Haya matamshi ni kusudi zao?

Maalim Jumar

JF-Expert Member
Dec 28, 2010
1,259
117
Habari zenu?
Nmekutana na baadhi ya watu wakitamka haya maneno...
1-Msa=Musa.
2- Mk*ndu=Mwekundu.
3- Mwananke= Mwanamke.
4- Leli=Reli.
5- Reri= Reli.
6-...................
7-....................
Endeleza!
 
Hayo maneno yapo mengi tu list haitakwisha na kama ume notice kila watu eneo fulani matamshi yao ya kiswahili yanakua tofauti, na hii ni kwasabu ya ile lugha asilia (native language) ambayo mtu anaiongea tokea utoto hivyo kumsababishia pronounciation yake ya kiswahili iwe vile. Kwa mfano hawa ni wakina nani? "Ntu kun'nyima kitu dhambi" akimaanisha kumnyima mtu kitu ni dhambi! Mifano ni mingi mno.
 
Habari zenu?
Nmekutana na baadhi ya watu wakitamka haya maneno...
1-Msa=Musa.
2- Mk*ndu=Mwekundu.
3- Mwananke= Mwanamke.
4- Leli=Reli.
5- Reri= Reli.
6-...................
7-....................
Endeleza!

Maalim umenichekesha sana...yaani bila kutaja yale mambo siku haijaenda kabisa.
hapo namba mbili umelazimishia labda utuambia unamaanisha nini hasa...
 
hapana wanielewa vbaya ndugu yangu!
Gaya maneno yameenea sana...hujawahi sikia?
 
Kwa kiswahili tunasema rahaja na wakati mwingine ni rafidhi ya watu washio maeneo mbali mbali.
 
Nkate=mkate. Nchuzi=mchuzi. Laisi=rais. Bola=bora. Lafiki=rafiki. Ntoto=mtoto. Lambilambi=rambirambi. Duh hayamaliziki yako mengi mno.
 
mi mwenyewe huwa hili neno nalisahau sana
chengine = kingine
naniliu = nanilii (au yote sio maneno ya kiswahili)
 
Kwa kiswahili tunasema rahaja na wakati mwingine ni rafidhi ya watu washio maeneo mbali mbali.
Si rahaja(lahaja) wala rafidhi(lafidhi)...naona umetutega XP.
Na hayo maneno si ya kiswahili ni yakiarabu...japo wengi hawatofautishi kiarab na kiswahili.
 
Maalim umenichekesha sana...yaani bila kutaja yale mambo siku haijaenda kabisa.<br />
hapo namba mbili umelazimishia labda utuambia unamaanisha nini hasa...
Ukikaa na washihir utacheka sana!
Mf*ra=Mpira.
Ub*o=ubao.
 
1.kuoga=kukoga au kuoga maji...kwani watu huogaganini? ukisema kuoga tutaelewa

2.kukojoa=kukojoa mkojo.....kwani watu wanakojoaga nini?ukisema kukojoa tutaelewa
 
nkuu una utani na wale ndugu zangu jua linakochomoza?
Nkate=mkate. Nchuzi=mchuzi. Laisi=rais. Bola=bora. Lafiki=rafiki. Ntoto=mtoto. Lambilambi=rambirambi. Duh hayamaliziki yako mengi mno.
 
Ustake ncheke! - Tanzania Kusini
Naomba maandazi Mbili - Kenya Nairobi
 
ajaja=hajakuja=hajaja=hakuja.
Hapa sijaelewa neno lipi ndio sahihi kufikisha ujumbe.
 
hivi hakuna neno jingine mbali na lugha ya kiarabu...kwa swahili? Neno Samaki.

-garlic =kitunguu thawm.
-union=kitunguu maji.
Ni sawa hizi maana ? Kwa swahili ni vipi tutamke?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom