Haya mambo ya Kutekana yalianza awamu ya nne, wakati wa mzee Mkapa hayakuwepo

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,745
139,523
Haya ya " fulani" katekwa na kuokotwa eneo fulani yalianza kusikika kwa uwazi katika serikali ya awamu ya 4.

Ndipo tulisikia Rais wa wanafunzi pale Muhimbili katekwa na kutupwa Mabwepande......mara Kubenea kamwagiwa tindikali.....mara mwandishi Kubanda katekwa na kung'olewa jicho nk nk.

Nimuombe Mungu wa mbinguni aturehemu waja wake tuondokane na hii hofu maana mtu akikamatwa kwa uchunguzi fulani raia wasikimbilie kusema katekwa maana inawaumiza na kuwatesa wanafamilia.

Ni hayo kwa uchache.

Maendeleo hayana vyama!
 
Niliposema bora JK aondoke,baadhi ya watu hawakunielewa na hata leo wengi hawanielewi.

Tukiendeleea hivi,ipo siku atakuja mwingine atafumbia macho watu kupigwa shaba hadharani, na kwa ujinga, mtasema bora JPM.

Awamu moja ikiweka precedent mbaya pasipo hatua zozote kuchukuliwa na ikafika hatua ikazoeleka,basi maana yake ni kuwa, awamu inayofuata inaweza kufanya mabaya zaidi kwani yale ya awamu iliyotangulia yalifanyika pasipo kuchukuliwa hatua zozote na yakapita

Watakaokuja kuunga mkono uzi wako huu ndio hao hao wanaoamini uzi wangu huu hapa chini nilikosea kuandika(ujinga wa mwanadamu).

Haya ya " fulani" katekwa na kuokotwa eneo fulani yalianza kusikika kwa uwazi katika serikali ya awamu ya 4.

Ndipo tulisikia Rais wa wanafunzi pale Muhimbili katekwa na kutupwa Mabwepande......mara Kubenea kamwagiwa tindikali.....mara mwandishi Kubanda katekwa na kung'olewa jicho nk nk.

Nimuombe Mungu wa mbinguni aturehemu waja wake tuondokane na hii hofu maana mtu akikamatwa kwa uchunguzi fulani raia wasikimbilie kusema katekwa maana inawaumiza na kuwatesa wanafamilia.

Ni hayo kwa uchache.

Maendeleo hayana vyama!

Nani hasa anawatuma hawa?

Tumeshindwaa Ku-deal na hawa wahalifu?
 
Kwa sasa nadhani wanashikiliwa tu siyo kutekwa.

To me Dr Uli ndo naweza sema yes alitekwa kweli kule kutekwa nakokujua mimi.

Leo hii Mtu anapatikana hana hata mchubuko hana hata njaa wala kiu ana nguvu zake hadi za ku-tweet na hawezi hata kusema nini kimetokea zaidi ya blah blah!
 
Haya mambo yakiendelea kuna siku raia nao watachoka na hivyo kuanza kujibu mashambulizi. Na huo ndiyo utakua mwanzo wa uasi ndani ya nchi!

Ni bora wanao husika, wakaachana na huu uhuni, maana kuna njia nyingi sahihi za kutumia kwenye ujenzi wa Taifa moja, badala ya hizi za kutisha na kujenga hofu kwa wananchi. Kwa nini umtese, umuue, umdhalilishe binadamu mwenzako! kisa madaraka!!!
 
Kwa sasa nadhani wanashikiliwa tu siyo kutekwa.

To me Dr Uli ndo naweza sema yes alitekwa kweli kule kutekwa nakokujua mimi.

Leo hii Mtu anapatikana hana hata mchubuko hana hata njaa wala kiu ana nguvu zake hadi za ku-tweet na hawezi hata kusema nini kimetokea zaidi ya blah blah!
Kama yule mmiliki wa wekundu wa msimbazi....alienda mwenyewe hadi hotelini kuwapigia simu wazazi wake wakamchukue!
 
