Haya ndio mafanikio ya CHADEMA toka 1992. What a shame!?

MIAKA 52 YA UHURU WA TANGANYIKA, CCM IMESHIKA DOLA, SO FAR NINI CHA MAANA WALICHOFANYA??? ZAIDI YA KUUA VIWANDA, VIONGOZI WAKE KUENDELEA KUJILIMBIKIZIA MALI HUKU WATANZANIA WALIO WENGI WAKIISHI MAISHA YA UMASIKINI WA HALI YA JUU ( TANZANIA IS THE POOREST COUNTRY IN THE WORLD ), DENI LA TAIFA LIKIENDELEA KUKUA KWA KASI MPYA NA ARI MPYA, ELIMU IKIZIDI KUPOROMOKA KWA KIASI KIKUBWA, VYOMBO VYA HABARI VIKIZIDI KUKANDAMIZWA NA WATAWALA ( KUFUNGIWA KWA MWANAHALISI ), WIZI WA KURA KATIKA CHAGUZI MBALIMBALI , WAKULIMA WAKIENDELEA KUKOPWA NA SERIKALI, MALIMBIKIZO YA MISHAHARA YA WAALIMU, MAISHA MABOVU YA WALINZI WA NCHI ( KOTA ZA POLISI OYSTERBAY, DODOMA POLISI LINE ni mifano hai ), GAP KATI YA WALIONACHO NA WASIONACHO LIKIZIDI KUONGEZEKA, ARDHI IKIPORWA KWA KASI NA WAWEKEZAJI WA KIGENI ( MFANO HALISI ARUMERU MASHARIKI, LOLIONDO ), UTOROSHWAJI WA WANYAMAPORI KWENDA NJE YA NCHI ( TWIGA WALIOP[ITISHWA KIA KUELEKEA UARABUNI na huu mtindo ulianza kuanzia enzi za utawala wa mwinyi ), BAJETI YA NCHI KUWA TEGEMEZI KWA ZAIDI YA ASILIMIA HAMSINI, MFUMUKO WA BEI KILA KUKICHA, UCHUMI KUKUA KWENYE MAANDISHI NA MAKABRASHA LAKINI WANANCHI TUKIWA NA MSOTO MKALI, MATUMIZI MAKUBWA YA SERIKALI KULIKO MAPATO, IKULU KUGEUKA KUWA PANGO LA WANYANG'ANYI ( WAFANYABIASHARA WANAINGIA IKULU KAMA RUTI ZA FAST JET : 3 TIMES A DAY BOTH WAYS ), UTENGENEZAJI WA MIRADI MINGI YA KIFISADI NA KUNUFAISHA WACHACHE ( RICHMOND ), UKWAPUAJI WA FEDH BENKI KUU ( EPA ), MIKATABA YA KIFISADI KATIKA RASILIMALI ZA NCHI ( MIKATABA KWENYE SEKTA YA MADINI, GESI ), UONGOZI WA KISASI KATI YA WATAWALA NA WATAWALIWA INAYOSABABISHA WATU KUBAMBIKIZIWA KESI ( BABU SYA, PAPII KOCHA ), SIASA KAMA VITA ( MABOMU YA ARUSHA ), VITENDO VYA KIGAIDI NA KINYAMA VIKISHIKA KASI DHIDI YA WAPIGANIA HAKI ( KUNG'OLEWA KUCHA , MENO vitendo walivyofanyiwa DR. ULIMBOKA NA KIBANDA ), SIASA IKITAWALA MPAKA KWENYE MAMBO YA MSINGI KAMA ELIMU ( DIVISION 5, KU STANDARDIZE MATOKEO YA KIDATO CHA NNE ), WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WAKIISHI MAISHA MABOVU YASIYOKUWA NA MAADILI KWA KUKOSA MKOPO ( HASA WAFUNZI WA KIKE WANAVYOJIUUZA KATIKA KUMBI ZA STAREHE), WATOTO WA VIGOGO WAKIUZA DRUGS BILA YA KUKAMATWA, YATIMA WAKIAMBUKIZWA UKIMWI NA VIONGOZI WA KISIASA ( PROF. KAPUYA DRAMA ), TO MENTION FEW,,,,,,,e.t.c

Umeandika mambo mengi lakini ume base kwenye mahisia zaidi na kuacha kabisa uhalisia wa mambo. Mfano suala la Kapuya tayari kwamba limeonekana ni uzushi, suala la vigogo kuwa matajiri sidhani kama ni hoja kwa kuwa utajiri sio laana na kama kuna kigogo amekuwa tajiri kinyume na utaratibu mtaje jina na huje na ushahidi. Hayo mengine yote ni uzushi na kukosa kwako shukrani kwa kazi nzuri inayofanywa na serikali.
 
