Freyzem
JF-Expert Member
- Jun 29, 2013
- 10,049
- 24,428
Baada ya lile tukio baya kabisa lililompata mbunge, T. Lissu la sept 7, 2017 na kukimbizwa Nairobi kwa matibabu yaliyookoa uhai wake na hatimae Ubelgiji, basi kumekuwa na sintofahamu juu ya stahiki zake alizopaswa kulipwa na bunge!
...Stahiki alizotakiwa kulipwa ni posho ya siku ya kwake yeye binafsi, pamoja na 20% ya posho yake kwa msaidizi mmoja ambapo gharama hizi ni nje ya gharama za matibabu!
..Kwa mujibu wa sheria Lissu alipaswa kulipwa posho takribani dola 450 kwa siku pamoja na dola 90 za msaidizi wake( ambaye ni mkewe) kwa siku na kufanya jumla ya dola 540 kwa siku!
..Hivyo, basi hadi hivi sasa ambapo ni takribani miezi 17 imeisha tokea aumizwe, ni kuwa anapaswa kulipwa si chini ya dola 275,000.
Ikumbukwe pia kiwango hiki kinazidi kupanda kadiri siku zinavyozidi kuendelea!
..zaidi ni kuwa kiwango hiki kililipwa kwa spika ndugu, J. Ndungai aliyekuwa amelazwa india kwa matibabu yaliyokuwa si chini ya miezi mitano, na pia hata aliyekuwa spika mstaafu Ndugu, S. Sitta baada ya kumaliza muda wake wa ubunge alilazwa nchini uingereza na bunge liliwajibika kumlipa japokuwa hakuwa mbunge!
..hivyo, basi kwenye hili suala la Lissu, ni vyema zaidi busara ikatumika kuliko kuingiza siasa na viroja, ili aweze kupata stahiki zake!
Wabunge wote, waungane wamtetee, mbunge mwenzao bila kujali itikadi, maana kama watashindwa kumtetea mbunge mwenzao, vipi kuhusu raia/ wananchi ambao ndio wapiga kura waliowapa dhamana..!? Watatetewa na nani...
Hakika, TAML usinyamaze kamwe...
Sent using Vertu Signature Cobra