Haya mambo makubwa inayofanya Serikali ya awamu ya 5 utayafaninisha vipi na machozi ya watu hawa?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Niwaulize wale mnaokesha kusifu serikali ya awamu ya 5 kua inafanya mambo makubwa sana, hivi mnaelewa kuna watu wanaumia na kuteseka kama haya makundi kwenye nchi yetu?
Vilio na machozi ya makundi ya hawa watu mtayafananisha na hayo yanafanywa?

1.Wakulima wa korosho
2.Wakulima wa Mbaazi
3.Watumishi wa umma
4.Wasiokua na ajira
5.Waliopoteza ndugu zao kwa kutekwa na kupotezwa
6.Vyama vya upinzani
7.Wafanya biashara
8.Asasi za kiraia
10.Viongozi wa dini
11.Wanafunzi vyuo vikuu

Hivi tunaelewa haya makundi yapo katika hali gani? Maumivu yao tunaweza kupima thamani yake na haya yanayofantwa na saerikali ya awamu ya 5? Kuna tatizo gani miradi ya maendeleo kuendelea kutekelezwa huku watu wakilifurahia taifa lao kuliko majonzi?

Nisiwe msemaji sana lakini muda hua shahidi mzuri wa kila jambo.
 
Mkuu acha unafiki nani kakwambia wanavyuo tuna majonzi na serikali yetu acha unafki sisi tunafutahia juhudi zinazofanywa na serikali yetu
 
Ishu ya Korosho ni kithibitisho tosha hata binti wa chekechea akipewa urais ataweza tu na mambo kwenda.

Yani kwa maksud unaharibu uchumi na kuvuruga maisha ya watu.
 
mkuu acha kuropoka unajua takwimu za wanachuo waliojiunga na ccm ndani ya miaka mitatu ya dr jpm
Duuuh nyie ndio wasomea tumbo.

Hivi kujiunga na CCM ndio maendeleo ?
Hujui hata hata Al- Shabub ina wanachama na Mashabiki Dunia nzima ?
Na wasipodhibitiwa Kundi hilo litakua na wanachama wengi sana kila mahali.

Hivi unafikiri kuwa CCM hawajui kuwa umaskini na Ujinga ni Mtani mkubwa wa wao kuendelea kutawala.

Unafikiri ni kwa nini nchi zote zenye maendeleo na ambazo binadamu yeyote na kiumbe yeyote hata mbwa anafutahiya kuishi sana vyama vingi na hawana ujinga wa kurubuni wanavyuo na wasomi ili wawaunge mkono huku Demokrasia ikihujumiwa?

Kama Mwanafunzi aliyewaokoa wenzake wasiangukiwe na Majengo yenye nyufa alikamatwa na kuwekwa ndani na wanaCCM wakashangilia nani ataokoka akiwa nje ya CCM?

Wanasiasa wabinafsi na wapenda vyeo na madaraka sio tu wanawatia watu umaskini lakini hata wakigundua kuwa kuwaondoa kabisa kwanye viumbe wanaopumua itawasaidia kuendelea kutawala hawasiti wala hawafikiri mara mbili kufanya hivyo.

Dunia hii kuna binadam akikosa pesa wanaweza akawa Mchamungu ,mpole mwenye utu na akawa na subra. Lakini dunia hii hii kuna binadam akikosa pesa anakua jambazi ,muuaji na mnyang'anyi. Kadhalika wanasiasa na watawala . Kuna wanaotawala na kutenda haki hata kama haki hiyo itawakosesha Madaraka hawafanyi dhulma. Lakini pia kuna wanasiasa kama manyanganyi na majambazi ,wao madaraka ,vyeo,fedha ,kuheshimiwa,kutukuzwa na kusifiwa ndio kipao mbele chao. Hawaoni shida kugawa fedha kwa mamilioni kuhonga wapiga kura au kununua kadi za kupigia kura au kutumia mabomu na mabunduki na kuteka wagombea . Kinachotafutwa hapa sio maendeleo ya nchi bali madaraka ambayo ni sehemu rahisi ya kupata fedha nyingi huku wakiombewa na viongozi wa dini . Wezi wanabarikiwa na kiwekewa mikono ya baraka .
Ndivyo dunia ilivyo.
Gharama za kuua Demokrasia ni kubwa sana mana unaweza kuchukua mpaka maisha ya halaiki za watu kwa maelfu.

Haki kamwe haijawahi kuleta vita wala mauaji popote duniani mana haki inatendwa kwa maelekezo ya kumtii Mungu kabla ya yote.
Kura zikipigwa kwa wazi zikahesabiwa kwa wazi zikabandikwa kwa wazi bila vitisho na figisu kwa maana kuwa wote waliogombea ni binadamu wenye familia na ni ndugu zetu katika nchi moja. Matokeo yakasomwa kwa wazi kama waliyonayo mawakala wote bila kupiga na kutisha na kuzuia mawakala wengine kamwe hapawezi kutokea Vurugu na wenye haki wakapigwa na kuuawa na waovu kwa sababu waovu ndio wanaotawala kwa uovu.

Ndio maana Yesu au Issah alifundisha kuwa Siku zote tuombe Ufalme wa Mungu uje! Kwa maana kwamba ufalme wa Mungu utasimamia haki na dunia itakua na amani.
Wengi wanakimbilia CCM kwa sababu ya kuchoka kuuteswa na kuumizwa lakini sio kwa sababu ya maendeleo. Maendeleo yangekua yanabadili imani na itikadi basi Nchi za magharibi zote zingekua na Chama kimoja na za Asia na Afrka zingekua ndizo zina vyama vingi tangu Enzi hizo za Giza.