Kwahiyo unataka kusema isha kuwa kawaida yaendelee?
Haya ya " fulani" katekwa na kuokotwa eneo fulani yalianza kusikika kwa uwazi katika serikali ya awamu ya 4.

Ndipo tulisikia Rais wa wanafunzi pale Muhimbili katekwa na kutupwa Mabwepande......mara Kubenea kamwagiwa tindikali.....mara mwandishi Kubanda katekwa na kung'olewa jicho nk nk.

Nimuombe Mungu wa mbinguni aturehemu waja wake tuondokane na hii hofu maana mtu akikamatwa kwa uchunguzi fulani raia wasikimbilie kusema katekwa maana inawaumiza na kuwatesa wanafamilia.

Ni hayo kwa uchache.

Maendeleo hayana vyama!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sema labda yalipumzika lkn yalianzia kipindi cha Mwalimu Nyerere.
Sikumbuki watu kutekwa wakati wa Nyerere zaidi ya kusoma mambo ya utekaji kwenye vitabu vya Elvis Musiba staring akiwa Willy Gamba.

Ninachokumbuka ni watu kuwekwa kizuizini!
 
Sikumbuki watu kutekwa wakati wa Nyerere zaidi ya kusoma mambo ya utekaji kwenye vitabu vya Elvis Musiba staring akiwa Willy Gamba.

Ninachokumbuka ni watu kuwekwa kizuizini!

Kwa kuwa tu haukumbuki haimanishi haikuwepo na sio tu walitekwa waliluliwa na wengine kufukuzwa nchi waliozaliwa na kuishi uhamishoni mmojawapo Munishi.
 
Kwangu mimi Ben Mkapa ndio rais bora kabisa, sijui lini tutampata mwingine kama yeye, alipikwa na mfumo akapikika.
Kumbuka naye alikuwa na kasoro zilizopelekea wapinzani wake kumuona hakufa kuwa rais.

Huwa tunakumbuka vizuri baada ya kupata kibaya, maana sasa tunalinganisha tulichonacho na kile tulichokikataa au kukipoteza.
 
Sema labda yalipumzika lkn yalianzia kipindi cha Mwalimu Nyerere.

Kwa hili uko sahihi, huu mchezo ulikuwa toka enzi za Nyerere,na kilichomsaidia Nyerere upande wa pili wa tabia zake kutofahamika ni kutokuwa na vyombo vya habari huru na vichache, na huu wigo mpana wa upashanaji habari wa hivi sasa haukuwepo. Hata hili tatizo la kuchezea uchaguzi, muasisi wake ni Nyerere kwa sababu alichokua anaongea kwenye mfumo wa siasa za vyama vingi, haikuwa anachomaanisha maana hukuwa muumini wa hoja kinzani.

Huu mchezo wa kuteka na kuwafanyia ukatili wale wote wanaokosoa mwenendo wa serikali ulishamiri wakati wa JK, chini ya kina Mwigulu, Wassira nk. Kilichosaidia kufunika uovu ule wa JK ni uhuru wa vyombo vya habari ambao ilikuwa kama speed gavana ya Ule uhayawani. Sasa hivi kwenye awamu hii ya Magufuli ndio imekuwa fashion, na pazia la tabia hiyo ni hii miundombinu michache inayotekelezwa. Sasa hivi inaonekana ni sawa kabisa kubambikizia kesi, kuteka, kupiga risasi, kumuua mkosoaji yoyote kwakuwa kuna ujenzi wa reli ya SGR, bwawa la umeme nk. Na kwakuwa watu wameingia woga, wanaishia kulalamika chini chini.

Matokeo ya tabia hizi zisizowafurahisha watu, ndio unaoana serekali inaona inafanya vyema lakini watu hawajitokezi kupiga kura, na hata kusifia, watu wanafanya hivyo kwa ajili ya hofu. Inakuwa kama umembaka mwanamke kisha unataka ule mate na yeye akubusu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom