Haya ndio madhara ya ufisadi, Tanzania yanyimwa mamillion

tamimusalim

JF-Expert Member
Jun 17, 2014
1,827
1,225
Rais wa Marekani Barack Obama akiwa katika ziara yake nchini Kenya, leo alifungua kongamano la ujasiriamali.

Ametangaza nchi 3 ambazo zitanufaika kabisa na mamilioni ya dola atakayotoa kuwasaidia wajasiriamali hasa wanawake na vijana.

Amezitaja nchi hizo ni Kenya,Mali na zambia.

Kwa mujibu wa wapekuzi wetu Tanzania ilikuwa moja ya nchi ambazo ingenufaika na pesa hizo, badala yake Mali ikachukua nafasi hiyo.
 
Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,030
2,000
Yaani zingekuja tz wangegawana hapo hapo magogoni kama zile mabilion ya jk
Acha wafaidi wengine
 
Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,408
2,000
Toka JK ameingia madarakani zimekuja hela nyingi sana kutoka nchi mbalimbali lakini anaondoka na kuacha deni la taifa trilioni 40 huku maisha yakiwa magumu kuliko alivyoyakuta.

Ujumbe ni kwamba misaada haimalizi umaskini, rasilimali tulizonazo zinatosha kutufanya matajiri, tunahitaji serikali responsible na sera nzuri, hatuhitaji wazungu
 
chegreyson

JF-Expert Member
Nov 23, 2011
925
500
africa ina nchi 52 rais obama amezitaja nchi tatu tu mtomada unataka kutuaminisha kwamba nchi zote zilizobaki ni fisadi?
acha kuwa na mawazo hasi kila wakati .nimeingalia na kusikiliza hotuba ya obama hakuna sehemu aliyosema kwamba tanzania ilikuwa katika program ile ,ila kwamba ajili ya ufisadi wamepeleka mali ,ukiwa na akili kidogo tu utagundua kuwa mali imewasilisha west africa,zambia southern africa kenya imewasilisha east africa
 
aliisaac1000

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
382
250
Acha ujinga , tanzania teyari inanufaika na awamu ya pili ya millenium challenge inayotoka marekani na nchi zilizochaguliwa zimelengwa kwa ukanda wa east. South na west africa
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
86,268
2,000
Toka JK ameingia madarakani zimekuja hela nyingi sana kutoka nchi mbalimbali lakini anaondoka na kuacha deni la taifa trilioni 40 huku maisha yakiwa magumu kuliko alivyoyakuta.

Ujumbe ni kwamba misaada haimalizi umaskini, rasilimali tulizonazo zinatosha kutufanya matajiri, tunahitaji serikali responsible na sera nzuri, hatuhitaji wazungu
Tatizo viongozi waliokuwepo kwenye madaraka wao kazi yao ni kumeza tu
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
86,268
2,000
Tanzania tumefikia hatua mbaya sana ya ufisadi huku viongozi wake wakiwa hawana hata aibu.
 
Hawkins

Member
May 23, 2015
58
70
Rais wa Marekani Barack Obama akiwa katika ziara yake nchini Kenya, leo alifungua kongamano la ujasiriamali.

Ametangaza nchi 3 ambazo zitanufaika kabisa na mamilioni ya dola atakayotoa kuwasaidia wajasiriamali hasa wanawake na vijana.

Amezitaja nchi hizo ni Kenya,Mali na zambia.

Kwa mujibu wa wapekuzi wetu Tanzania ilikuwa moja ya nchi ambazo ingenufaika na pesa hizo, badala yake Mali ikachukua nafasi hiyo.
Tanzania haikuwa moja kati ya hizo nchi sababu ni nchi tajiri iliyobarikiwa kuwa na utajiri kuliko nchi Nyingi sana, lakini ikakosa uongozi bora hivyo hata ingepata hizo dola zingeishia mifukoni. Pia usizoee misaada kwan ina gharama zake
 
Hawkins

Member
May 23, 2015
58
70
Unajua gharama ya hiyo misaada? Tatizo wa tz tunapenda sana misaada, muda ukifika wa mikataba isiyoeleweka ikiwa ni gharama ya hiyo misaada mnaanza kulialia hovyo.
 
Top Bottom