Haya mambo ya kumwagiana maji wakati wa 'Birthday' mtakuja muue mtu

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,898
11,745
Nimekuwa nikiona watu mbalimbali wanafanya hizi sherehe za kuzaliwa wanamwagiwa maji wanaloa tepe tepe ipo siku mtaua mtu na huo ushamba wenu, kwanza sherehe gani hiyo ya kumwagiana maji kiasi hicho, yaani unamkuta mwanaume na ndefu zake baba jitu zima na lenyewe linamwagiwa maji au kumwagia wengine wanaume tumebaki wachache.

Hivi hakuna namna nyingine ya kusherehekea bila kumwagiana maji, hivi mnajua kuna wengine wamezaliwa na matatizo yao ya kiafya, hivi ulimbukeni wa kumwagiana maji tumeutoa wapi hivi kwa huu ujinga nchi hii itapata maendeleo kweli, hata kama ni kumbukumbu nyie mmezidi.
 
Yaan bahati nzuri siku yangu ya kuzaliwa ipo sikukuu kila mtu busy la sivyo tungegombana na watu
 
Back
Top Bottom