Haya mambo huwezi amini yanatokea katika Taifa lenye wasomi halafu hakuna anayehoji

TRA walikuja na utaratibu mzuri wa kutangaza makusanyo ya kila mwezi, utaratibu ambao ulianza mwaka jana mwishoni.

Kama mtakumbuka,awali walikuwa wanatupa mchanganuo wa makusanyo hayo kutoka kwenye vyanzo vikuu mbalmbali.

Kwa mfano,walikuwa wakituonyesha ni kiasi gani wamekusanya kutoka vyanzo mapato ambavyo havihusishi kodi kama vile faini za barabarani,n.k

Pia walikuwa wakitupa mchanganuo ni jinsi gani fedha zote zilizokusanywa zitatumika.


Cha kushangaza,utaratibu huu ukasitishwa ghafla na badala yake tukawa tunapewa tu taarifa kuwa mwezi huu tumekusanya kiasi fulani bila mchanganua wa mapato na matumizi.

Cha kustaajabisha hakuna anaehoji sababu za kubadili utaratibu huu wakiwemo waandishi ambao huitwa na kupewa taarifa hizi na TRA waandishi ambao tulitaraji wangehoji kwa niaba yetu.

Cha kushangaza zaidi hata wanasiasa wa upinzani na wasomi wa nchi hii nao hakuna anaehoji!!

Yote tisa. kumi ni ya mwezi uliopita (mwezi November) ambapo hata mapato yake hayajatangazwa na hakuna sababu zilizotokewa lakini nchi nzima kimyaaa!!!!!

Si wanasiasa,si waandishi,si wasomi wote kimya isipokuwa members wa JamiiForums tu kupitia Jukwaa hili la siasa ndio wanaojaribu kuhoji.

Sasa najiuliza sisi ni taifa la watu wa aina gani?

Je,tumekataa tamaa?

Ni waogo?

Ukimya huu unatusaidia au ndio unawaongeza nguvu wenye mamlaka kufanya watakavyo?

Au hatuhoji kwasababu tu utaratibu huu haukuwa wa kisheria?Inaangia akilini kweli?

Mzee Kenyata huenda alikuwa sahihi kama kweli alisema maneno yale.

Kweli wa kuhoji haya ni watumiaji wa JamiiForums tu?!

All I can say is that,some people would be happier if JamiiForums never existed and perhaps they wish so.
Umesikia mjomba , kuna msemo unasema hivi , Ngoma ya watoto haikeshi .
 
Hela zitaendelea kuadimika hadi makanisani - Magufuli

Kuna makusanyo hapo ?
Kuna tatizo hapo?Mana yake yale mafisadi yaliokuwa yanatoa fungu la kumi kwa hela za wizi,hawataweza tena kupeleka pesa kanisani.Mfano mzuri tu ni lowassa hakuna tena michango ya milioni 100 makanisani kama zamani
 
Back
Top Bottom