Chimunguru
JF-Expert Member
- May 3, 2009
- 10,678
- 4,350
Eh Bwana mdogo. msingi wa utani wa makabila ni vita hapo zamani wakati makabila yalipokuwa yanahama. kulitokea uhasama kati ya makabila mbayo ni watani wenye nguvu waliahama sehemu walipokuwa wakiwaachia wageni au wageni walishindwa na kuendelea na safari, hivyo kuleta hisia za kudharauliana na kuanza kutaniana, aidha makabila mengine ilikuwa ni dhuluma za biashara mfanao wasumbwa na wahaya- hawa wasumbwa walikuwa wanasafirisha chumvi na kuwauzia ila kwa kuangalia tofauti ya tamaduni zao wakaanza kutaniana. makabila mengine ni majirani walitaniana kwa kudharau baadhi ya tamaduni na mila tofauti. kwa kifupi ni hayo
Mmewahi kuwasikkiai Wadoe (wanapatikana Bagamoyo), wanatania kila kabila...
sijawahi kuwasikia hao. wanafanana akili na wakwere?
Mngekuwa na ubavu wa kuwapiga wahehe si mngelinga? wahehe ndo kabila lenye nguvu kushinda Yote kusini mwatanzania na tanzania kwa ujumla na ndo kabila pekee lenye historia ya kumpiga mjerumani, na ndo maana wangoni mkaungana na mjerumani kuja kupigana na wahehe.Hii ilitokana na vita vya enzi hizo za mababu zetu, mfano wangoni walipoingia Bongo toka South, waliingia Sumbawanga wakapiga kule, wakapita Tabora wakatwanga wanyamwezi na wasukuma, Iringa furusha wahehe, na wabena halafu ndo waka settle SONGEA/RUVUMA. sasa huko walikopita kote hawa sasa hivi ni watani wa WANGONI- Wafipa, wasukuma, wanyamwezi, wahehe, na kuna makabila menine madogo madogo na si strategy ya Nyerere wala mtu binafsi hii ni HISTORIA.
Wakurya ni wajukuu wa wahaya, kwa hiyo hata iwe vipi babu / bibi hawezi mdharau mjukuu. Na mjukuu hawezi chukizwa na utani wa babu/bibi.
Huo ujukuu ulianzaje? na kwanini wakurya hawana dharau na majivuno kama wahaya?
Thibitisha hitimisho lako la kuwa wahaya wanadharau na majivuno. Je wajua kuwa babu /bibi na mjukuu wanaweza kuwa na tabia tofauti kulingana na mazingira?
Mleta mada tambua kwamba there is no one who can make you inferior without your permission. Kwahiyo suala kwamba wahaya wana dharau ni kutojiamini kwako kutako kufanya ujisikie unadharaulika.