Haya Mapigano ya Wasonjo na Wamasai Mpaka lini?

Kiti

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
359
234
[h=2]Watano wauawa mapigano kati ya Wasonjo, Wamasai[/h]


Na Charles Ngereza



13th October 2011


email.png

B-pepe



printer.png

Chapa



comment_bubble.png

Maoni









WATU watano wa jamii ya Kimasai, wameuawa katika mapigano yanayoendelea kati ya Wamasai na Wasonjo.
Akizungumza na Nipashe jana, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali, alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo.
“Ni kweli watu watano wameuawa jana usiku na wanatokea Kijiji cha Magaiduru,” alisema bila kutaja majina ya marehemu.
Alisema hali ya usalama sio nzuri kutokana mazingira ya vijiji hivyo kutawanyika na misitu mikubwa.
“Siwezi kukupa taarifa zote. Kwa sasa tupo na vikosi vya polisi huku porini. Kesho nitawapa taarifa kamili ya hali halisi,” alisema.
Naye mwangalizi wa hospitali teule ya Wasso, Moses Kikonya, alisema maiti za watu hao zilifikishwa katika hospitali hiyo jana asubuhi.
Alisema mpaka sasa majina ya watu hao hayajafahamika ila wanadaiwa kutoka katika familia ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Oloirien Magaiduru Kashanga Kusalet.
Alisema miongoni mwa miili ya marehemu hao, ipo ya mtoto wa miaka mwenye umri unaokadiriwa kuwa miaka mitano na mwanamke mmoja na wazee watatu wenye umri wa miaka kati ya 50 na 60.



CHANZO: NIPASHE


0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom