Haya ndio mambo matatu yanayowasumbua matajiri na wanasayansi waliobobea

Papa Mobimba

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
1,153
1,359
Dunia inakwenda kwa spidi sana. Na wanasayansi kila kukicha wanajaribu kuchochea spidi hiyo. Inawezekana wengine wamestuck karne ya 20, na wengine wako karne ya 21, lakini inawezekana wengine wako karne kadhaa mbele yetu.⁣

Huko duniani kuna vitu vinaitwa AI (ARTIFICIAL INTELLIGENCE) wana sayansi wanataka kujaribu kuunganisha ubongo wako na kompyuta. Wanaamini kwamba wakiweza kuimaster vizuri AI na kuitumia vizuri, italeta suluhu kubwa sana kwenye matatizo yanoyoathiri mfumo wa fahamu.⁣

Tuachane na hilo twende kwenye mambo ambao wanasayansi na dunia wanaangaika nayo kwa sasa. Mambo hayo matatu ni kuwafanya binadamu waishi milele, binadamu kuwa na uwezo wa kimungu na kuhakikisha binadamu wanakuwa na furaha wakati.⁣

Bilget, Bezos, Sundar Pichai, Mark yule jamaa wa Facebook na utajiri wao wote wanaogopa kifo sawasawa na kapuku hoye yae anayekaa Tandale kwa Mtogore. Na wao pia wanaumwa japo magonjwa yao yanaweza kuwa tofauti na ya huyu kapuku wa JF. LAKINI BADO WANAUMWA NA IPO SIKU WANAJUA WATAKUFA.⁣

Matajiri wamewekeza pesa nyingi sana katika tafiti, angalau kuhakikisha hata kama hawatoishi milele. Basi angalau waishi miaka 150. Ni kweli umri wa binadamu umeongezeka sana ukilinganisha na karne iliyopita ambako hakukuwa na chanjo dhidi ya magonjwa, hakukuwa na madawa, vita na ubabe vilitawa. Bado wanasayansi kupitia pesa za matajiri wanataka kuona binadamu anaishi zaidi na zaidi.⁣

Wanasayansi wanataka kujaribu kuumba mtu, kondoo au mbuzi kujizaa hata kama hakuna jike wala dume. Kuna kitu kinaitwa cloning. Wanataka John au Mariam ajizae. Wanataka kujaribu kujua kama Juma atakufa mwaka 2030 na nini kitamuua leo.⁣

Furaha je. Watu wanatafuta pesa wakiamini wakizipata watakuwa na furaha, moyo na akili yao itatulia. Hebu angalia nchi zilizo endelea kiwango cha upweke kilivyo juu. Nchi kama uingereza wameweka waziri kabisa anayehusika na mambo ya upwake. Kama ungejua utamzaa mtoto mwenye akili sana, mrembo akipita dunia inatetemeka lakini siku moja atakuja kujiua kisa kaachwa na bwana.⁣

Wanasayansi wanaangalia ni gene ipi wataibadili kuhakikisha kuwa wanafanikiwa kumfanya mtu kuwa na furaha wakati wote, January mpaka December, asubuhi mpaka asubuhi. Wako maabara wanafanya kazi hiyo⁣

Sina hakika kama watafanikiwa leo ama kesho kabla mimi na wewe hatujafa. Hata tukifa wajukuu zetu watakuja kutisimulia siku tukikutana katika maisha mengine baada ya haya maisha ya hapa duniani.⁣


 
hahahaha wanahangaika nami naombea wasifanikiwe maana sie makapuku tutaendelea kata moto huku wao wakienjoy miaka 200+ .
kifo ndo haki ya kweli
 
Back
Top Bottom