Haya ndio maisha ya mabeberu ambao kila uchao huwaza kujilimbikizia utajiri wa madini nchini kwao

Mbase1970

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
6,054
4,601
BULLIONISM, IMPERIALISM na NEOCOLONIALISM.

Bullionism is an economic theory that defines wealth by the amount of precious metals owned. Bullionism is an early or primitive form of mercantilism. It was derived, in the 16th century, from the observation that the English state possessed large amounts of gold and silver (bullion). Despite the fact that there was no mining of precious metals in England, because of its large trade surplus.

Imperialism is a state policy, practice, or advocacy of extending power and dominion, especially by direct territorial acquisition or by gaining political and economic control of other areas. Colonialism was a form of imperialism.

Neo-Colonialism is the control of less-developed countries by developed countries through indirect means. It is continuing dependence of former colonies on foreign countries, its where the power of developed countries used to produce a colonial-like exploitation.

Haya ndio maisha ya mabeberu wanyonyaji ambao kila uchao huwaza kujilimbikizia utajiri mkubwa wa madini nchini kwao.

Haya matofali ya dhahabu yametoka kwetu Afrika na nchini kwetu Tanzania tangu hawa mabeberu walipokaa na kukubaliana kuligawana bara la Afrika ili wavune utajiri mkubwa tuliobarikiwa na Mwenyezi Mungu mtukufu katika ardhi yetu ya Afrika.

Ajabu na kweli tangu hawa mabeberu walipoanza kuyatwaa madini yetu chini ya mwamvuli wa Ukoloni na baadae Ukoloni Mamboleo kupitia sera za uwekezaji, sisi hatujawahi kupata maendeleo yoyote ya kujivunia, nchi zetu zimeendelea kuwa fukara wa kutupa.

Sheria na mikataba ya madini ndio silaha inayotumika kutuangamiza kwa kututoa sadaka mbele ya makucha ya mabeberu.

Imeelezwa kuwa miaka ya mwanzoni ya 1990's mabeberu kwa kutumia taasisi zao za kifedha (WB na IMF) walitengeneza sera za kiuchumi na kifedha ambazo kwa jicho la nje ni kana kwamba zililenga kutusaidia nchi za Ulimwengu wa tatu lakini nyuma ya pazia sera hizo zilikuwa zinachonga njia ya kuusimika vilivyo Ukoloni Mamboleo kwa kutega mirija ya unyonyaji na uhamishaji wa rasilimali na utajiri wa Afrika kupeleka huko kwenye mataifa ya mabeberu.

Tunaelezwa kuwa baina ya 1994 na 1997 mawakala wa mabeberu walifanya ziara hapa nchini mara 17 wakijitanabahisha wanahangaika kutusaidia ili kujikwamua kutoka kwenye lindi la umasikini na tuanze kufurahia matunda ya utajiri wa rasilimali zetu kumbe huu ulikuwa ni mtego.

Matokeo ya harakati hizo yalipelekea tukapata Sera ya Madini ya mwaka 1997 ambayo nayo ikapelekea kupata sheria ya madini ya mwaka 1998 inayotajwa kuwa ni copy n'paste kutoka sheria ya madini ya Zambia ambayo nayo ilisimikwa na mawakala hao hao wa nchi za mabeberu. Leo zinatukaba koo.

Sera mbalimbali za kiuchumi na kifedha, mikataba na sheria zimekuwa zikipitishwa kwa mashinikizo ya mataifa ya mabeberu na kusimamiwa na mawakala wao. Lengo msingi likibaki kwenye dhana yao ya Kujilimbikizia utajiri wa maliasili (bullionism) kupitia Ukoloni Mamboleo (Neo-Colonialism) ambao huu ni mbaya zaidi ya Ukoloni halisi.

Leo hii tumejikuta tumenasa kwenye tope zito sio Tanzania, sio Zambia, sio Ghana, sio Cote d'voire, sio Botswana, sio Liberia, sio DRCongo wala Afrika Kusini kote tumeshikwa tunanyonywa tunaibiwa. Na tunajua kuwa tunaibiwa na tunawajua wanaotuibia. Na wamejizatiti sana Kisheria kwa kuwa wanajua wanachofanya. Tunafanyaje?

Rais wetu amethubutu, ameamua kutoboa pandora box ni dhahiri manyigu watatoka watasambaa na watajitahidi kumng'ata kila mtu. Amavubhi ni hatari lazima tupambane nao. Hakuna namna wala woga ila tuwakabili Amavubhi hawa mpaka tuwashinde kwa gharama yoyote. Kila silaha itumike ili tushinde vita hii.

"Bara langu Afrika, ulipewa jina baya
Wakajitapa wasomi, ukaitwa giza nene
Wakaja na misahafu, nchi wakazikalia
Mpaka tone la mwisho, damu yangu ukombozi"

Iwe tumeanza vizuri ama vibaya lazima tuwakabili manyigu na tuwashinde.

Afrika ni yetu! Aluta Continua!






Hii makala imeandikwa na Said Msonga katika Facebook page yake.

Ni mwana ACT-Mageuzi
 
Back
Top Bottom