Haya Mambo ya team ndani ya CCM Ni fake news

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,086
42,891
Mtu yupo huko alipo anaamka asubuhi anaanza kujifanya anakijua chama vizuri anaanza kukuchambulia team zilizopo CCM kumbe hata kikao kimoja Cha chama hajawahi kuhudhuria.

Atakusimulia kwamba CCM Kuna team Membe mara CCM sijui Kuna team Nape kumbe uzushi mtupu.

Kwa taarifa yenu CCM ni miongoni mwa vyama imara sana Africa hakiyumbishwi kama mnavyofikiria. Hakuna cha teams wala kikundi chochote kisicho rasmi chenye nguvu kuzidi nguvu ya vikao chini ya Mwenyekiti.

Kwahiyo nawasihi acheni kupoteza muda kuwaza mambo ambayo hayapo. Makundi ndani ya chama yalishazimwa yote baada ya uchaguzi kila kiongozi amerejea kwenye kazi yake wajumbe na wenyewe wamepunguzwa so hakuna tena zile za kujuana kwenye chama.

Mnaotegemea ndani ya CCM kutakuwa na kutokueleweana leteni ushahidi wenu hapa. Kama hamna ushahidi kaeni kimya acheni kutunga hadithi mkifikiri mtawagombanisha wale mabwana. Wakina Membe na kina Lowassa walishamaliza mgao wao na sasa ni zamu ya JIWE kusukuma gurudumu Mpaka 2025.
 
CCM mtu anaenda na mwili tu akili anaicha alikotoka unafikiri kutokuelewana kungetokea wapi? Akili inayotumika na mtu mmoja tu wengine wanafuata kwa makofi na ndiyo, ila sehemu yoyote yenye watu wanaotumia akili zao wenyewe kufikiria lazima kutokuelewana kupo mkuu nikusema tu ipo steji ipi,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe umehudhuria kikao kipi cha chama ukajua hazipo hizo timu?


Loyalty To country Alyways,To government When it deserves
 
Neno hilo hao uvccm hawataki kulisikia kabisa maana wao ndoto zao za kila uchao ni ccm mbele kwa mbele hata kama inafyatuka gia
CCM mtu anaenda na mwili tu akili anaicha alikotoka unafikiri kutokuelewana kungetokea wapi? Akili inayotumika na mtu mmoja tu wengine wanafuata kwa makofi na ndiyo, ila sehemu yoyote yenye watu wanaotumia akili zao wenyewe kufikiria lazima kutokuelewana kupo mkuu nikusema tu ipo steji ipi,

Sent using Jamii Forums mobile app

In God we trust
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom