Haya mambo ya hatujapokea taarifa au hatujatangaziwa hata Mwalimu Nyerere aliyakataa

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,188
2,000
Hivi karibuni kumekuwa na matamko mfano hatujapewa taarifa kwamba kwenda kuhiji ni lazima mahujaji wawe wamechanjwa chanjo ya Corona AU hatujapewa taarifa toka Kenya kwamba mahindi toka Tanzania yamezuiliwa kuingia Kenya n.k.

Hizi kauli hata mzee Nyerere aliwahi kuzikataa eti hatujatangaziwa kwamba azimio la Arusha limeisha kufa, kwani unangoka utangaziwe si akili yako tu inatosha kujua azimia la Arusha limekufa, kama kuna Azimia la Zanzibar ambalo lilieleza watu wafanye kinyume na azimio la Arusha, mfano ruksa kuwa na hisa katika makampuni, ruksa kulima mashamba makubwa n.k hiyo pekee si inatosha kabisa kukujulisha azimio la Arusha limekufa? UNANGOJA UTANGAZIWE?

Kweli unangoja mtu akutangazie kwamba kwenda Macca hadi uchanjwe kwani wewe hujiongezi? Hivi kweli nchi itaruhusu wageni zaidi ya Millioni mbili kutoka sehemu zote duniani waingie bila tahadhari yoyote? Unangoja tangazo kwani wewe huna akili ya kujua tu kwamba lazima hatua fulani zichukuliwe?

Hili la Mahindi unangoja tangazo kwani vifaranga vile 6000 vilivyoingizwa toka Kenya na kuteketezwaa Arusha wakati ule Kenya walisubiri tangazo

Inatakiwa kujiongeza.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom