Haya matatizo ya wizi wa air-port na bandari bado hayaja kwisha tanzania?

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,293
Points
2,000

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,293 2,000
[h=1]MSAADA TUTANI: YALE YALEEEEEE.....[/h]
Anko nanihii ambaye ni mkuu wa
wilaya ya nanihiino na balozi wa nanihii,

Bila kukupoteza muda, naomba unisaidie kupata maoni ya wadau kuhusu swala hili ambalo kwa muda sasa linanisumbua saaaaaaaaana kichwa. Ni kuhusu wizi wa mizigo Airport ya uwanja wa ndege Dar.

Sijui mimi nina gundu, sijui ndo utaratibu? ila nimechoka.

Mwaka jana June nilienda home kutoka Japan nilikuwa na digital Camera nne,laptop moja, simu za mkononi tatu na vifaa vingine vidogo vya electronics. Hizi zilikuwa ni zawadi kwa ajili ya ndugu zangu kwani ilikuwa ni siku
nyingi sijaenda nyumbani..


Tulivyotua eapoti ya uwanja wa ndege wa Dar, nilishangaa kuona masanduku yangu hayajafungwa. Na ile kufungua nikakuta vitu vyangu vyote havimo! Nikalalamika sana mpaka kwa mkuu wa kitengo cha mizigo nikaambiwa wala hawajaona kitu.

Nikabwaga manyanga...vekesheni yangu yote sikuwa na raha.

Sasa la kusikitisha zaidi, juzi nilikutana na mzungu mmoja raia wa Norway, yeye ni mhadhiri wa wa Chuo. Katika maongezi yetu nikamwambia natokea Tanzania, akasema alikuwa Tanzania mwezi wa tano ila akasema hatasahau safari hiyo, kisa? Akasema aliibiwa vifaa vyake vyote vya electronics alivyofika Airport.

Anasema aliumia sana kwani aliibiwa laptop iliyokuwa na information muhimu sana alizotakiwa kupresent kwenye mkutano Tanzania, kidogo achanganyikiwe.

Sasa hapa ndo mambo yananichanganya zaidi, kabla ya kwenda nyumbani nilituma laptop mbili kupitia Express mail, nilitrack mzigo mpaka Dar. Ila zilivyofika Dar. Posta wakasema kwamba hawajapata mzigo wowote na wala hawana information zozote, niliongea na Postal manager Dar. akasema wala wao hawausiki kabisa na kupotea kwa mizigo kwani hawaiwafikii.

Naomba wadau mnipe mawazo, tukisafiri na vitu vyetu wenyewe vinaibiwa na tukisema tuvitume bado vinaibiwa! Besides insurance, nini cha kufanya kuhakikisha unapata mizigo yako kamili?

Na nimefuatilia na watu wa ndege wanasema mizigo haifunguliwa tena mpaka final destination. Tafadhali nimechooka na hii kitu.

Mungu azidi kutubariki
Libeneke lidumu

Mdau Mwenye Usongo
 

Visenti

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2008
Messages
1,029
Points
1,170

Visenti

JF-Expert Member
Joined Jul 24, 2008
1,029 1,170
Mzizi mkavu, Pole sana mkuu, wizi wa mizigo eapoti ni janga la dunia nzima, si swala la JNIA tu, inashauriwa kuwa;-

  1. Usiweke vitu vya thamani ktk mzigo ambao utakuwa "checked"
  2. Fungasha mzigo wako kwa kutumia TSA-approved luggage locks or locking luggage straps

Kuhusu kutuma vitu vya thamani toka majuu ni bora utumie courier kama DHL au FedEx, vifurushi vyako kamwe visipitie Posta ambako siku hizi wanaiba hata barua!
 

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2011
Messages
31,204
Points
2,000

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2011
31,204 2,000
pole sana....

Vitu vya thamani usitumie posta, dhl mpango mzima......

Sera ya wizi airport na bandari itakuwa wameitoa kwa ccm.....wanafisadi tu mizigo ya watu, na wahusika wametia pamba masikioni
 

Forum statistics

Threads 1,389,121
Members 527,846
Posts 34,017,499
Top