GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
- Hivi kweli logically tu Mtu unaweza ukawa umepatwa na mateso ya karibia na kuuliwa pengine yaliyoambatana na ' ufirauni ' mwingine halafu ukakosa nguvu na ukawa hujiwezi kabisa na huku damu zikikutiririka lakini nguvu za kuvunja mlango ukawa nazo?
- Hivi kiusalama au kiutaratibu tu Mtu unaweza ukawa umeumizwa au kufanyiwa matendo ya kikatili halafu badala ya usiku huo huo wa Saa 9 kwenda kuripoti Police Wewe unaamua kwanza kulala pamoja na maumivu yako yote makali ambayo pengine yangehitaji Wewe kupelekwa Hospitali kupatiwa matibabu ya haraka? Hivi kuna asiyejua kuwa Kituo cha Police cha Oysterbay huwa kipo wazi 24 hours?
Japo nazidi kuchanganyikiwa na haya mawili ILA sijakubali ' usanii ' huu na nadhani hapa sasa ndiyo nyie mnaojiita Great Thinkers wa hili ' Jamvi ' la JF mjitokeze ' kutiririka ' ili muweze kutupa ' ufafanuzi ' wenu wa Kimantiki kabisa.
Nasubiri nione ' mtiririko ' wenu wa kihoja ili ikiwezekana basi kutokana na hiyo michango yenu mtakayoijenga hapa juu ya hayo ' matukio ' mawili na Mimi GENTAMYCINE sasa niweze ' Kukomaa ' na kuwa Great Thinkers kama nyie na niachane rasmi na huu ' Upopoma ' au ' Ungumbaru ' wangu.
Nawasilisha.