Haya mambo kila napokumbuka Machozi yananitoka.Watanzania wa sasa sio wale nliokuwa nawasikia nilipokuwa Ulaya na Marekani

Kiduku Lilo

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Messages
962
Points
1,000

Kiduku Lilo

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2018
962 1,000
Last week nlikuwa nmekaa sehemu na jamaa yangu Uswege. Yeye ni mwenyeji kidogo Dar. Akanambia "Billman twende leo ukale nyama choma ya ukweli mitaa flani" siku hiyo nilikuwa natumia Ile GMC nliwaambia.nikamwambia aendeshe.maana nlijua anataka aendeshe naye kidogo gari za ukweli.

Sema ilishindikana maana hii gari nliiisajiri kwa finger print zangu kwa ajili ya security.huweze endesha maana hutaweza ingiza gear.basi hapo akawa hana namna.nikamwambia ingekuwa ile Range ya Kijivu ningemfanyia makeke aendeshe.mi sina hiyana.

Alinikumbusha jamaa yangu pale ofisini siku moja akaomba nimpe ile Ford Ranger naye kidogo asikie anaendesha gari.si unajua ni refu.akashindwa timing akakwaruza toyota ya mtu mmoja ile toyota ikakwanguka kidogo.

Mwenye toyota akaja juu kashuka macho yamemtoka kuja kwenye gari yangu.nlimuuliza tu tsh ngapi kupiga rangi akanambia sijui nini nini akataja tsh 50,000. Nikajua huyu kataja hiyo kidogo sababu tu ya mshtuko.basi nikavuta draw nikampa tsh 300,000. Nikamwona kabisa katoa macho kwa mshangao.

Nlimwomba samahani nikamwambia Ally tuondoke zetu.toyota yake ilikwaruzika kama tu urefu wa kidole hivi pembeni.si sana.

Basi tumekaa sehemu ya nyama choma nlishangaa jamaa wanachoma nyama nzuri sana ya mbuzi.very delicuous. Halafu bei rahisi tu kilo moja ya nyama ya mbuzi 20,000 nikaagiza walete kilo mbili na ndizi za kukaanga.ndizi moja wanauza tsh 5,000. Jamaa wana bei poa sijaona.mimi napenda kupiga msosi so nikawaambia walete ndizi 6 kwangu na Ally naye akaagiza aletewe.naye kilo moja ya nyama na ndizi 4. Kila ndizi tsh 5,000.

Tumekaa tunasubiri msosi mara nikamsikia jamaa anamfokea vibaya sana Mhudumu. Jamaa nlimshangaa mwanaume mzima anadai change tsh 7,500? Mpaka anamkashifu dada wa watu kwa maneno mabaya sana.

Watanzania nlikuwa nawasikia ni watu waungwana ila kumbe siyo.nliumia yaani tsh 7,500 tu ndo umwite mtu mzembe?

Nlimwita yule dada nikampa tsh 10,000 amrudishie jamaa bwege.mwanaume huwezi dai tsh 7,500 hata siku moja.sisi kwetu ni taboo kabisa.

Basi maskini nikamwona dada wa watu hana raha kabisa.ili kumwondolea mawazo nikaenda kwenye gari nikachukua tu 100,000 nikamwambia angalau naye akimaliza kazi anywe anywe kidogo.

Yule dada alitaka hata kunikumbatia.nlishangaa sana. Nikawaza kama ngempa pesa si angenikiss kabisa?maana pale nilimpa tu hela.

Basi baadaye tunaaga yule dada akaomba namba yangu ya simu maskini.nikampa.ila nliumia wanaume tumekuwa wakatili sana mtu kabisa anadai tsh 7500? Hii unadai ukafanyie nini?imenitesa sana hiyo hali.umaskini ni mbaya sana.

Leo nmepata muda baada ya kutoka hotel flani nyota tano kupata dinner.kuna mdada wa usafi kazini leo ni birthday yake.so nikaona nimtoe yeye na boyfriend wake na marafiki zao wakale na kunywa pale hotelin.ame enjoy sana na wenzie.basi nikawa nmerudi home ndo nikawa naangalia JF.

NMESIKITIKA MPAKA KUTOKA MACHOZI.JAMAA KABISA ANASEMA ANATAKA KUMNUNULIA MAMA YAKE TOYOTA. Nikawaza sana. Kweli jamaa kaona ndo zawadi ya kumpa mama yake ni Toyota? Kwa nini asingejichanga hata akamnunulia gari kama Evogue au BMW ? why amnunulie Toyota? Na Magari yapo?

Mi nakumbuka kipindi hicho mwaka juzi namnunulia mother JEEP mpya toka kwenye karatasi ya mwaka huo huo 2017. Alifurahi sana.sasa nawaza jamaa hataki mama yake pia afurahi?

Nmeumia sana.vijana tuwapende wazazi.wakati huo anamnunulia mama yake Toyota unaweza kuta yeye ana Gari. Hata wazazi wanapenda Magari jamani wanunuliwe tu.siyo kuwanyanyapaa kwa kuwanunulia Toyota. Hizi Toyota si ndo hata kuna pikipiki zake za Toyo? Nmeona wana pikipiki za miguu miwili na mitatu zinaitwa Toyo.

Vijana tujitume,tutafute pesa tuwasaidie watu wasio nazo.maisha yenyewe mafupi haya.hasira za nini na kutokwa povu kwa mambo madogo tu?
 

Forum statistics

Threads 1,382,646
Members 526,426
Posts 33,832,678
Top