Haya ndio mabadiliko ya tume huru yanayo pendekezwa na wana CHADEMA. Je, unakubaliana nao?

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
302
274


Wanabodi,

Siku mbili zilizo pita, wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) walifanya kongamano jijini Dar Es Salaam katika shughuli zao za kudai tume huru ya uchaguzi. Katika kongamano hilo, wanawake hawa walipewa majukumu ya kudai tume huru huku wanaume wakipewa majukumu ya kudai katiba mpya na wazee kudai haki.

Mwanzilishi wa jukwaa la katiba Tanzania Bw Deus Kibamba alihutubia kongamano hilo ambapo kama chama wali elezea mapendekezo waliyonayo kwa ajili ya tume huru ya uchaguzi. Kusikiliza mapendekezo hayo angalia video iliyo ambatanishwa kwenye chapisho hili (1:37:00 mpaka 2:15:00)

Mapendekezo hayo ni kama ifuatavyo

1. Katiba iliyopo haielezi vya kutosha kuhusu tume huru ya uchaguzi. Sura nzima inayo zungumzia tume huru ya uchaguzi iongezwe kwenye katiba. Sura hii iwe baada ya sura ya kwanza na iitwe "Madaraka ya umma kupitia demokrasia ya uchaguzi Tanzania".

2. Katika sura hiyo, ina pendekezwa kuwe na tamko, " Nchi hii itaongozwa kwa misingi ya uhuru, haki na demokrasia. Kutakuwa na chombo cha kusimamia haki za wananchi kupitia vyombo vya uchaguzi.

3. Jina la tume uhuru liwe " Tume huru ya uchaguzi Tanzania" au kwa Kiingereza " Tanzania indepent electoral commision (TIEC)" na kwa Zanzibar " Zanzibar independent electoral commision"

4. Muundo wa tume huru: Tume iwe na kamisheni na secretariet. Kamisheni iwe na wajumbe 7. Mwenyekiti na makamu wake wawe majaji au majaji walio staafu. Mjumbe mmoja atoke chama cha wana sheria. Wajumbe wengine wawe na vigezo vya kuwa majaji. Vigezo hivyo vyakuwa majaji lazima wawe navyo kwa muda wa miaka 15 kabla ya kuwa viongozi kwenye tume huru.

Tume huru iwajibike kwa mambo yote ya kisera na kimaamuzi. Secretariet ya tume iwe chini ya mkurugenzi wa tume ya taifa ya uchaguzi na sio mwenyekiti.

Mwenyekiti ndio asimamie uongozi wa kamisheni ya tume ambayo ndio bodi. Kamisheni ihusike kwenye kusimamia, kushauri, kuinidhamisha na kuiwajibisha secretariet.

Wafanyakazi wa tume: Watumishi wa tume wanao jitegemea

5. Mwenyekiti wa tume: Kuwe na mchakato ambao unahusisha vyombo vya kitaalam. Kwa mfano team ya majaji kupendekeza majina mawili kwa Rais baada ya kuchuja. Rais amchague mmoja wao na kupeleka jina bungeni. Wabunge wamjadili aliye chaguliwa na kupitisha. Jina la mwenyekiti lipelekwa kwa jaji mkuu kabla ya kuapishwa.

6. Mkurugenzi wa tume: Nafasi za ajira zitangazwe kwasababu ni mtaalam. Majina ya washindi ya pelekwa kwenye kamati ya uchaguzi

7. Uhuru wa bajeti uwepo kwa tume huru

8. Wagombea binafsi kuruhusiwa kugombea kwenye uchaguzi

9. Vyama vya siasa viruhusiwe kuungana wakati wowote

10. Matokeo ya uchaguzi yaweze kupingwa mahakamani

11. Ushindi wa uchaguzi wa urais uwe ni baada ya kupata kura zaidi ya nusu

Je, unakubaliana na maoni ya wana CHADEMA?
 
Wawe tayari kutoa jasho, na ikibidi hata kuishi mahabusu kuipigania hiyo tume.

Ni wajibu wao kuwashawishi waTanzania na kuwaelimisha kuhusu matakwa ya hiyo tume ili wananchi wawaunge mkono kwa hayo wanayoyapendekeza.

Wananchi waeleweshwe kungali mapema, bila uwepo wa "Tume Huru", hakuna uchaguzi utakaofanyika 2025; na kazi ya kuuzuia uchaguzi huo wakabidhiwe wananchi wenyewe kuitekeleza.

Kuna kazi kubwa na ngumu mbele yao, lakini ni kazi inayowalazimu waifanye, tena kwa ufanisi mkubwa katika miaka hii mitatu na ushee, kabla ya uchaguzi.

Hakuantena cha lelemama, CCM hawana mchezo mbele ya utamu wa kujinufaisha wenyewe.
 
Wakati wa mchakato wa maoni nilipendekeza mwenyekiti wa tume asiteuliwe, nafasi itangazwe na wagombea wachujwe na jopo la majaji kulingana na ujuzi wao na mshindi aapishwe na mahakama, siyo rais. Hivyo sikubaliani na namba tano.
 
....na tume hii iwe na wafanyakazi wake hadi ngazi ya kata sio kutumia political cadres wa chama dola
 
Back
Top Bottom