mtotomtamuu
JF-Expert Member
- Dec 4, 2016
- 602
- 1,454
Ifike mahali Serikali yetu iwe kitu kimoja linapokuja suala la msimamo halisi wa Nchi. Nchi nzima iegemee kwenye ukweli ili kama haya mateso tunayapata tujue tunayapata kwa usalama wetu au kwa ajili ya siasa
Nimetoka Ubungo leo kuelekea mbagala hadi sasa Serikali haijaruhusu magari kusimamisha abiria, sasa kitu kilichonisikitisha zaidi ni namna ya Abiria wabavyopangwa kama mafungu yani watu wanapata shida sana, sehemu ya kusimama ile kwenye mabasi makubwa yale ya Eicher watu wanachuchumaa kwa mstari kama wakimbizi, yote hayo askari asijue kama kuna watu wamesimama kuepuka faini, Na watu wengi wanakosa usafiri sababu gari ni chache na sheria ni level seat
Sasa kinachonishangaza mimi ni Serikali imetangaza kuwa kwa sasa kumesaliwa na wagonjwa wanne nchi nzima na kuaminisha watu kuwa hali ni shwari na watu kwa sasa barakoa washazitupa na wanajiachia, sasa kama mnachokisema ni kweli kwa nini muache watu wanateseka kwenye usafiri wa Daladala?
Ni muda muafaka wa Serikali kurudisha usafiri wa Dala dala kwenye hali yake kama kweli hali ni shwari la sivyo mtakuwa mnatudanganya,