WanaJF,

Tokea CDM ianzishwe mnamo mwaka 1992, sasa yapata miaka ipatayo 23.
.....

FaizaFoxy hebu mfundishe huyu dogo jinsi ya kukokotoa hesabu.
Tangu mwaka 1992 hadi leo (2013) ni miaka 23...???
Sijui hapa mtoa hoja anakata wasomaji wapate Taswira gani ya uwezo wake wa mahesabu..??
 
Last edited by a moderator:
Mbona hizo success hazipimiki? Jaribu kuongeA kama msomi. Do you know Chadema's set goals? je walilenga ku-achieve nini na lini? Then from there ndio unasema wamefanikiwa au lah. But out of that utakua unaongea hadithi za Abunuasi

Wewe jamaa upo bongo kweli?! Maana hakuna asiyejua kuwa goal kubwa ya CDM ni kuivuruga amani ya nchi na kukwamisha maendeleo. Kama kuna goals zingine basi ni kama cover tu ya hiyo main goal.
 
FaizaFoxy hebu mfundishe huyu dogo jinsi ya kukokotoa hesabu.
Tangu mwaka 1992 hadi leo (2013) ni miaka 23...???
Sijui hapa mtoa hoja anakata wasomaji wapate Taswira gani ya uwezo wake wa mahesabu..??

Hiyo ni minor error tu na usiifanye kuwa ajenda kuu kwenye huu uzi. Hoja kuu hapa ni kujadili mafanikio ya CDM na malengo ya kuanzishwa kwa chama. Je, yamefikiwa?
 
Last edited by a moderator:
Hiyo ni minor error tu na usiifanye kuwa ajenda kuu kwenye huu uzi. Hoja kuu hapa ni kujadili mafanikio ya CDM na malengo ya kuanzishwa kwa chama. Je, yamefikiwa?

Kama hata wewe ambaye umesoma, lakini hata hesabu ndogo ya kutoa inakushinda, hebu fikiria mamilioni ya watanzania ambao wako vijijini wakiteseka kwa umaskini wana hali gani.
Hesabu hujui, sasa mafanikio gani unayataka ...??
Jinsi uluvyovurugwa na hali mbaya ya maisha chini ya CCM, mpaka hesabu ndogo ya kutoa inakushinda....!!!
Chadema inalenga kuwakomboa watanzania kama wewe na mimi kutoka kwenye makucha ya wanyonyaji wa mali za watanzania, ili hata wewe uweze kuwa na amani ya kutosha kuweza kupiga hesabu ndogo vizuri...!!
Upo hapo...????
 
Wewe jamaa upo bongo kweli?! Maana hakuna asiyejua kuwa goal kubwa ya CDM ni kuivuruga amani ya nchi na kukwamisha maendeleo. Kama kuna goals zingine basi ni kama cover tu ya hiyo main goal.

Hapo kwenye blue,

Tanzania ni moja ya nchi tajiri sana barani Afrika.
Lakini wananchi wake ni maskini sana, na hawana maendeleo kabisa.
Tangu Tanzania ipate uhuru, imepita miaka 52 sasa...!! Na bado hakuna maendeleo yoyote yale kulinganisha na utajiri uliopo..!!
Sasa wewe kama kweli unafikiria vizuri, hebu angalia kama Chadema imekwamisha maendeleo yako kwa miaka 52 sasa..!!
Piga hesabu (ingawa hujui hesabu...!!)
Tangu uhuru ni miaka 52... na Chadema tangu ianzishwe ni miaka...???????
Nani kakwamisha maendeleo...???
 
