Haya makundi matatu, moja litawakoa wagonjwa kwa kukubali yaishe

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,442
Katika vuta nikuvute ya Serikali na madaktari inahusisha makundi matatu. Kuna 1(Rais), 2(Madaktari) na 3(Mawaziri yaani Nkya, Mponda).

Ninaamini mgomo uliotishiwa kuanza leo ukitekelezwa utapelekea vifo vya watu wengi kama uliopita. Kwasababu hivi vifo vinaweza kuzuilika iwapo kundi moja litawaonea huruma wagonjwa wasio na hatia. Kwa mfano Madaktari wakisitisha mgomo wao watu wataendelea na matibabu kama kawaida, lakini wakiendelea na msimamo wao Rais anaweza kuwasimamisha hawa mawaziri watu waendelee na matibabu kama kawaida, lakini pia Rais akiendelea na msimamo wa kuwalinda hawa mawaziri, Waziri Mponda na Nkya kwa kuwaonea huruma binaadam watakaokufa kutokana na mvutano huu wanaweza wakaacha kazi ili waokoe uhai wa binaadam kwani uwaziri kitu gani mbele ya uhai wa binaadamu??. Sasa Ninaamini katika haya makundi matatu siyo wote wana roho ya kiuaji, Sisi binaadamu naturally ni wabinafsi lakini katika hili ninaamini hatakufa mtu kwani sidhani kama Madaktari,Kikwete, Mponda na Nkya watakubali watu wafe ili wao washinde katika mvutano huu.
 
Makundi yanayotakiwa kuwahurumia wananchi kutokana na athari za mgomo wa mafoc ni mawili tu!Rais & waziri & naibu waziri.Madoc wanadai haki.
 
Msitegemee kuwa huyo mkweree ndiyo atawaokoa hao wananchi wasife katika sakata hili kwani kama alivyoonesha kwenye mgomo wa kwanza yeye hajali maisha ya wananchi bali maslahi yake tu na ndio maana mgomo ulipoanza mara ya kwanza akakwea pipa akaenda kustarehe DAVOS kwenye mkutano ambao ulimletea aibu kubwa yeye binafsi kwa kushindwa kujibu maswali!! Msitegemee la maana toka kwa Vasco...!
 
Rais ndie mteuzi wa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Mganga Mkuu wa Serikali. Katibu Mkuu na Mganga Mkuu waliposimamishwa naamini Rais aliafiki. Iwapo Waziri na Naibu wake hawa kusimamishwa ni kwa sababu hawahusiki au wana imunity gani? Hili ni kosa la kiutawala linalosababisha makosa mengine yajitokeze kama la kumpa Rais masaa 72 kuwatimua kazi Ponda na Nkya! Hata kama ni dhahiri hawafai si sahihi kutoa mashinikizo ya namna hii.
 
Kipo bora kutokutii shinikizo la kipuuzi na au kuokoa uhai wa watu wasio hatia????
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom