaka juzi katika mpaka wa Tunduma na kufunguliwa – jalada namba TDM/IR/1763/2010.

  Katika tukio hilo ambalo Vuyo na Cloete walinaswa na dawa hizo walizozificha kwenye gari aina ya Nissana Hard body yenye namba za usajili CA – 508 – 656 lililokuwa likimilikiwa na Vuyo Jack waliokuwa wakitokea mkoani Morogoro kuelekea Afrika ya Kusini, Cloete alikuwa akisoma katika chuo cha Capetech.

  Kwa mujibu wa taarifa za ndani ambazo zimethibitishwa na Mkemia Mkuu wa Serikali dawa hizo za kulevya ni paketi 26 za cocaine zenye uzito wa kilo 28.5 paketi tatu za Heroine zenye uzito wa kilo 3.25 na paketi nane aina ya Morphine zenye uzito wa kilo 3.25, madawa hayo yote yanathamani ya zaidi ya sh bilioni 1.2

  KUSOMA SAKATA ZIMA INGIA HAPA MBEYA YETU BLOG

 2. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Halafu mtoto Azra hajui hata hiyo dawa ya kulevya inafananaje, jamani wamtoe huko bwana hana kosa.
   
 3. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Lailaani uongozi mbofu ulioka madarakani!

  Hakuna mwingine wa kubeba lawama hizi ya wanainchi zaidi ya jk & viongozi wake wote wabovu!
   
 4. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Loooh.......
  Hili halikubaliki!!!
   
 5. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  huyo mtoto amewakosea nini?
   
 6. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Mimi sina wakumlaumu at this particular point, kama ikitokea taasis ikataka kumchukua ikanyimwa ndipo nitapaza sauti kukemea kitendo hicho. Naona watu humu JF wanalaan tu kwa keyboard lakini sijaona anayesema kuwa anamtaka amlee.
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Wangefanya mawasiliano na ubalozi wao kuwaomba wakamchukue huyo mtoto sidhani kama watakataliwa kumchukua!!!
   
 8. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  kwani social workers hawapo?huu ndo utata wa serikali yetu.viongozi walitakiwa wamuhangaikie mtoto achukuliwe na hawa jamaa wa social welfare
   
 9. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  sii mara ya kwanza kutokea nendeni segerea mtaona watoto wa wafungwa na mahabusu hata bangwe pale kigoma nlishuhudia mwaka 2008.
  watoto wamahudumiwa vizurin kabisa na kutibiwa na isitoshe magereza ya wanawake ni wasafi na sio wengi kama jela za wanaume
  siteteti watoto kukaa humo ila ndugu wanaruhusiwa kuwachukua kuwalea.
   
Loading...