Poleni kwa majukumu ndugu zangu.
Mi ni msichana niko kwenye mahusiano na mwanaume mmoja. Lakini simuelewi kabisa maana hataki tuitane majina kama baby, dear, sweet nk. Yaani anataka tuwasiliane kawaida na tuitane majina yetu halisi. Ukimuliza anasema we niite vyovyote.
Kingine amekuwa ni yeye tu anakuja kwangu lakini kwake anasema utapafahamu tu. Akija namwandalia chakula anakula anashiba na matunda atajisevia kwenye friji lakini cha ajabu hatoi hata 500 akuambie hata nunua mboga na wote ni wafanyakazi.
Hata nikiumwa atauliza tu unaendeleaje na akija haji hata na ndizi ya 200. Anakuja anasubiria ale aondoke. Sio siri wapendwa ananikera lakini nitumie lugha gani kumfikishia ujumbe? Anadai ananipenda lakini napata wasiwasi hivi hata tukiishi pamoja atakuwa responsible kwel!
Naombeni mawazo na ushauri wenu wapendwa maana nawaza bila kujua la kufanya.
Asanteni.