Haya ndio majibu kuhusu hoja ya wanachuo kuhusu haki yao ya kikatiba ya kupiga kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya ndio majibu kuhusu hoja ya wanachuo kuhusu haki yao ya kikatiba ya kupiga kura

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by ALU-MASOLI, Oct 15, 2010.

 1. ALU-MASOLI

  ALU-MASOLI Member

  #1
  Oct 15, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  :argue:
  Wanajamii wenzangu, je haya majibu yanasadifu kile kilichokuwa kikidaiwa na walengwa wa lile lalamiko?
  CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
  UFAFANUZI KUHUSU FURSA KWA WANAFUNZI KUPIGA
  KURA CHUONI WAKATI WA LIKIZO


  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinapenda kufafanua kwamba, ingawa tangu tarehe 24 Julai mwaka huu wanachuo walio wengi wamekuwa mapumzikoni, hakuna kampasi
  yoyotote ya Chuo Kikuu iliyofungwa. Shughuli zote muhimu za Chuo, zikiwemo
  ufundishaji wa makundi kadhaa ya wanafunzi wa shahada za kwanza, utafiti, huduma
  za maktaba, utoaji wa ushauri wa kitaaluma na shughuli mbalimbali zinazohusiana na
  mafunzo ya uzamili na uzamivu zimekuwa zikiendelea muda wote. Kwa kifupi, Chuo
  kimeendelea kutoa huduma kwa wadau wake wote.

  Kwa hiyo ni wazi kwamba siku ya uchaguzi, yaani tarehe 31 Oktoba 2010, vituo vya
  kupigia kura vilivyopo ndani ya kampasi za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam vitawapokea
  na kuwahudumia watu wote wenye stahili ya kupiga kura hapo bila usumbufu wowote.
  Watakaohudumiwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na Tume ya Uchaguzi ni
  pamoja na wanafunzi, wafanyakazi waliojiandikisha Chuoni na wananchi kutoka
  maeneo yanayozunguka kampasi za Chuo.

  IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
  CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
  13 Oktoba, 2010
   
 2. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Haijakaa sawa, inamaana wanafunzi wa chuo watoke mikoani kuja kupiga kura dar?
  Halafu warudi makwao wangoje chuo kufunguliwa? Au sijayaelewa hayo majibu!
   
 3. ALU-MASOLI

  ALU-MASOLI Member

  #3
  Oct 15, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ndio wanavyomaanisha mkuu....
  hapo hawajajibu kabisa hoja ya msingi. la zaidi ni siasa tu.
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nguvu ya umma wataingia line wenyewe ngoja tupaje msemaji mmoja mdhungu utasikia CCM na TUME wanafanya mambo
   
 5. ALU-MASOLI

  ALU-MASOLI Member

  #5
  Oct 15, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  UDSM yathibitisha vituo vya kura
  Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 14th October 2010 @ 22:55 Imesomwa na watu: 149; Jumla ya maoni: 1


  CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimesema siku ya uchaguzi Oktoba 31, mwaka huu vituo vyote vya uchaguzi vilivyomo ndani ya kampasi za chuo hicho vitakuwa wazi na vitawapokea wale wote wanaostahili kupiga kura hapo bila usumbufu wowote.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chuo hicho, Dar es Salaam, jana watakaohudumiwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni wanafunzi na wafanyakazi waliojiandikisha na wananchi kutoka maeneo yanayozunguka kampasi
  hizo.

  Juzi katika mkutano wa wadau wa amani Mkurugenzi wa NEC, Rajabu Kiravu alifafanua juu ya wasiwasi uliokuwapo wa wanafunzi wa vyuo ambao wako mapumzikoni kushindwa kupiga kura kutokana na wengi wao kujiandikisha katika vituo vilivyopo katika kampasi za
  vyuo wanavyosomea.

  Alisema hakuna ushahidi wowote unaonyesha kuwa wanafunzi wote wamejiandikisha vyuoni kutokana na tume hiyo kutoa muda tofauti katika vipindi vitatu tofauti kwa wananchi kuweza kubadili vituo kulingana na eneo watakalokuwapo wakati wa kupiga kura.

  Alisema daftari halitafunguliwa tena. Naye Namsembaeli Mduma anaripoti kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, wameendelea kuitaka Serikali kuamuru kufunguliwa kwa vyuo vyote nchini kabla ya Oktoba 29, ili kuifanya Tanzania kuwa nchi inayoheshimu katiba na demokrasia kwa vitendo.

  Rais na Mwenyekiti wa Taarifa kwa Umma wa Chama cha Haki za Binadamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mhapa Peter alisema juzi wakati wa mjadala kuhusu uvunjwaji wa haki hiyo ya kupiga kura kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kuwa kutotatuliwa kwa tatizo hilo
  kutaiondolea Tanzania sifa ya kuwa na demokrasia ya kweli na heshima ya haki za raia wake.
  Source:
  http://www.habarileo.co.tz
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Oct 15, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,467
  Likes Received: 4,126
  Trophy Points: 280
  Hawa vipi waliopo mikoani sasa inakuwaje?
   
 7. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2010
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Waende kwenye vituo vyao,, si wapo wengine walijiandikisha huko mikoani na sasa wapo Dar,, nao pia wanao uhuru wa kwenda huko ili kutumia haki yao ya KIDEMOKRASIA
   
 8. emmathy

  emmathy Senior Member

  #8
  Oct 15, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hawa jamaa wanachekesha sana kwani hata bila tangazo nathani watu wenye uwezo kufika chuoni wangeenda kudai haki yao ya msingi.Point ni jinsi gani watu wa mkoani watafika na kupiga kuraaa............ni afadhali kawma chuo kingekuwa kimefunguliwa watu wangeunga ila watoto wa wakulima watafikaje huko wakati hata ada zenyewe ni shida kuzipata? Bado hawajatoa majibu dhidi ya haki za wanachuo kupiga kura
   
 9. ALU-MASOLI

  ALU-MASOLI Member

  #9
  Oct 15, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mkuu ishu ni kwa wale walioko mikoani ambao walijiandikisha pale chuo jijini DSM inakuwaje? hao ambao wako mikoani na walishajiandikisha huko wataitumia haki yao huko huko. Tulichokuwa tunasubiri jibu la serikali ni hawa ambao wako mikoani na walijiandikisha chuo. Na bad enough ni wengi na ni wapiga kura potential.
   
 10. M

  MJM JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Hivi hawa ndiyo wasomi wa nchi hii? Wangejaribu kuficha upumbavu wao kwa kukaa kimya. Njaa zetu zitatufikisha pabaya
   
Loading...