Haya Matukio yananifanya niwe na Wasiwasi zaidi na 'Professionals' walioko nchini kwangu Tanzania

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,518
108,794
1. Meli ya MV Bukoba ilipozama Ziwani tarehe 21 May, 1996 Wamarekani kupitia Satellite yao waliona na Kutushtua huku wenyewe tukibung'aa bung'aa tu.

2. Miaka kama Mitano au Saba iliyopita (kama sijasahau) Mvua Kubwa sana ilinyesha Mkoani Dar es Salaam iliyoleta Madhara makubwa cha Kushangaza Mitambo ya Hali ya Hewa ya Marekani ilishaona na Sisi Waswahili kama Kawaida yetu tulikuwa tunabung'aa bung'aa tu.

3. Hivi karibuni tu nchi ya Marekani kupitia Ubalozi wao umetoa Tahadhari juu ya uwepo wa Tukio ( Tishio ) la Ugaidi nchini Tanzania huku wenye Kazi yao (Intelijensia) Police Tanzania wakiwa hawajui lolote na kama Intelijensia ya Police Tanzania inachokijua ni kujua tu wapi Vijiwe vya Gongo na Bangi vilipo.

Tanzania bado sana.
 
Kwani wewe huwezi kuunganisha dots kuwa Wamarekani walimaanisha Ujio wa Lissu ndio Viashiria vya Ugaidi nchini? Unafikiri Intelijensia ya Tanzania hailijui hilo?
 
Nilipata kuisoma hiyo taarifa na ilitolewa moja kwa moja na United States Embassy, Ingawa wao walionya zaidi juu ya tishio la kuwepo kwa vikundi vidogo vidogo vya uhalifu kufuatia na taharuki za mihadhara ya kisiasa inayoendelea hapa nchini na kusema kwamba wageni kuwa makini katika maeneo ya mahoteli,migahawa,viwanja vya ndege na N.K
 
Tunahitaji mabadiliko makubwa nchi hii. La ajabu wanaokuwa viongozi ni wale wapuuzi wasio na weledi wala elimu. Wenye elimu kamwe hawapewi nafasi.

Wazungu wanajua madini yetu yapo wapi na ni kiasi gani kuliko sisi na tunategemea takwimu zao kujua tuna gesi, wanyama, mafuta, nk kiasi gani!
 
Genta omba scholar ukasome uje kutusaidia kusukuma gurudumu la Tz

Hlf upewe kitengo ili uendeshe mambo

Charismatic fellar game changer
Labda nikasome zaidi nikayasaidie Mataifa makubwa Mawili ninayoyapenda yenye Viongozi Intelligent na Mataifa yenye Raia (Wananchi) Intelligent ya Rwanda na Israel ila siyo Tanzania ambako Watu Werevu (Intelligent) Wanapuuzwa na Kudharauliwa mno na Wenye Mamlaka.
 
Back
Top Bottom