CCM siasa vyuoni sawa lakini vingine ni uhaini na uhalifu wa kuwafanya wanafunzi kufukuzwa vyuoni ; sio haki wala jambo la kufurahiya mana hujui kuwa watoto wako na wajukuu zako wote wataipenda CCM tu bila wengine kutopenda siasa na wengine vyama vingine.
Kama ilivyo mpira ; sio watu wote ni mashabiki wa Yanga au Simba . wengine hawana ushabiki wa timu yoyote. Kama tunavyotofautiana kwa nje ya miili yetu ,akili zetu na mawazo na maarifa na imani zetu pia zimetofautiana . Ndivyo tulivyoumbwa. Na kila mmoja anapenda kuona anatendewa jema kama mwingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Awamu ya tano imenunua ushindi wa Taifa Stars 🌟
Eti?

Nikweli. Nilianza kuwaza hivyo lakini uzalendo ukasema, usithubutu hata kuwazia jambo kama hilo!

Uganda hawakuwa na cha kupoteza? Walishavuka kwenda Misri?

Mbona maswali yanazidi kuwa mengi!

Acha nibaki na uzalendo wangu, bila kujali kama upuuzi huo ulifanyika kweli.
 
Siku zote MTU anayethamini sana Mali, hathamini utu wa wengine. Hivyo hivyo na anayethamini utu , Mali hazimbabaishi.
 
Niwaulize wale mnaokesha kusifu serikali ya awamu ya 5 kua inafanya mambo makubwa sana, hivi mnaelewa kuna watu wanaumia na kuteseka kama haya makundi kwenye nchi yetu?
Vilio na machozi ya makundi ya hawa watu mtayafananisha na hayo yanafanywa?

1.Wakulima wa korosho
2.Wakulima wa Mbaazi
3.Watumishi wa umma
4.Wasiokua na ajira
5.Waliopoteza ndugu zao kwa kutekwa na kupotezwa
6.Vyama vya upinzani
7.Wafanya biashara
8.Asasi za kiraia
10.Viongozi wa dini
11.Wanafunzi vyuo vikuu

Hivi tunaelewa haya makundi yapo katika hali gani? Maumivu yao tunaweza kupima thamani yake na haya yanayofantwa na saerikali ya awamu ya 5? Kuna tatizo gani miradi ya maendeleo kuendelea kutekelezwa huku watu wakilifurahia taifa lao kuliko majonzi?

Nisiwe msemaji sana lakini muda hua shahidi mzuri wa kila jambo.
lazima wengie waumie ili taifa lisonge,hakuna namna,ni principle hiyo popote pale duniani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu acha kuropoka unajua takwimu za wanachuo waliojiunga na ccm ndani ya miaka mitatu ya dr jpm
Acha kuropoka wewe Mpare unakijua unachoongea au ni huo mkopo ulioubahatika na kushika Kadi mkononi?
Vyuo vyote vimekatazwa kujiunga na Siasa na hasa UDOM ndio maana unatamba una Kadi ya Chama,
waruhusini basi ACT wajitangaze au wape uwanja hapo Chuoni kwako UDOM uone km kuna atakayebaki CCM
 
Niwaulize wale mnaokesha kusifu serikali ya awamu ya 5 kua inafanya mambo makubwa sana, hivi mnaelewa kuna watu wanaumia na kuteseka kama haya makundi kwenye nchi yetu?
Vilio na machozi ya makundi ya hawa watu mtayafananisha na hayo yanafanywa?

1.Wakulima wa korosho
2.Wakulima wa Mbaazi
3.Watumishi wa umma
4.Wasiokua na ajira
5.Waliopoteza ndugu zao kwa kutekwa na kupotezwa
6.Vyama vya upinzani
7.Wafanya biashara
8.Asasi za kiraia
10.Viongozi wa dini
11.Wanafunzi vyuo vikuu

Hivi tunaelewa haya makundi yapo katika hali gani? Maumivu yao tunaweza kupima thamani yake na haya yanayofantwa na saerikali ya awamu ya 5? Kuna tatizo gani miradi ya maendeleo kuendelea kutekelezwa huku watu wakilifurahia taifa lao kuliko majonzi?

Nisiwe msemaji sana lakini muda hua shahidi mzuri wa kila jambo.
Binadamu ni kiumbe muhimu kuliko kitu chochote. Kwani maendeleo unamfanyia nani kama sio binadamu. Unamuua binadamu na kumteka, kumvunjia nyumba anayoishi. Unamfanyia nani hayo maendeleo?? Hayo madaraja atapita nani kama co binadamu. Watanzania, hasa Magufuli na serikali yake wanatakiwa wajue kuwa binadamu ni kiumbe muhimu sana duniani kuliko kitu chochote. Huwezi kununua binadamu Magufuli jua hilo
 
Niwaulize wale mnaokesha kusifu serikali ya awamu ya 5 kua inafanya mambo makubwa sana, hivi mnaelewa kuna watu wanaumia na kuteseka kama haya makundi kwenye nchi yetu?
Vilio na machozi ya makundi ya hawa watu mtayafananisha na hayo yanafanywa?

1.Wakulima wa korosho
2.Wakulima wa Mbaazi
3.Watumishi wa umma
4.Wasiokua na ajira
5.Waliopoteza ndugu zao kwa kutekwa na kupotezwa
6.Vyama vya upinzani
7.Wafanya biashara
8.Asasi za kiraia
10.Viongozi wa dini
11.Wanafunzi vyuo vikuu

you will never get an omelet without breaking an egg.

Back
Top Bottom