Hiyo ni minor error tu na usiifanye kuwa ajenda kuu kwenye huu uzi. Hoja kuu hapa ni kujadili mafanikio ya CDM na malengo ya kuanzishwa kwa chama. Je, yamefikiwa?

CCM ina mafanikio yapi tangu kuanzishwa mfumo wa Vyama vingi?
( Mafanikio toka uanzishwe mfumo wa Vyama Vingi)
Weka hapa!!
 
Hapo kwenye blue,

Tanzania ni moja ya nchi tajiri sana barani Afrika.
Lakini wananchi wake ni maskini sana, na hawana maendeleo kabisa.
Tangu Tanzania ipate uhuru, imepita miaka 52 sasa...!! Na bado hakuna maendeleo yoyote yale kulinganisha na utajiri uliopo..!!
Sasa wewe kama kweli unafikiria vizuri, hebu angalia kama Chadema imekwamisha maendeleo yako kwa miaka 52 sasa..!!
Piga hesabu (ingawa hujui hesabu...!!)
Tangu uhuru ni miaka 52... na Chadema tangu ianzishwe ni miaka...???????
Nani kakwamisha maendeleo...???

Maendeleo hayatokei over night wewe acha kuwaza kwa kutumia akili zako za darasa la tatu. Unadhani Tanzania ilipaswa kuwa tajiri baada tu ya kupata uhuru?! Au miaka 20 baada tu ya uhuru?! Mambo hayapo hivyo. Nchi inaendelea ila muda nao una nafasi yake vile vile. Hivyo kama CDM wakitupunguzia fujo na kuifanya serikali isitenge fungu kubwa la pesa kwenye wizara ya mambo ya ndani, definately nchi itasonga mbele kwa kasi zaidi.
 
Nimekuja Moshi ni aibu wakuu. Mji umerudi nyuma, hakuna kipya kwa kifupi pamechoka. Nimeuliza nikaambiwa tatizo ni NDESAMBURO na madiwani wa CHADEMA.
 
WanaJF,

Tokea CDM ianzishwe mnamo mwaka 1992, sasa yapata miaka ipatayo 21.

Lakini katika kipindi chote hiki cha uwepo wa chama hicho katika uwanja wa siasa za ushindani, bado tija ya CDM haijaonekana kabisa, zaidi zaidi ni mambo ya ajabu ajabu tu ndio ambayo yamekuwa yakifanywa na chama hicho ambayo kimsingi mambo hayo ndio huitwa MAFANIKIO YA CDM. Baadhi ya MAFANIKIO ya CDM tangu kuanzishwa kwake ni:

i) Kuchochea mgawanyiko wa kikabila na kikanda nchini. Hapa wamefanikiwa ingawa sio kwa kiasi kikubwa kutokana na kudhibitiwa na serikali ya CCM.

ii) Kushushwa kwa hadhi kwa jiji la Arusha na kupelekea kupungua kwa idadi kubwa ya watalii na kushuka kwa mapato ya jiji hilo. Hapa pameratibiwa na Lema.

iii) Kuhamasisha vijana watumie mihadarati kama vile bangi, gomba, milungi, kuberi na viroba. Hapa wamefanikiwa sana hasa kwa vijana wa Arusha na Mbeya.

iv) Kuwekeza kwenye matusi na fujo. Hapa CDM imefanikiwa mno hasa ukizingatia chama kimemkabidhi hii sekta mtu aina ya Sugu (mb) ili kuweza kuiratibu. Katika historia ya nchi yetu, ni kwa mara ya kwanza tumeshuhudia ngumi kupigwa bungeni pamoja na kutukanwa kwa viongozi wa kitaifa.

v) Kutoa kafara Watanzania kwa kisingizio cha haki ya maandamano na mikusanyiko. Wote tunajua kuwa Mbowe ni mfanyabiashara na miaka ya hivi karibuni baada ya kumwaga damu ya kutosha ya Watanzania biashara yake imeonekana kustawi. Unaweza ku-connect dots hapo.

Haya ni baadhi tu ya mafanikio ya CDM ila ni imani yangu yapo mengine mengi ambayo yamefanywa na chama hicho cha kifamilia. Hivyo kuwa huru kujazia jazia mafanikio unayo yafahamu ya hiki chama

Ile issue ya Prof Kapuya ccm wameizima!
 
ungu wan

Eeeh! Mungu, pokea sifa baba maana humpa kila mtu sawa swa na matendo yake!. CCM walianzisha udini kwa CUF, wakahamia CDM, wakaongeza ukabila, ukanda. Na sasa Mungu mkuu, umeanza kuwapa matunda ya kazi yao!. Sina wasi wasi na kazi yako!. Naamini kama ulivomuumbua Ole medeye jana bungeni, Hammy-D naye utampa haki yake kwa kazi anayofanya katika post zake hapa jukwaani!. Amina!!
 
Wewe yawezekana kabisa huijui historia ya hii nchi na ndio maana ina kupelekea kuandika andika vitu vyepesi ukidhani humu JF watu wana upeo kama wako hivyo watakubaliana na hoja ulizoweka. Ngoja nikukumbushe, kwanza kabisa suala la katiba mpya fukuto lake lilianza ndani ya CCM, pili masuala ya kupambana na ufisadi huko zamani yalikuwa yakiitwa kupambana na wahujumu uchumi hivyo sio vitu vigeni na wala havijaanzishwa na CDM.

Ubongowa kuku uko parabola, hivyo kuku husahau baada ya kama dakika tu. Ndiyo maana ukimfukuza baada ya muda anarudi tena na kufanya kilekile ulichomfukuzia. Kuku hufanya vituvyake kwa mazoea tu na siyo akili. I have therefore came to conclude that Team Lumumba you are like chickens!!
 
Umenirahisishia kazi ya kutambua upeo wako ni wa kiasi gani hasa kwa ID name uliyoitumia. Nadhani wasomaji wataweza ku-connect dots kati ya ID name yako na pumba ilizoandika kwenye bandiko lako.
 
Umenirahisishia kazi ya kutambua upeo wako ni wa kiasi gani hasa kwa ID name uliyoitumia. Nadhani wasomaji wataweza ku-connect dots kati ya ID name yako na pumba ilizoandika kwenye bandiko lako.
Tuko Kisesa msibani, kada mwenzetu aliuwawa na wananchi wake kwa kuwapora ardhi, ubani wako ni muhimu sana , mengine baada ya msiba.....
 
Nimekuja Moshi ni aibu wakuu. Mji umerudi nyuma, hakuna kipya kwa kifupi pamechoka. Nimeuliza nikaambiwa tatizo ni NDESAMBURO na madiwani wa CHADEMA.

Wewe inzi wa kijani ndo maana umekosa pa kueneza kipindupindu.
 
Hiyo ni minor error tu na usiifanye kuwa ajenda kuu kwenye huu uzi. Hoja kuu hapa ni kujadili mafanikio ya CDM na malengo ya kuanzishwa kwa chama. Je, yamefikiwa?

Unajadili mafanikio yao ili iweje wakati si chama tawala? Mr Inzi wa Kijani.
 
Na haya ni baadhi ya mafanikio ya CCM;

1. Kuua viwanda na kuwafanya vijana wakose ajira kwa kiwango kikubwa.
2. Kuongeza kiwango cha wanafunzi kufeli na kuanzisha division five,
3. Kuhimiza ujangili na kupunguza idadi ya tembo kwa kumuwezesha katibu wa chama kuwa na kampuni inayosafirisha meno ya tembo nje ya nchi,
4. Kuwapiga mabomu wazee wa Afrika Mashariki wanapodai mafao yao,
5. Kuwalinda mafisadi na kuendekeza siasa uchwara kama alivyonukuliwa Rostam Aziz mwaka 2011,
6. Chama kushamiri kwa biashara ya madawa ya kulevya,
7. Kushindwa kuyafikia malengo ya millenia mfano kupunguza vifo vya mama na watoto,
8. Kuingilia uhuru wa vyombo vya habari na kuwaua waandishi,
9. Kushusha hadhi ya Tanzania katika jumuiya ya Afrika Mashariki
10. Chama chetu (CCM) kimefanikiwa katika kusimamia biashara ya kimataifa kwa kubadilishana vyandarua na dhahabu...CCM hoyeee!

Dah!!! Yaani ulivyo yapangilia vizuri mafanikio, mpaka inavutia ndg yangu....nakupa Division Five
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom